Mbona katika kukiuka taratibu mmeshikila tu suala la mitambo ya Dowans? Vipi mazungumzo yanayoendelea na IPTL na Artimus? Vipi ununuzi wa ndege za ATC? Vipi ununuzi wa Panton la Ferry? Haya mambo yalivyofanyika hiyo sheria ya manunuzi ilikuwa bado au vipi?
Hebu tusahau kama fedha hizo zinaingia mfukoni mwa Rostam na tuelekeze akili zetu kwenye mambo yafuatyo:-
1. Mgao utafanya viwanda vipunguze uzalishaji na hivyo kuikosesha serikali mapato.
2. Wafanyakazi wa viwandani watapunguzwa kazi kutokana na kupungua kwa uzalishaji. Hivi ni familia ngapi zitaathirika?
3. Viwanda vitaendeshwa kwa hasara kwa matumizi duni ya rasilimali zake.
4. Kuathirika kwa sekta zingine kama kilimo, utalii etc. kutasababisha kushuka kwa uchumi kwa ujumla.
Hivi haya yote hamyaoni jamani. Mmeshikilia tu eti afadhali nchi iingie gizani kuliko kununua mitambo ya Dowans. Are we really thinking staright au tumeingiwa na kawazimu fulani?
Ninyi subirini tu mgao ndio mtaona raha ya huu upuuzi wenu mnao usimamia kwa nguvu zenu zote.. Tena si mbali Aug/Sept 09.
Niko upande wako kaka!!! siku hizi kila jambo limekuwa siasa!!! 90% ya wachangiaji hata hawakusoma press release ya TANESCO lakini wanavyochangia wao wanafahamu kuliko TANESCO...
Bongoland bwana!!!
Richmond ndio isiyofahamika. Dowans inafahamika acha uongo!!!Zamani nilikuwa nikijiuliza shetani anawezaje kuja na kuishi miongoni mwetu wanadamu bila sisi kujua??
Nizidivyo kuishi nakupata umri nagundua kwamba ni rahisi kuliko nilivyodhani kwa ibilisi kujitoma miongoni mwa bin adamu na kujichnganya kiulaini.
Ni vipi mitambo mikubwa iliyojaa karibu eka 4 pale Ubungo iwekwe katika ardhi ya Tanzania na mtu asiye fahamika?
Ni vipi waziri apite kila kona kutaka kununua mitambo ya umeme kutoka kwa mmiriki asiyefahamika?
Ni Vipi Rostamu Azizi atoe Ofisi yake kumpa mmiliki wa kampuni ya Dowans asiye julikana?
Hivi ni kweli tulidai Uhuru ili kuwa huru? Au tulidai Uhuru kutoka kwa Waingereza ili tuwe koloni la wahuni kadhaa ndani ya nchi?
Ni vema tukae katika Giza kuliko kununua mitambo ya umeme kutoka kampuni yenye utata wa mmiliki na iliyogubikwa na kila aina ya ushetani.
Kwa sababu MH Zitto ni mmoja wa watu wanao tetea Tanesco kununua mitambo hii.
Nakuomba MH Zitto unipe jibu la swali hili.
Nani ni mmliki wa Kampuni ya Dowan.
TANESCO walikuwa na miaka karibia 50 ya kutuonyesha ya kuwa they know what they are doing and they have failed miserably, in my eyes, hawana credibility! Wakati rushwa imekithiri mpaka kwa fundi umeme wa mwisho ambaye anataka hongo katika mtaa wenu wakati wa harusi ili wasiwazimie umeme, mi sina heshima kwao! They may be good professionals (engineers etc - which I have reservations about) lakini hawana ability to think, analyze, synthesize and top of all it, hawana utu wanapoamua kutumia nafasi zao kuzimazima hovyo umeme.
TANESCO imejaa incompetent, greedy people. Wacha wabinafsishwe tu! Wote wapewe barua zao, watimuliwe kazi tuanze moja! Tuna ma-engineer huko nje ya nchi ambao with the right incentives and circumstances watakuwa tayari kurudi na kujenga nchi yao, si hawa ambao wanaangalia maslahi yao binafsi.
So Kasheshe mkuu, I am not impressed by TANESCO and in my eyes they have ZEROOOO credibility! Na bosi wao ndo kabisaaaaa! Sorry kama we ni mdau! Just me expressing myself!
Richmond ndio isiyofahamika. Dowans inafahamika acha uongo!!!
DOWANS hawana issue yoyote na identity!!!
Msikieni tena mbunge kijana alivyobwabwaja......msikilize kwa umakini Dr Mwakyembe.....
Bubu Ataka Kusema,
Mkuu hizi zabuni za nini ikiwa wenye shida ni sisi.. kwa nini tanesco wasiende shopping wenyewe kununua mitambo wanayoitaka.. why middlemen kwa kila tunachokihitaji wakati njia za kupata mtambo unaotaka zipo..
Toka Rada, ndege ya rais tumeweka middlemen, ndege za ATCL, nasikia hata mabus ya kufufua UDA kila siku kuna mtu wa kati na kadhalika why tusiagize na kununua sisi wenyewe..
Tender hutolewa kwa kazi za contracting sio manunuzi jamani tutajifunza lini sisi wenyewe kuendesha vitu vyetu!..
Naipongeza sana IPP media, kwani waandishi wake wamefanya azi inayotakiwa kufanywa na mwandishi wa habari, get out there and findout the facts! Same kudos to Mwanahalisi!
