WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 970
Tatizo hapo sio Mkataba mbovu au Mkataba Mzima. Tatizo hapo ni umeme! Umeme leo Tanzania hatuna wa kututosha na wakati wa kuingia hii mikataba tulikuwa desperate, Richmond wakafanya madudu, Dowans wakasema sisi tutafanya, wakafanya kweli, sasa hata ukiwa na mkataba ambao si mbovu, utakataa kuwalipa gharama zao? mitambo wameleta, wameijaribu, tena wameileta kwa haraka sana kuliko ilivyokuwa Richmond, halafu umeshapata mvuwa, huna tatizo la umeme, ukurupuke tu, useme sasa hatuihitaji hii mitambo! khaa, hiyo mahakama ipi itakayo kwambia haya umeshinda usilipe ondoka. Haiiingiiii akilini. Tuwe wa kweli.
Nadhani umekosa kuona nilichokuwa nakisemea:Nilichangia HOJA ya Ruta kuhusu ukinzani wa arbitration na Katiba. Maana yangu ni kuwa kilichopitishwa kwenye arbitration kitabakia final.
Kuhusu hii hoja yako kwenye bold ambayo ni nje ya kile nilichokuwa nakisemea, nasikitika kuona msimamo kama huu kwa mzalendo unless uwe siyo mzalendo.
Ina maana desperation itakufanya uue mtoto wako kwa vile tu unahitaji kitu fulani? Kwani tusingeweza kupata deal nzuri zaidi ya hii inayotuingiza hasara ya mabilioni? Ni watu wangapi wangeweza kufaidika na pesa hizo tunazolazimika kulipa leo needlessly? Umeshajiuliza kwa mfano ni watu wangapi wanapoteza maisha kwa sababu ya kutokumudu gharama za matibabu ya magonjwa yanayotibika kirahisi tu?
Umeshajiuliza kwanini nchi yetu inaendelea kudidimia kwenye lindi la umasikini ilhali tumejaaliwa rasilimali za kila aina? Moja ya sababu kubwa ni uzembe wa namna hii - uzembe unaotokana na kutokujali kuweka maslahi ya taifa mbele!