Wadau, kuna taarifa zimenifikia kuwa Tanesco imesema sasa mitambo ya Dowans basi, je kuna mwenye uwezo wa kutafuta taarifa zaidi afanye hivyo?
Kama ni kweli, kulikuwa na sababu gani za kufanya jaribio hilo? nani alitoa hoja hiyo kwa shirika ambalo, mwezi October tu mwaka jana lilikanusha tetesi kuwa lilikuwa mbioni kununua mitambo hiyo?
Je nini sababu za kubatilisha uamuzi wake wa sasa, hasa baada ya kututisha kuwa nchi itaenda gizani, kama vile hatujawahi kuliona giza, na kwamba Dowans ilikuwa ni suluhisho pekee?
Wakati Dr Rashid anachukua shirika, alielezwa kuwa ni mtu mwenye hekima na uwezo wa juu. Muda mfupi baadaye, alijaribu kujiuzuru kwa madai ya kuingiliwa kiutendaji, na sasa katika zogo la Dowans, ana nafasi gani ya kuaminika?
Watu wanasiasa kama Zitto, wana nafasi gani sasa katika kutetea utawala bora unaofuata sheria? Zitto alikuwa mkweli alipokuwa akitetea uwezekano wa kununua mitambo ile au alikuwa anataka kuiingiza serikali "king?"
Je, nani hasa alikuwa nyuma ya plani za kuhakikisha mitambo inanunuliwa, na mwekezaji hapati hasara, ni mmiliki wa awali wa Richmond, binamu yake Dowans, au maswahiba wake waliomsaidia kupata tenda iliyosababisha wanene wajiuzulu mwaka jana?
mambo yote haya yana kishindo gani uchaguzi ujao, 2010?
Tujadili tafadhali.