Tanzania ni nchi yenye umakini sana katika suala la kuwa na mipango ya muda mrefu. Matatizo yapo katika maeneo kadhaa kama yafuatayo:
- Ukosefu wa ushirikishaji wa wananchi katika kufikia mipango hiyo na hivyo mipango hiyo kukosa uhalali na uchangiaji chanya wa wananchi katika utekelezaji wake.
- Kutumika kwa wataalamu walio na mahusiano maalumu na wanasiasa zaidi ya kigezo cha utaalamu uliokubuhu.
- Utegemezi wa mataifa na asasi za nje katika kugharamia utekelezaji wa mipango hiyo.
- Uingiliaji wa maslahi binafsi na ya kisiasa ya muda mfupi katika utekelezaji wa mipango hiyo ya muda mrefu.
Pia ni utamaduni wa watanzania kuacha kujishughulisha kutafuta na kufuatilia taarifa za mipango hiyo kutoka serikalini. Tuna tatizo kubwa la upashanaji habari lakini pia hatuna utamaduni wa kujisumbua kutafuta habari hizo.
Haya ni matatizo ya kimfumo ambayo ni uthubutu wa kubadili mfumo wetu wa kisiasa, kijamii na kiuchumi tu ndio utakaotutoa hapa tulipo lakini sio vinginevyo.
Tuthubutu kuwa sehemu ya mabadiliko na sio kuendelea kusubiri MASIHA FEKI ndio watuletee mabadiliko tunayoyataka. Kupiga kelele tu haitoshi. Watanzania tulipiga na tunaendelea kupiga kelele dunia nzima ikatusikia lakini bado tupo katika lindi la matatizo ambayo yanazidi kuongezeka badala ya kupungua.
omarilyas
Hakuna
Mtu kakosea anaambiwa kakosea kuomba radhi ni yeye na utashi wake utakavyomtuma.
mimi nafikiri huu mtindo wakusema eti kusimamia unachoamini hapa hatupo ktk dini hiki ni chanzo cha udikiteta.
Dikteta kwa kuamini mawazo yake zaidi kuliko yaliyo ya wengi ndicho humponza dikteta,Mimi nafikiri kiongozi umetumwa umepewa dhamana ya kuwakilisha kusimamia mawazo ya walio wengi yani wananchi na sio mawazo yako.
Mara nyingi japo si mara zote kiongozi yoyote anayesimamia mawazo yake badala ya wananchi hata kama mawazo yake yapo sahihi mwisho wa mwisho huishia kuwa dikteta na kutoa vitosho anavyoviona yeye vinamfaa maana anaamini mawazo yake siku zote yapo sahihi.
Kaka hiyo haina maana kuwa hatuna mipango ya muda mrefu. Ipo tena mingi tu. Hata katika sekta ya KILIMO kaka. Ukitoa mipango mingi ya miaka ya nyuma hivi sasa kuna Mpango wa ASDP (Agriculture Sector Development Programe) ambao ulipaswa kupatiwa shilingi trilioni moja kila mwaka kwa miaka saba. Kaka ukipitia kwa umakini mpango huu wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo huo utashangaa sana inakuwaje tunaanza kuja na mipango ya bandikabandua kama ule wa mbolea na fedha za EPA na kuacha kuuwezesha mpango huu ili ufanikiwe.
Tatizo kubwa katika mpango huu ni kuwa haukushirikisha wadau wengi katika kuuandaa, umekosa uhalali kwa upande wa walengwa halisi, unategemea msaada wa nje kuweza kuugharamia na zaidi wanasiasa wengi hawaujui kwa undani na hivyo kuuona hauna maslahi yao kisiasa haswa katika kutimiza malengo yao ya muda mfupi.
Fuatailia mpango huo pamoja na mabadiliko ya kisera yanayoendelea uone ni jinsi gani watanzania tunavyopenda kuja na mipango ya muda mrefu lakini hatuko tayari kukomaa nayo kutokana na mapungufu yetu kimfumo na kibinfsi.
omarilyas
Nakushauri usome insha moja inasema "the tyranny of the majority".. utaelewa kuwa mawazo ya wengi siyo lazima yote yawe sahihi! Na kuhusu dhamira mawazo ya majority hayalazimishi mtu ukane dhamira yako ndiyo maana kuna watu wameenda na kuwa mashahidi kuliko kukana kile walichokiamini katika dhamira zao.
Sasa kama wewe unapenda kufuata mawazo ya wengi kwa vile yana mvuto zaidi hilo jingine lakini mtu anayefuata mawazo yake kwa vile dhamira yake inamtua kuwa ni sahihi huyo ni mtu huru.
