Download hapa katiba ya Chama Cha Kijamii (CCK)

hahaaaa! nyani bana huwa haoni................???? wewe hujioni ulivyo mpiga debe wa magamba??? nasikia mabosi zako akina nape,sitta,na wengineo wanatembea wakiwa wamejipaka mafuta ya kuzuia sumu mikononi!! heheeeee! na wewe chunga watakulisha!

we mpemba upo??VIPI HR NA MAALIM WAMEPATANA HUKO AU??
 
Husna naomba unitumie namba yako ya simu (Tongue in cheek). BTW hii CCK sio Prototype ya CCJ?

Serious kabla hata sijasoma katiba yenu (because most of katibas za vyama ni nzuri including our evil party CCM).
Mimi ninataka kufahamu msimamo wenu wakati huu tete wa kuandika katiba mpya.
  1. Muundo wa Muungano
  2. Madaraka ya Rais wa JMT
  3. Kuwepo/kutokuwepo kwa wabunge wa viti maalumu
  4. Kuwepo/kutokuwepo kwa RCs DCs
  5. Mameya wa majiji kuchaguliwa na madiwani
  6. Tume huru ya uchaguzi (muundo na upatikanaji wa wajumbe wake)
  7. Matokeo ya kura za Rais kutohojiwa na chombo chochote kile
  8. Wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri
  9. Uteuzi wa CJ, CDF, IGP, Wakuu wa mashirika nyeti ya umma kufanywa na Rais pasipo kuidhinishwa na chombo chombo chochote kile au nafasi hizo zitangazwe na kugombewa kulingana na qualification
  10. Muundo wa SMT kuwa na Rais, VP, PM ni sahihi
Ukinijibu haya machache labda yanaweza kunipatia/kutonipatia hamu ya kusoma katiba yenu.

Nyongeza katika hayo;
11. Nini msimamo na watafanya nini kuondoa utaratibu wa kuwahoji wabunge kama wanaunga mkono ama la kwa kusema Ndiyo au Siyo?
 
...hakuna mwenye akili yeyote anayeweza kukubali kuwa CCK ni chama,maybe mngeiita NGO

nadhani chadema ndio inapaswa kuwa NGO,tena haihitaji hata elimu ya darasa la nne kuliona hilo,acha uhaba wa akili
 
Husna naomba unitumie namba yako ya simu (Tongue in cheek). BTW hii CCK sio Prototype ya CCJ?

Serious kabla hata sijasoma katiba yenu (because most of katibas za vyama ni nzuri including our evil party CCM).
Mimi ninataka kufahamu msimamo wenu wakati huu tete wa kuandika katiba mpya.
  1. Muundo wa Muungano
  2. Madaraka ya Rais wa JMT
  3. Kuwepo/kutokuwepo kwa wabunge wa viti maalumu
  4. Kuwepo/kutokuwepo kwa RCs DCs
  5. Mameya wa majiji kuchaguliwa na madiwani
  6. Tume huru ya uchaguzi (muundo na upatikanaji wa wajumbe wake)
  7. Matokeo ya kura za Rais kutohojiwa na chombo chochote kile
  8. Wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri
  9. Uteuzi wa CJ, CDF, IGP, Wakuu wa mashirika nyeti ya umma kufanywa na Rais pasipo kuidhinishwa na chombo chombo chochote kile au nafasi hizo zitangazwe na kugombewa kulingana na qualification
  10. Muundo wa SMT kuwa na Rais, VP, PM ni sahihi
Ukinijibu haya machache labda yanaweza kunipatia/kutonipatia hamu ya kusoma katiba yenu.

Bobuk,chama chetu bado ni kichanga na ndo kwanza tuko katika harakati za kujipanga,Hivi sasa navyoandika technical commitee ya chama imejifungia kufanya mjadala mkubwa juu ya mambo mbalimbali ya kiseralikiwemo swala lamuungano ili kufikia maamuzi ya pamoja juu ya sera ya chama kuhusu muungano.

zingatia maombi yako yote kuhusu madaraka ya rais,wabunge wa viti maalum,tume ya uchaguzi,nk yote yapo katika mjadala wa ndani ya chama
 
Usife moyo kutokana na kauli za ovyo ovyo za baadhi ya watu humu JF kwani uanachama wa JF hauna mchujo. Watu wenye akili timamu wanatakiwa kukupinga kwa hoja, sio kejeli na matusi.

Lakini pia jitahidi sana kujibu hoja za msingi zinazotolewa humu, la sivyo jitihada zako humu hazitazaa matunda.

Vinginevyo umefanya jambo la maana sana. Hongera na kila la kheri.

Ni kweli bwana mchambuzi,kuna watu wanaudhi sana bila kutambua haki yetu ya kikatiba ya kuanzisha chama,tumewapuuza na tunasonga mbele,iko siku watatuelewa!
 