Kwa hiyo kama tunavyoweza kuona there is no emergency, naomba pia watuhabarishe kuhusu hii ishu ya LUKU because it is another usanii!
Dr Idris ni mtu hatari sana, si tuafukuzwe kazi bali akamatwe mara moja na atueleze alikuwa ana njama gani ya kuhujumu nchi!
....kaka kikwete ana lawama zake kwa kuwa makaburasha ya mahitaji ya tanesco alipewa tangu mwaka 2006 ....hajatekeleza hata moja ........so tumuiteje???
hali ya tanesco kifedha ni hohehahe wanategemea kutukamua sisi wanachi...
for that i have a reason kuendelea kumpenda mwalimu nyerere...kwani hadi sasa uwanja wa ndege tunaotumia arusha,kilimanjaro,dar,mtwara everywhere alijenga yeye....
umeme wa bei nafuu tunaotumia leo wa mabwawa ya maji alijenga yeye...na mengine mengi..baada ya hapo ni sarakasi tu..!!
Hayo matatizo ya Tanesco yalianza 2006?, Kikwete ndie aliyepiga kifuwa kuyatatuwa, au umesahau? Na alipobaini kuwa watu aliowaachia majukumu ya kutatuwa matatizo ya umeme wamefanya madudu (Lowassa, Karamagi, Msabaha), hakuwasamehe wala kumtetea hata mmoja, akawacha sheria ichukuwe mkondo. Au yote hayo huyajui. Besides, akatimuwa uongozi wa juu karibu wote wa Tanesco, akmuweka trouble shooter (Dr. Rashid), ambae ana track record nzuri, katika taasisi zote alizoongoza kwa wakati wake, hakuna scandals na madudu anayo yakuta anayanyoosha. Kaanza kuiweka sawa Tanesco, watui wanalalamika, Jee hamuujuwi uozo uliokuwa Tanesco kwa miaka ne miaka rudi? mnafikiri JK au trouble shooter wake wanaweza kuya tatuwa matizo hayo kwa mwaka mmoja? No way, Tanesco ni shirika kubwa lililooza kila sehemu, lina hitaji total overhaul, na ndio Dr, Rashid yupo mbioni kuliweka sawa na at the same time anataka watu wasitaabike kwa umeme, simple solution: Mitambo tayari ipo Ubungo, madudu yamefanyika, yanashughulikiwa. Kesi ipo Paris, Jee hamkumbuki ya IPTL, kwa kujidai kuvunja nao mkataba sasa tunalipa kutoke puani na vinywani mwetu, IPTL kesi wameshinda, ikabidi tulipe gharama za kesi zao na zetu, fidia, na faida na pia kulipa muda wote ambao wallikuwa idle na mkataba bado uendelee.
Ukifikiria hayo machache tuu, Dowans hali kadhalika, kesi watashinda, kwani ipo Paris, hakuna longo longo huko. Mkataba ni wa kimataifa, mitambo itumike isitumike tutailipia, gharama za kesi, zao na zetu tutazilipia. Na ikiwa IPTL imetutokea puwani basi hii itatutokea (sijui wapi?).
Simpo solushen, negotiate na hawa jamaa, nunua mitambo ya mambo yao kwa bei nafuu, kila mtu alipe gharama zake za kesi (ambayo hatushindi kabisa), watu wapate umeme. Other than that ni kuwatesa wa Tanzania.
Tatizo hili ni pure commercial na watu walichukulie hivyo, mambo ya kuchanganya politics na commerce ndio yanatuweka pabaya. Jee hatuoni yaliyokwisha tukuta tukajifunza?
Miezi 6 inatosha kabisa kutengeneza turbine ya hata 200MW hivyo bado wanamuda mzuri tu wa kuweza kununua mpya wa 100MW kwa $30-40million.
Mkuu,
Kununua mitambo chakavu ya Dowans (wezi) ni sifa ya troubleshooter au trouble maker?
Mkuu,
Kununua mitambo chakavu ya Dowans (wezi) ni sifa ya troubleshooter au trouble maker?
Mkuu,
Kununua mitambo chakavu ya Dowans (wezi) ni sifa ya troubleshooter au trouble maker?
Napenda uelewe kuwa, mitambo yote mikubwa ni bora zaidi iliyokwisha tumika kwa muda mfupi na kurekebishwa faults zote zilizojitokeza kuliko kuinunuwa brand new, ambayo hakuna company yoyote duniani itayoweza kukupa guarantee kuwa ni ''plug and play''. commissioning tu ya mitambo mipya kama hii inayoongelewa, inachukuwa at least mwaka mmoja. Jee unafahamu hilo?
Besides, Dr. Rashid lazima anafata ushauri wa ma engineer wake kuhusu hii mitambo, Jee, unajuwa ameshauriwa nini na ma-engineer wake? I'll best my last penny, a good engineer, taking into consideration ya mgao wa umeme na hasara zake, taking into consideration ya purchasing process ya kwetu na bureaucracy zake, taking into consideration, manufacturing, supply, testing, commissioning, handover,...atashauri bora hii iliyotumika 400 hours.
Hakuna ubishi katika hili.
Unajua Dr Idris Rashid amebadilisha uwamuzi wa kununua mitambo hiyo kwa sababu za kisiasa tu, na sio kwa technical reasons!