"wajinga ndio waliwao" hiyo kujibu swali lako la kwanza.
Picha ipi wewe? watu wanadai haki zao humo, wee unafikiri utavunja tuu mikataba ya watu? Dowans lazima walipwe na wale waliowakopesha Dowans hiyo mitambo lazima walipwe. Usifikiri watu wanafanya biashara za kizamani za kuficha chini ya uvungu!
Si humu JF ndio mlikuwa mnashabikia Dowans wafutiwe mikata na mitambo isinunuliwe, tukasema, na hata mbunge wenu Zitto akasema "inunuliwe"! Great Tinkers waka-kataa! sasa mnalia nini? mlishindwa great thinkers na kujuwa consequences zake?
Ushauri wa bure: Kaeni chini na Dowans, wataelewa tatizo, lakini msijidai ubabe, enzi za ubabe zimekwisha! Hamsomi makosa ya zamani?
Nyerere alijidai ubabe kwa makaburu waliokuwa wanaunganisha materekta akawafungia akasema "sirudi" nyuma ntageuka "jiwe"! alivyoona mambo yamemkalia vibaya, kwani wale jamaa walikuwepo kihalali kabisa, akaona bora ageuke jiwe, akawawacha waendelee na shughuli zao.
Na haya ya Dowans tungejifunza kwa Nyerere! mbona hajageuka jiwe?