Kila mtu akitaka madaraka anatumia sentesi "tumaini/ matumaini mapya kwa watanzania" mwisho wa siku hakuna mabadiliko yeyote..kifupi ww na matapeli wenzio mnaoanzisha chama kipya ni wale wale tu!!!

nadhani tungekuwa matapeli serikali isingetupa cheti cha usajili wa kudumu,na kwa bahati mbaya inaonekana hujui hata taratibu zinazotumika kusajili chama,tunakuonea huruma sana!
 
Ngoja tuisome vizuri,sasa mkuu naomba ulijibu hili kwenye kituo kimoja wewe pamoja na katibu wako mlisema serikali ifute rudhuku kwenye chama,sasa we unafikiri vyama vitajiendeshaje? Si ndio vitakua mali zenu sasa?

jambo la kujiuliza ni kuwa ruzuku imetusaidia nini? zaidi ya kuleta migogoro isiyokwisha kwenye vyama,kutokuwajibika kwa wananchi,uvivu wa kufikiri na kubuni miradi ya kujiendesha,lakini ruzuku ikiondoka vyama visivyotokana na watu vitakufa na vitabaki vyama vyenye mtazamo wa kujali maslahi ya watu ambapo watu wenyewe wataguswa katika kuvisaidia na kuviendesha na demokrasia ndani ya vyama itaanza kuonekana
 
Kwako Mhusika wa CCK humu Jamiiforums:

Huu ni mwanzo mzuri sana kwa CCK, haswa kitendo cha kuiweka katiba yenu hadharani ili mpate mawazo. Katiba za CCM, CUF, NCCR, CHADEMA, hazikuchukua mawazo ya wananchi. Hakika hii ni dalili kwamba hiki ni chama cha wananchi. Mimi ni mwana ccm lakini naamini katika ushindani wa hoja, sio uadui wa kisiasa, kwani mwisho wa siku, taifa huja kwanza kabla ya vyama. Nina maoni machache kuhusu katiba yenu kama ifuatavyo:

1. Kwanza ni pale mnaposema mnasimamia haki na maslahi ya makundi yafuatayo: wakulima, wafugaji; wafanya kazi wote. Lakini kwenye wajasiriamali mnasema “inapobidi”. Hii ni hatari kwa sababu kuu mbili:
Moja – inaweza kutoa tafsiri kwamba nia ya CCK ni kuwaacha wajasiriamali wapambane wenyewe na nguvu za soko, ambalo tumekwishaona huko Mbeya, Mwanza, na hata DSM jinsi gani nguvu hii inawapa tabu wajasiriamali wadogo wadogo, ambao asilimia karibia 70 ni vijana. Na vijana ndio nguzo muhimu ya chama chochote cha siasa Tanzania i.e. asilimia 70% ya watanzania hawajavuka miaka 30, na asilimia 60 ya wapiga kura Tanzania ni vijana wa kati ya umri wa miaka 16 na 35. Hakikisheni hamtoi tafsiri kwamba mnawatupa hawa.

Mbili – hatari ya pili ya kuzungumza suala la CCK na ujasiriamali katika hali ya ‘ikibidi’, ni kwamba, kwa hali ya sasa, mfanyakazi, mkulima, mfugaji, pia ni mjasiriamali kwa njia moja au nyingine. Inawezekana CCK mnajaribu kukwepa hali ya Chama kutekwa na wafanyabiashara au kuonekana ni chama cha wafanyabiashara kama ilivyo CCM, lakini ukweli unabakia wazi kwamba ili CCM, Chadema, NCCR, CCK wafanikiwe, lazima wawe na ukaribu sana na wafanyabiashara. Ni muhimu kwa vyama kukwepa hilo ‘kisiasa’, ila sidhani kama ni sahihi sana kuliweka kama inavyosomeka kwenye hivi sasa. Jaribuni kulitafutia maneno mengine ya kufikisha ujumbe huo huo mnaokusudia.

2. Katika itikadi mmelenga pazuri, kwani ni ‘unique’ from CCM, CDM n.k. Itikadi hii pia ipo more practical na pia realistic kwa mazingira ya wananchi walio wengi. Vyama vingine havionyeshi jinsi gani vitamkomboa mtanzania kutoka kwenye soko huria lililokuwa so unfair kwa maskini. Havitoi tafsiri kwa wananchi kwamba wapo tayari kukaa meza moja na maadui watatu wa Maendeleo na kufikia makubaliano juu ya masuala ya Maendeleo, na badala yake tafsiri ni kwamba wote wanashindana kwenda ikulu kutekeleza yale yale ya maadui hawa kaka yalivyo bila kuhoji: WorldBank, IMF na WTO. Hili suala ni muhimu sana kwani ni wadudu hawa watatu ambao wamemwacha Mtanzania ameduwaa ndani ya soko huru. Na kama mnamthamini Nyerere, jaribuni kuweka mkazo hapa. Lengo sio kuwafukuza hawa bali kuweka msimamo badala ya kuwakenulia kama inavyofanya CCM na Chadema kwa sasa.

