The only way out ni kutochagua CCM
Mtaambiwa kutoa order mpaka mitambo itengenezwe ni miaka 2 kisha kuship hiyo mitambo TZ itatumia zaidi ya mwaka 1 kutokana na ships zipo busy sana.Mtaambiwa kuja mafundi kuifunga kwenye grid ya taifa watachukua mwaka kutokana na economic crisis.Watakwambia ndo maana tunataka mitambo ya DOWANS kwa vile ipo hapa hapa TZ.Ukipiga hesabu hapo tayari uchaguzi mwingine
Kipa,
Kikwete ana makosa na mapungufu yake lakini sio ktk hili..Ikiwa sisi tumeshindwa hata kutumia vizuri fedha zilizotolewa kwa dharura kweli tunaweza jenga nchi ktk miradi ya muda mrefu..Trust me vyama vinginevyo vilivyoletea Uhuru barani..waliobakia wote ni madikteta tu!
"Wale ambao zamu yao ya kula hii nchi....imepita"-Dr Mwakyembe...
Dr Mwakyembe-"nusu anayotamka Zitto sio maamuzi ya kamati yake......."
Kwanza msikieni Dr Slaa......Dr Slaa na mpito wa Dowans
Kisha wasikie Zitto na Dr Mwakyembe link below
Dowans na malumbano ya kamati za bunge
Credit:kennedyblog
Phillemon Mikael,
Mkuu walioingia mkataba na IPTL, Songas, Richmond/Dowans ni TANESCO..hivyo huwezi kutenganisha serikali na Tanesco ikiwa nchi yetu bado inaendeshwa Kikomunist.. nachokataa mimi ni pale unapotenganisha Tanesco na serikali wakati Idrissa amechaguliwa na rais kushika wadhifa huo. Hili sio shirika huru mkuu wangu, tunadanganyana tu kwani ni watu wale wale wangekuwa madarakani kama lingekuwa shirika la Umma chini ya Ujamaa.. Hawa wote wanatakiwa kulaumiwa, Toka Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete ahadi hizi zilikuwepo hazikuanza jana, hawa wote wanakula sahani moja isipokuwa wanalala vitanda tofauti..Mwenye donge mkononi sasa hivi ni Idrissa na lazima alaumiwe yeye kwani maamuzi yake ndio yatakayo tuweka kizani - hadi lini Mungu ndiye anajua...
No. Hakuboronga huko kote na ndio maana kapewa Tanesco aiweke sawa, ilikuwa hoi bin taabani, Dr. Rashid ndio aliyoi-save, na madudu yote ya Tanesco kayakuta na ndio anajaribu kuiweka sawa.
BOT hali kadhalika, aliyakuta madudu akaweka sawa na alipoondoka tu, madudu yakaanza upya, matokeo yake nadhani mnayafahamu.
Voda, kaifanyia kuwa kampuni ya mawasiliano yenye nguvu (kwa idadi ya wateja na mapato) kuliko kampuni nyingine yeyote ya simu Tanzania.
Hilo sina taabu nalo kwa sababu sina chuki na mtu binafsi, bali kiongozi anayefanya fyongo kwenye mambo ya muhimu kwa nchi yetu. Nikiridhishwa bila shaka yoyote kuwa hana maslahi binafsi kwenye yale anayoyafanya nitampigia hata saluti!!🙂Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni!
Rev. Kishoka,
Mbona kama TANESCO wamejibu mengi ya maswali yako? Soma tena statement ya TANESCO.
Muhimu sasa ni wapi kwa kupata mtambo mpya kwa bei poa ambao utaokoa taifa kutoka kwenye hasara ambayo tunaingia sasa.
Wakati tunaendelea kulumbana kuna watu wengi tunaendelea kuathirika na ukosefu wa umeme kwenye shughuli tunazofanya. Matokeo yake serikali inakosa pesa kupitia kodi na pia mnunuzi anaishia kulipa pesa zaidi kufidia gharama za generators na mafuta pamoja na kupungua kwa uzalishaji.
Inabidi serikali ije na jibu la haraka vinginevyo tishio la TANESCO huenda kweli likatokea. Kuna sehemu ambazo nazijua mimi tayari zinapata umeme 20% ya muda na hiyo ni March, sijui ikifika September itakuwaje?
Nafikiri njia nzuri kwa sasa ni kuikabidhi hii tender kwa bunge ili watatua matatizo ya umeme Tanzania. They have talked the talk, may be it is a right time to let them walk the walk. Sisi tunachotaka ni umeme, longo longo zingine hazitusaidii kitu.
Kasheshe,
Mkuu unakosea hapa unaposema wa kulaumu ni serikali wakati aliyetaka kununua mitambo hii ni TANESCO hali fedha zinatoka serikalini ambako wewe unasema huchukua forever..
Nasikitika kusema kuwa uwezo wa Dr Rashid kuendesha TANESCO umefikia mwisho, kwa kuwa TANESCO haina Strategic Plan yake ya miaka walau 5 tu? Ni aibu kwanini kila siku wanakimbilia zima moto, hawakuwa na fall back position baada ya mafisadi kuvunjiwa mikatana yao? hapa ndipo nashindwa kuwaelewa WaTZ. Jamaa amedeclare kuwa ameshindwa pia na TANESCO kwa kushindwa kuweka malengo ya muda mrefu na ndio maana anatutishia. WaTZ tuamke, MJOMBA mtimue kazi Dr Rashid (yawezekana PhD yake pia ni kama za wale wa CCM wanaojaribu kuzihalalisha)
Rev. Kishoka,
Mbona kama TANESCO wamejibu mengi ya maswali yako? Soma tena statement ya TANESCO.
Muhimu sasa ni wapi kwa kupata mtambo mpya kwa bei poa ambao utaokoa taifa kutoka kwenye hasara ambayo tunaingia sasa.
Wakati tunaendelea kulumbana kuna watu wengi tunaendelea kuathirika na ukosefu wa umeme kwenye shughuli tunazofanya. Matokeo yake serikali inakosa pesa kupitia kodi na pia mnunuzi anaishia kulipa pesa zaidi kufidia gharama za generators na mafuta pamoja na kupungua kwa uzalishaji.
Inabidi serikali ije na jibu la haraka vinginevyo tishio la TANESCO huenda kweli likatokea. Kuna sehemu ambazo nazijua mimi tayari zinapata umeme 20% ya muda na hiyo ni March, sijui ikifika September itakuwaje?
Nafikiri njia nzuri kwa sasa ni kuikabidhi hii tender kwa bunge ili watatua matatizo ya umeme Tanzania. They have talked the talk, may be it is a right time to let them walk the walk. Sisi tunachotaka ni umeme, longo longo zingine hazitusaidii kitu.
Mkandara,
TANESCO hawakusema wanataka kununua mtambo wa DOWANS walisema wanaomba serikali inunue mtambo wa DOWANS.
Tuwe makini TANESCO hawana fedha za uwekezaji fedha walizonazo ni za operations and maintenance.
Bado sijaona kwa nini lawama zinapelekwa TANESCO yet serikali ndio haikuwekeza kwenye sekta ya UMEME kwa muda mrefu,.