Umesoma vizuri hiyo kesi ya dowans na rdevco inahusu nini lakini? Yaani ulitaka Serikali inunue mitambo ambayo ipo kwenye kesi!! Halafu unajua PPA ya TZ inasemaje kuhusu manunuzi?
Sikiliza, sasa hakuna cha kununuwa hiyo mitambo, hilo ni suala lilikuwa kabla hukumu haijatolewa. Ni mapendekezo ya walioona kuwa hili la kulipa gharama kibao litakuwepo ikiwa kesi itaendelezwa. Yalitukuta kwa kuvunja mkataba na IPTL hatujasoma.
Watu wanashindwa kuelewa kuwa hakuna mfanya biashara asiye taka faida, na katika hili la Dowans, mitambo ilishafikishwa pale Ubungo na ikawa-commissioned na miwili kati ya hiyo ni brand new. Leo uwaambie wafanya biashara hatuitaki, halafu wao wakae kimya, wanakutizama wanangoja wafilisike? Hakuna mahakama duniani itayoipa ushindi Tanesco kwenye kesi hii, iende itavyokwenda. Ingekuwa mitambo haijaletwa, au imletwa chini ya kiwango, au mibovu, au mitambo hewa, hapo ndio tungeweza kushinda.
Hawa mahakimu wanaotizama hizi kesi ni watu makini na wanapitia mikataba na wana-tazama real situation na wanajuwa biashara za kima-Taifa zinaendeshwaje.
Hata ukiwalaumu wana-sheria wa Tanesco, bure tu. Walijkuwa hawana cha kufanya kwa hili, na walijuwa kuwa hii kesi hatushindi, lakini na wao wamepelekewa kazi waikatae? Wangeikataa ndio hayo hayo malipo lazima, sasa wafanye nini, wajaribu bahati yao, na ndicho walichofanya. Sasa sisi tubaki na porojo tuu humu.
Mimi nasema, fungilia mbali Tanesco na waache wafanya biashara waendeshe, tena si kwa kuingia ubia au kuwapa waendeshe lakini mali yetu, hapana. Ya ama wainunuwe iwe mali yao 100% au hisa zingine wauziwe wa Tanzania, kama yalivyofanywa mashirika mengine yaliyokuwa yanatia hasara kila siku, mbona leo yanaingiza faida? simply ni kuwa, hata umuweke nani kuendesha haya mashirika ya uma hataweza! wacha wenye vipaji vyao wafunguwe mashirika. Serikali ibaki kuweka kanuni tu, kama tunavyoona kwenye mambo ya mawasiliano, lilipokuwa shirika la uma moja tu, bei za mawasiliano zilikuwa juuu sana, hamna ufanisi, una book simu leo ya kwenda nje unaweza uipate baada ya wiki. Baada ya kuruhusu mashirika binafsi ya mawasiliano si tunaona matokeo,leo mawasiliano ni rahisi kuliko miaka 30 nyuma, huoni ajabu hapo, halafu hilo shirika moja tu, likawa halina faida.
Leo hii ikiamuliwa yaje mashirika mengine ya kugawa na kufuwa umeme, utaona bei za hii nishati zitavyo poromoka na hautosikia sijui nani kaiba mitambo sijui nani kaiba transformer, sijui nani kaiba mafuta ya transformer.
Leo nilikuwa na msikiliza Mhando wa Tanesco, nikamshangaa sana, anasema wanaweka Tranformer mara tano sehemu moja na kila wakiweka inaibiwa mafuta. Yaani huu kama si upumbavu ni nini, umeshaweka mara ya kwanza, umeibiwa, ya pili umeibiwa, hujatafuta solution tu? wewe unaendelea kuweka Transformer nyingine mpaka mara tano. Halafu unakuja kujisifu kwenye TV? what a shame. Halafu ndio kampuni itaendelea kwa kuendeshwa na watu kama huyu?