DOWANS vs TANESCO - Why TANESCO Lost?

DOWANS vs TANESCO - Why TANESCO Lost?

Baada ya kuzisoma zote na kuzimaliza inasikitisha na kuhuzunisha kodi yangu inaliwa na watu wachache Tanzania. Kwa kusummarize niliyoyaona katika hii documents kwanza natanguliza shukrani kwa invisible kwani hii inatoa picha halisi mambo yanavyokwenda nchini. Pili ninaweza kusema machache kutokana na kesi hii kuwa uzembe, mafia network, kukurupuka kumechangia sana kwa sisi kufika hapo. Tatu hii pesa hakuna jinsi italipwa tu maana ikikaa jamaa wanachaji interest mwisho wa siku tunaweza kujikuta tunadaiwa Trilioni kadhaa na serikali ikashindwa kulipa ikabakia kuuza rasilimali zake kwa wanaotudai (Na ndio lengo la hawa wakubwa).

Ukiangalia mtiririko wa kesi ni kwamba Dowans wamerithi mkataba wa Richmond na Tanesco. Kiukweli ukisema defence ya Dowans ni kwamba ule mkataba katika macho ya sheria ni mkataba uliokuwa sahihi kabisa kwani una vigezo vyote vinavyouita a valid contract. Kwamba Richmond ni briefcase company hilo ni jambo lengine kwani kipengele cha mkataba sahihi hakuna kipengele kinachozungumzia mazingira ya kampuni ya mfukoni sheria iko vp (Nadhani hili somo kwa wanasheria wetu warekebishe hicho kipengele ili kiaccomodate hilo otherwise tutaumizwa tena tu na wajanja). Hivyo kisheria huo ni mkataba sahihi hatuna jinsi.

Tukija katika Dowans na POA ya RA ni vema waungwana mkafahamu kuwa Dowans wamerithi mkataba na urithishwaji wao ni valid kabisa na hivyo basi hata kama mtasema Dowans ni kampuni ya mfukoni ni vema mkajiuliza je tuna haki hapa? Sasa basi huu ni uzembe wa wanasheria wetu wakati wanasign mkataba hawakuupitia vizuri kwani wangeliweka clause kuzuia transferability ya mkataba tusingelikuwa tunazungumza haya sasa (au pengine walishapewa mshiko wao ndio maana wakajifanya wameoverlook who knows!!!) Sasa kwa mujibu wa hii kesi Dowans wana haki ya kudai compensation kwa kuvunja makubaliano unless kama Tanesco wangelifanya makubaliano ya kumaliza haya maswala nje ya mahakama ndio ingelikuwa ishu nyengine.

Kwa kumalizia ni RA na wenzie wametuingiza mjini hapa na wanasheria wetu wanatakiwa kujiuzulu pamoja na menejimenti ya Tanesco. Vilevile wale wote waliosign mkataba huu wafikishwe mahakamani kwa kulitia taifa hasara maana sijawahi kuona mkataba wa ovyo kama huu ambao mtu anaruhusiwa kutransfer mkataba kwa mtu mwengine bila kushirikisha upande wa pili ni jambo la kushangaza. Vilevile sidhani kama inawezekana hii kesi ikawa appeal maana wao wamerely katika Laws of Tanzania , ila wanaweza kufungua kesi ya udanganyifu kwa Dowans kuwa ni kampuni feki ila sijui kama nia hiyo ipo ikisha wawadai fidia ya mabilioni ya fedha kwa hasara (kwani hata ICC wamesema kama wangelifanya utafiti vizuri Tanesco ingelikuwa na valid defence of misrepresentation and falsity) hivyo basi wanaweza kuwatingisha huko ikawa kesi tamu.

In the end I am sad to say hizi pesa zitalipwa to waungwana hakuna janja hapa na kodi yangu italiwa ila wanaweza kufungua kesi ya udanganyifu halafu hela zetu zikarudia kwa njia hiyo. Nimekasirika sana hata maji leo sitaki nimesusa!!!!
 