Kifupi kama mimi ndiye Kikwete basi huyu Idrissa anatakiwa kuwakilisha barua yake ya kujiuzuru mara moja.. maneno yake tu yanatosha kuonyesha hawezi kazi alokabidhiwa..
Hata hivyo labda kwa wale wasiomjua, huyu mkuu tunampa heshima yake lakini... Lol! salaaleh! hafai hata kwa kulumangia..
Nakushauri usome insha moja inasema "the tyranny of the majority".. utaelewa kuwa mawazo ya wengi siyo lazima yote yawe sahihi! Na kuhusu dhamira mawazo ya majority hayalazimishi mtu ukane dhamira yako ndiyo maana kuna watu wameenda na kuwa mashahidi kuliko kukana kile walichokiamini katika dhamira zao.
Sasa kama wewe unapenda kufuata mawazo ya wengi kwa vile yana mvuto zaidi hilo jingine lakini mtu anayefuata mawazo yake kwa vile dhamira yake inamtua kuwa ni sahihi huyo ni mtu huru.
Mkandara, Zitto akitambua ni wapi alipotoka na akaja kuomba radhi mimi sina tatizo; siyo hapa tu bali hata kwa hadhara ya Watanzania. Ni sehemu ya uungwana na ukomavu. Tatizo langu ni kuwa baadhi ya watu wanaonekana kukwazwa kupita kiasi kana kwamba Zitto hatakiwi kufanya makosa, kupotoka au kwenda nje ya mstari fulani. Kwamba, akichukua msimamo basi ni lazima uwe sahihi wakati wote. Hilo haliwezekani. Hakuna mwanadamu anayeweza hivyo.
Ndiyo maana kwa maoni yangu, nashangazwa na ukali wa maneno ya watu kwani naelewa kuna wale ambao wanatambua kuwa kijana amekosea na wamejaribu kumshawishi aone makosa hayo; bado hilo hatujui kama ameona makosa hayo.
Tatizo ni kuwa watu wanataka Zitto akubali tu kuwa amekosea hata pale ambapo dhamira yake na akili yake haimshawishi kuona makosa hayo. Dhamira ya mwanadamu iko juu ya sheria n.k NI lazima afanye kile ambacho dhamira yake ambayo imejengwa vizuri (well formed conscience) inamuambia kuwa ni kitu sahihi.
Nadhani tukimpa muda wa kutafakari na kupitia taratibu hoja hizi zote na ushahidi ambao utazidi kutokea huko mbeleni ataweza kuona ni wapi alipoenda pembeni na kwa kiasi gani. Kwa sababu naamini kama alivyosema Halisi yawezekana kabisa kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo hayakuripotiwa sahihi. Uzuri ni kuwa wengi wetu waliouelewa msimamo wa Zitto siyo kutokana na magazeti bali tumesoma aliyoyaandika yeye mwenyewe.
Ombi langu ni kuwa watu wasiwe wakali sana kulazimisha mtu achukue msimamo wao kama mtu huyo hajashawishika kufanya hivyo. Vinginevyo tutamfanya achukue uamuzi wa kinafiki. Tumpe nafasi apime na kuona uzito wa ushahidi uliopo kwanini hatulazimiki na hatuna sababu ya kununua majenereta yaliyoletwa na Dowans, na akishashawishika hivyo basi yeye mwenyewe atajua achukue hatua gani. Vinginevyo, atakuja hapa na kuomba radhi na watu watasema "haitoshi, inabidi ujiuzulu"; na wengine watasema "haitoshi kujiuzulu, itabidi ujivue uanachama" (tayari kuna watu wameshatoa mapendekezo hayo humu humu).
Ninachoelewa ni kwamba kuna wale ambao wanamkosoa Zitto kwa ni nzuri lakini siwezi kushangaa kuna wale ambao wanamkosoa ili kumfanya duni na kumharibu kuliko ukweli wa hali halisi.
..tungeitumia vema tusingenunua madege mabovu,mapantoni na mitambo mingine.....!!!!
Bubu
.......naomba umsome vema Mkuu Omarilyas, anachoongelea hapo juu ni sahihi kabisa...........
Halisi,
Zitto nimemsoma kw amakini sana kauli zake hapa JF
1. Zitto alizungumza kwa niaba ya Kamati
3.Kosa lake kisiasa ni kukubali kuburuzwa na msimamo wa kamati yake.......kama alivyotuonyesha awali kuwa anasimama na kamati yake
4.Nia yake ya kukutana na Kamati ya Shelukindo...naweza kuelewa ilikuwa ni opportunity nzuri kwake...