Lakini katika malengo na madhumuni – CCK inasema kwamba “itahakikisha shughuli za uchumi haziruhusu ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi kwa manufaa ya watu wachache binafsi”. Itikadi yenu ya Social Economic Conservatism haiwezi shamiri bila kukubali ubepari ambao mtaji wake mkubwa ni umiliki binafsi wa mali. Mnachotakiwa kuonyesha kwamba mnaukubali ubepari na soko huria, ili mradi muwe na uwezo wa kukemea vitu hivi pale vitapomkandamiza maskini. Vinginevyo moja ya criticisims kubwa wanazopata Social Democrats ni kwamba wana restrict sana individual rights, sana sana economic freedom kutokana na kuwa na an intrusive government. CCK inatakiwa kukimbia hoja hii kwa kufafanua hicho kipengela cha “mali na njia kuu za uchumi” kwa lugha ambayo itatoa tafsiri nzuri kwa mfano kwamba CCK inaamini katika soko huria n.k, ili mradi kunakuwa na involvement ya serikali katika uchumi nia kubwa ikiwa ni kuzuia unequal distribution of resources n.k, kwani mnaamini kwamba kufanya hivyo kutapelekea uwepo wa soko huria lenye faida kwa wengi n.k. katika maelezo yenu, ionekane kwamba restrictions of individual rights ni muhimu katika kufanikisha hilo i.e. kufanya ‘soko’ liwe fairer kwa kila mtu.

Pia kwenye itikadi ni vizuri muweke msisitizo kwenye imani ya chama kwamba mnaamini itikadi yenu ndio njia pekee ya kujenga jamii mnayoitaka au envision kama CCK. Asset kubwa na unique katika Jina la CCK ni “JAMII”, itumieni vizuri hii.

3. Kuhusu ukomo wa mwanachama:
Sijaone maelezo kuhusu ni kikao gani kinahusika na hili. Inawezekana imeelezwa kwenye katiba lakini nikapitiwa. Pia sijaona sehemu inayoelezea iwapo mtu atafukuzwa uanachama, ataendelea kuwa mwanachama kwa mfano kupitia vitengo vingine kama vijana, wazee, wanawake?

4. Kuhusu Miiko ya uongozi – hili halijazungumzwa. Ni muhimu kwa sehemu juu ya sifa za uongozi ziendane sambamba na miiko ya uongozi. Suala la ‘hasi na chanya’

5. Pia ni muhimu mkazungumzia ngazi ya JIMBO kama mlivyofanya kuhusu Shina, Kata/Wadi, Mkoa na Taifa. Ngazi ya majimbo ni muhimu sana katika shughuli za chama.

6. Na mwisho ni ushauri tu kwamba CCK kianzishe utamaduni wa kuchapisha literature mbalimbali mfano mipango ya CCK kati ya sasa na mwaka 2015 n.k. Chama pia kije na mwongozo, lakini muhimu zaidi kwa sasa ni kuja hata na vipeperushi vidogo tu vya rangi, hata kurasa hata moja, vinavyoelezea kwa muhtasari kuhusu CCK, huku pakiwa na kauli mbiu ya CCK ambayo ni ‘catchy’, ‘inspiring’, ‘easy to remember’ and ‘unique’ from other parties. Chadema, CCM, CUF hawatumii mbinu hii ambayo ni very powerful. Badala yake, huwa wanasubiri wakati wa uchaguzi mkuu, na kupelekea hali ya wananchi kuchananyikiwa kutokana na idadi ya vipeperushi kutoka vyama mbalimbali. Kauli mbiu yenu ya sasa ni nzuri: 'mabadiliko ni sasa, mabadiliko ni sisi'

Ni hayo machache niliyoyabaini kwa haraka haraka.

kwanza hongera na tunashukuru kwa namna ambavyo unatoa mawazo yako,wewe ni mzalendo na una kila dalili ya kuwa unaipenda nchi yako,maoni yako ni ya msingi na tunayafanyia kazi,katiba yetu ni ya muda na itapitishwa na mkutano utakaofanyika miezi takriban kumi na moja ijayo.Mungu akubariki sana
 
Wametumwa hao.....Hebu ona aliyewatuma CCJ-CCK haya twendeee CC-JK .....maandalizi kama gamba likigoma kuvuka akimbilie huko
 
WATANZANIA GANI WALIOWATUMA NA WKO WANGAPI KILA MKOA WANAOWAUNGA MKONO??

JE NI KWELI KUWA MWAKYEMBE,SITTA,NAPE,ANNA KILANGO,LEMBELI ,NA KIMARO NDIO VIONGOZI HALISI WA CCK,KAMA SIO IKITOKEA MBELENI WAKAJIUNGA NA KUSEMA WAO NDIO WALIOKIANZISHA UTARUDI HAPA NA KULA MATAPISHI YAKo??

Simple mind nornally discuss people, modarate mind discuss events, but GREAT MIND ALWAYS DISCUSS IDEAS AND CHANGES
 
Back
Top Bottom