Kwa kumalizia ni RA na wenzie wametuingiza mjini hapa na wanasheria wetu wanatakiwa kujiuzulu pamoja na menejimenti ya Tanesco. Vilevile wale wote waliosign mkataba huu wafikishwe mahakamani kwa kulitia taifa hasara maana sijawahi kuona mkataba wa ovyo kama huu ambao mtu anaruhusiwa kutransfer mkataba kwa mtu mwengine bila kushirikisha upande wa pili ni jambo la kushangaza. Vilevile sidhani kama inawezekana hii kesi ikawa appeal maana wao wamerely katika Laws of Tanzania , ila wanaweza kufungua kesi ya udanganyifu kwa Dowans kuwa ni kampuni feki ila sijui kama nia hiyo ipo ikisha wawadai fidia ya mabilioni ya fedha kwa hasara (kwani hata ICC wamesema kama wangelifanya utafiti vizuri Tanesco ingelikuwa na valid defence of misrepresentation and falsity) hivyo basi wanaweza kuwatingisha huko ikawa

Mkuu mimi siyo mwanasheria ila nakumbuka kuna sehemu kwenye hiyo ruling, appeal kama haina nafasi. The decision was final! Nilielewa au ignorance ilichukua nafasi?
 
lakini mtu yoyote mwenye akili huwezi kwenda kwenye abitration ambayo mwisho wa siku haikupi chance ya ku-appeal . sema kwa sababu serikali kupitia hiyo tanesco walijipanga kushindwa ndio maana wakajipeleka kichwa kichwa na utetezi goi goi ili kufanikisha walicho kuwa wanata. nacho ni kuilipa dowans

Na mimi nimeona kwamba ni upuuzi. yaani appeal haipo!
 
Thank you big man the docs are very informative for us who sources of informations are inferior! Considering that i have never seen PM signature b4 but through the doc.
 
Mkuu mimi siyo mwanasheria ila nakumbuka kuna sehemu kwenye hiyo ruling, appeal kama haina nafasi. The decision was final! Nilielewa au ignorance ilichukua nafasi?

Mkuu,

ICC wakiamua ndio mwisho ila wanaweza kufanya kama walivyofanya kuna kesi moja ya France waliquestion the independence of one of the judge in the France court of appeal. Sasa naona kama kuna mganda hapa kwenye hii case kama ana any connection na RA (Kwa vile amehamishia investment zake huko) kunawezekana kukawa na some conflict of interest (if any) sasa this is just a hunch... Njia ya uhakika ni kuwafungulia kesi Dowans (counter argument ya udanganyifu) then kuwadai fidia ili waombe solution nje ya mahakama tupunguze hilo deni.

Otherwise hii kesi hakuna jinsi tutalipa tu sijui pengine kunaweza kuwapo huo upenyo but Arbitration judgement nyingi ni final hakuna appeal.
 
Mdondoaji said:
In the end I am sad to say hizi pesa zitalipwa to waungwana hakuna janja hapa na kodi yangu italiwa ila wanaweza kufungua kesi ya udanganyifu halafu hela zetu zikarudia kwa njia hiyo. Nimekasirika sana hata maji leo sitaki nimesusa!!!!
Mkuu,

Kabla hujakasirika kiwango hicho, hivi waweza kunisaidia? DOWANS walilirithi mkataba huu toka kwa 'kampuni hewa' ya RICHMOND, sasa kwa mawazo yangu ni kuwa "hakuna mkataba" au TANESCO/Serikali waliingia mkataba mpya na DOWANS? Kivipi na kwanini?

Baada ya kugundua kuwa RICHMOND ilikuwa "FAMBA" bado wanasheria wetu wa TANESCO waliendelea kuiacha serikali na shirika letu kuingia mkenge mwingine kama huu?

Kutojua sheria kunatusababishia wengine kushindwa kuelewa kwanini kila kitu kimeenda hivi, enlighten me please
 
Hapa ngoja nikeshe Nayo ngoja ninywe na Kahawa kabisa hapa
 
Mkuu,

Kabla hujakasirika kiwango hicho, hivi waweza kunisaidia? DOWANS walilirithi mkataba huu toka kwa 'kampuni hewa' ya RICHMOND, sasa kwa mawazo yangu ni kuwa "hakuna mkataba" au TANESCO/Serikali waliingia mkataba mpya na DOWANS? Kivipi na kwanini?

Baada ya kugundua kuwa RICHMOND ilikuwa "FAMBA" bado wanasheria wetu wa TANESCO waliendelea kuiacha serikali na shirika letu kuingia mkenge mwingine kama huu?

Kutojua sheria kunatusababishia wengine kushindwa kuelewa kwanini kila kitu kimeenda hivi, enlighten me please

UWEZEKANO NI MKUBWA wale wanasheria wa TANESCO wamepewa rushwa wafunge mdomo.
 
Sina cha kusema zaidi ya kubadili fani na kusoma sheria maana mambo mengi yanafanywa kiholela tu na wanasheria wanaangalia tu na kubaki kupiga makelele badala ya kuchukua hatua!
 