IPP MEDIA
09 Mar 2009
By Simon Mhina
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Estherina Kilasi ambaye pia ni Mbunge wa Mbarali (CCM)...alisema maneno ambayo yamemkariri Mwenyekiti wao (Zitto Kabwe) yalikuwa maoni yake binafsi na wala sio ya kamati kwa vile hakuna hata kikao kimoja ambako walikubaliana na ombi la kununua mitambo hiyo.
``Wala hatujawahi kutoa ushauri wowote juu ya suala hilo, zaidi ya kuwaelekeza Tanesco walifikishe kwa kamati husika ya Nishati na Madini,``alisema
Akifafanua, alisema kilichotokea siku hiyo ni semina ambayo Tanesco waliiandaa na kuwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo kwa lengo la kuwaelezea mipango ya kununua mitambo ya Dowans kwa kuwa wana kiasi cha Sh. bilioni 60 kwa ajili hiyo.
``Sisi tuliwahoji kama mnazo Sh Bilioni 60 mnashindwajwe kuongezea kidogo ili mnunue mitambo mipya? Vilevile tukawahoji hivi mambo haya mnayotuambia kwenye semina wameyapeleka kwa wahusika ambao ni Kamati ya Niashati inayoongozwa na William Shelukindo?,`` alisema Kilasi na kuongeza:
``Baada ya hapo tuliwashauri suala hilo walifikishe kwa wahusika (Kamati ya Madini) na hakuna hata mahali pamoja tulipolitolea uamuzi suala hilo kwa vile halituhusu.``
Mbunge huyo alisema kufuatia kauli za Zitto ambazo zimezua malumbano, na kuifanya Kamati yao ionekane ina `walakini` wanamsubiri kwa hamu arejee ili wamuweka kiti moto.
``Unajua baada ya semina ile mimi nilienda Zambia, huku nyuma ndo nikasikia malumbano, lakini baada ya kurejea nimewauliza wenzangu na hasa makatibu wanaoandika muhtasari, kama kuna kikao kingine kimeketi na kutoa uamuzi, lakini wakasema hapana. Sasa tunamsubiri Zito arejee safarini ili tumuulize kulikoni? ``Alisema.
Aliyosema Zitto Kabwe kwamba yametokea kwenye kamati yake wenzake wamemruka! Makamu Mwenyekiti amesema Kamati ya Hesabu haikuwa na mpango wa kukutana na Kamati ya Madini kwa sababu "halituhusu."
Sasa najiuliza, ni kwa nini Dr. Slaa alisema kwamba hatujui yaliyotokea kwenye kamati ya Zitto? Hata Dr. Slaa hakumwamini Zitto? Duuuh, hii inatisha mbona!
Makamu Mwenyekiti wa Zitto kasema hivi:
Omarilyas, ndiyo hapo nasema huwezi kuwa na mpango nzuri kwenye makabrasha tu halafu ukija katika utekelezaji ni sifuri. Kwa maoni yangu mipango ya muda mrefu ambayo unaiweza kuiita mizuri ni ile ambayo utekezaji wake pia unakamilika 100%, vinginevyo hiyo mipango ni mizuri tu ikiwa kwenye makabrasha lakini mafanikio yake Watanzania hatuyaoni kwa sababu utekelezaji wa mipango hiyo hakuna.
Topic ni Zitto au Dowans?
Kama Mtanzania Zitto is entitled to whatever he said. Sielewi kelele zinatoka wapi!
Mkandara,Kipa,
Kikwete ana makosa na mapungufu yake lakini sio ktk hili..Ikiwa sisi tumeshindwa hata kutumia vizuri fedha zilizotolewa kwa dharura kweli tunaweza jenga nchi ktk miradi ya muda mrefu..Trust me, matukio yote haya nadhani ni bora ungewatazama viongozi wetu wanaoendesha shughuli hizo kabla ya rais..Kikwete atafukuza wangapi..
Huko CCM karibu asilimia 80 wameoza sasa Kikwete ni ktk fungu la kaa walioko ktk kapu wanasubiri kuchomwa..Binafsi naanza kuamini kabisa kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kuibadilisha CCM na Ufisadi ni ukweli ambao hatutaki kuukubali..
The only way out ni kutochagua CCM wameshindwa kama KANU, ZAPU, UPC na vyama vinginevyo vilivyoletea Uhuru barani..waliobakia wote ni madikteta tu!