Hey people don't give up,we're over 39 millions citizens we can decide not to pay, if we want to and no one can stop us but if we sit our asses down and talk like parrots then we gonna pay dearly,I think it's high time now we do things collectively...they can't kill us all
 
kaka asante sana tunashukuru kwa kututendea haki watanzania wenzako! Kama kuna mengine mengi tunayaomba tuzidi kuwajua wabaya wetu.
 
Mkuu,

Kabla hujakasirika kiwango hicho, hivi waweza kunisaidia? DOWANS walilirithi mkataba huu toka kwa 'kampuni hewa' ya RICHMOND, sasa kwa mawazo yangu ni kuwa "hakuna mkataba" au TANESCO/Serikali waliingia mkataba mpya na DOWANS? Kivipi na kwanini?

Baada ya kugundua kuwa RICHMOND ilikuwa "FAMBA" bado wanasheria wetu wa TANESCO waliendelea kuiacha serikali na shirika letu kuingia mkenge mwingine kama huu?

Kutojua sheria kunatusababishia wengine kushindwa kuelewa kwanini kila kitu kimeenda hivi, enlighten me please


Mkuu,

Kwanza la kusikitisha ni kwamba wanasheria wanafahamu fika kutokujua sheria (negligence) is not a defence for failure to exercise due diligence. Sasa kama walidhani wanatumia kigezo hicho kama defence ni kichekesho. Pili mkuu hebu soma hii kutoka katika hukumu yao nanukuu:-

Para 519:-

Tanesco alleges that these representations were false. However based on the evidence adduced before the tribunal the representations were of fact true........................ Malizia hadi mwisho but mkuu Richmond na Dowans are in fact companies that were actually registered in US, Costa Rica and Tanzania. Sasa kwa mazingira hayo mkuu ni kwamba hizo ni kampuni na ule mkataba ni mkataba halali. Ingelikuwa Dowans au REDVCO hazipo registered either in one of the areas mentioned then ingelikuwa kesi nyengine kwa hapa na mtiririko wa kesi navyoona mie ni ngumu.

Nikirudia maneno ya jamaa wa ICC Tanesco walitakiwa waexercise due diligence ambapo hawakulifanya hilo na ndio hapo wameumia.
 
Sina cha kusema zaidi ya kubadili fani bna kusoma sheria maana mambo mengi yanafanywa kiolela tu na wanasheria wanaangalia tu na kubaki kupiga makelele badala ya kuchukua hatua!

Mkuu wanasheria makini wapo ila 10% ndio inawazingua si unajua mjini Dar kila mtu anataka aendeshe Vogue mjini na sio Nimrod Mkono peke yake!!!!
 
Hivi kweli mnaamini Wanasheria wa Tanzania walioshiriki kupelekwa huko ICC na kukubali mapema kuwepo vipengele hivyo vya arbitration wakati Tanzania yenyewe inayo Mahakama ya Biashara na utaratibu wa kutatua migogoro ya kibiashara walifanya hivyo kwa sababu hawajui au hawana uwezo?
 
Hivi kweli mnaamini Wanasheria wa Tanzania walioshiriki kupelekwa huko ICC na kukubali mapema kuwepo vipengele hivyo vya arbitration wakati Tanzania yenyewe inayo Mahakama ya Biashara na utaratibu wa kutatua migogoro ya kibiashara walifanya hivyo kwa sababu hawajui au hawana uwezo?

Mzee Mwanakijiji,

Kuna njia nyingi za kisheria za kutatua migogoro katika mikataba. Njia moja wapo ni Litigation (kwenda mahakamani), Usuluhishi (mediation) na Abritration.

Katika dunia ya sasa ya mikataba mikubwa mikubwa watu wengi huwa wanapendelea sana Arbitration (International Commercial Arbitration) kwa sababu hii ndio njia rahisi na ya haraka na inayotoa nafasi kwa parties kupresent case yao bila ya kuwa na technicalities za kisheria ukilinganisha na Litigation ambayo huwa inachukua muda mrefu kesi kumalizina na kuwa na technicality nyingi sana. Lakini pia Arbitration unatoa nafasi kwa mgogoro kupata kusuluhishwa na wataalam katika field husika ya mgogoro na hivyo kutoa usawa zaidi kuliko kwenda mahakamani ambapo majaji wengi wao huwa ni wanasheria tu.

Kama umefuatilia post yangu hapo juu, kitendo cha TANESCO kuchagua Arbitration sio kosa, kosa ni jinsi hicho kifungu cha Arbitration kilivondikwa (Arbitration Clause). Kwa kweli kilivondikwa hata mtoto anaesoma sheria mwaka wa kwanza hawezi kukubali kuandika kifungu cha ajabu kiasi hicho.

Nashindwa kuelewa mawazo ya TANESCO wakati wanaandika au wana negotiate huo mkataba walikua wanafikiria nini kichwani. Sipati picha unakua na kipengele kinachokataza kukata rufaa, kinachopinga kuhoji maamuzi ya Arbitration tribunal. What if Dowans colluded with Arbitrators to get such an Arbitration Award?

Kwa namna yoyote ile kwa sasa hata kama tukienda wapi hii Arbitration Award ni ngumu kuihoji au kukata rufaa manake tayari tumeshafunguwa mikono kwa kifungu cha mkataba...! Katika ushauri wangu nilipendekeza Mwanasheria Mkuu wa TANESCO afukuzwe kazi mara moja. Hapa ndio tatizo lilipo.

Tutaishia kupiga siasa tu lakini hapa hii hela Serikali haina ujanja lazima italilpa tu...! Ukitaka kujua soma sheria ya Tanzania Investment Act. Utaona ni kiasi gani Serikali imejikoroga katika ku-guarantee favourable conditions to Investors. Pia usisahau Tanzania ni member wa MIGA (Multilateral Investment Guarantee Agency). Sasa tusipolipa hawa Dowans najua watatumia mwanya huo kupiga kelele Duniani kuonyesha kwamba Serikali ya Tanzania haiheshimu wawekezaji na hii inaweza ikakimbiza sana wawekezaji na kuiweka Tanzania katika black list ya investment destinations.

You must look this issue with a big picture. Watu wameshaisoma hii issue 1 day ahead of everyone. Hapo ndio utajua kwamba una deal na smart people.
 
....................... Sasa kwa mujibu wa hii kesi Dowans wana haki ya kudai compensation kwa kuvunja makubaliano unless kama Tanesco wangelifanya makubaliano ya kumaliza haya maswala nje ya mahakama ndio ingelikuwa ishu nyengine...........!!!!

Asante sana Mkuu Mdondoaji kwa ufafanuzi zaidi..................Naomba maoni/mtizamo y/wako kuhusu the argument ya kununua ile Mitambo ya DOWANS
 
....................... Ukitaka kujua soma sheria ya Tanzania Investment Act. Utaona ni kiasi gani Serikali imejikoroga katika ku-guarantee favourable conditions to Investors. Pia usisahau Tanzania ni member wa MIGA (Multilateral Investment Guarantee Agency). Sasa tusipolipa hawa Dowans najua watatumia mwanya huo kupiga kelele Duniani kuonyesha kwamba Serikali ya Tanzania haiheshimu wawekezaji na hii inaweza ikakimbiza sana wawekezaji na kuiweka Tanzania katika black list ya investment destinations....................

I agree with you Mkuu.............however.....on a fair ground investor genuine atapingana na HUU UTAPELI WA WAZI WAZI..............huu ni uhalalishaji wa utapeli...................kwenye biashara hizi za investment kubwa kubwa the bottom line ni kuwa both parties wanatakiwa KUNUFAIKA.........kwa kiwango gani? thats another argument.............honestly tuwalipe DOWANS kw amanufaa yepi tuliyoyapata..............Tanzania as a country.........na hata mataifa mengine itakuwa ni shame kuangalia.....eti kwa sababu Mwanasheria wa Tanesco alikuwa Mzembe hivyo.....punishment iwe kwa Taifa............na punishment hiyo haiishii hapo bali ina-effect kwa other INVESTORS.....and in turn ni sisi sis walipa kodi tuendelee ku-pay!!!.............kama kuna investor wanakubaliana na huu UPUUZI basi hakuna ma-Investor Genuine..............

kw ahiyo the point is...........waache DOWANS wapige kelele halafu tuone hayo mataifa.........yatakayo-support...........huu UTAPELI/USHENZI..................ili hao Investors wasije kuingia kwneye matatizo ya UTAPELI kama huu wa DOWANS inabidi nao washiriki kupiga vita utapeli huu otherwise nao watakuwa ni MATAPELI TU.................na hatuwataki............

Angalia biashara BAE na kesi yake kwa Tanzania............ingawaje iliamuliwa kinamna fulani ya kuikingia BAE.....lakini unaona ni jinsi gani people think about VALUE for Money..........hivi kwa DOWANS tutasema value for money ikoje/iko wapi
 
Invissible, hiyo PART I siwezi kui download...nadhani kulingana na configuration yangu ya mtandao...naomba uiweke kama PART II. Asante,
 
Back
Top Bottom