Mwakyembe kachemsha sana....na hasa pale anapozungumzia "operation Snagara" na pia kuhusu "Posho"........sikutegemea hii toka kwake.......nilitgemea angetuchambulia vipengele vya sheria za manunuzi (yeye akiwa mwanasheria) pamoja na kutupa facts zengine ambazo wananchi hatuzijui kuhusiana hii saga........leo hii katufanya MABWEGE.......damn!
zitto bado yuko sahihi kwani ushauri wake hauna hisia kama wafanyavyo sitta, mwakyembe na wenzao.
ccm wana mambo yao na zitto amewashika patamu kwani tabia yao mbaya ya kuendekeza ushabiki kwenye masilahi ya nchi imepitwa na wakati.
zitto asonge mbele na maoni yake kwani hata ile ya buzwagi sitta alimkebehi na kumwadhibu kupitia genge laooooo.
kwa nn akina sitta na wenzao hawakemei mambo chungu mbovu yaliyomo zaidi ya dowans ila kwa kuwa hili wana masilahi bianafsi wanajifanya vinara???
mangapi ushabiki wa ccm unaendelea kukumbatia na sitta kama kada amayanyamaziaaaa...
Zitto waeleimishe kuwa hizo kamati sio siasa ni utendaji na utaalamu tena unaotakiwa kuwa muwazi kila mambo kwa mustakabali wa taifa letuuu..
kwa hili zitto anazidi kuijenga chadema kwa watu MAKINI.....
nyambalaaWakuu suala la mitambo ya Dowans limejadiliwa mna na ktk threads mbali mbali humu jamvini. Personally nimeona ni vema tukawa na thread maalum kama mada isemavyo hapo juu. Hii ni kutokana kwamba Tanesco, Zito na kamat yake, na wale wote wanaotaka kutuaminisha kwamba ununuzi huo ni jambo la busara wanaegemea hapo.
1. Eti kuna mkaguzi kutoka ujerumani amekagua mitambo hiyo na kuiona ni ok na mingine ni mipya ikiwa imetembea for only 400 hrs.
2. Eti mitambo hii itaweza kutembea kwa miaka 13 bila kufanyiwa overhaul.
Ningependa kuanza na huyu the so called mkaguzi:
1. Anatoka kampuni gani?
2. Ana qualifications gani?
3. Ana uzoefu gani na kazi kama hii na amewahi kutumika wapi na kampuni zipi?
4. Ana bima yeyote inayotulinda iwapo ikigundulika alituingiza mkenge?
5. Anatambuliwa na Pratt and Whitney kama mkaguzi wa mitambo yao i.e is he a certified inspector?
6. Mtaalamu huyu aliletwa na Dowans au Tanesco na ni lini alianza kuwa contacted?
7. Kama ni Tanesco nini kilipelekea Tanesco kumuita mtaalamu huyu? Ina maana walikuwa na nia ya kununua mitambo hiyo kabla hata ya kuangalia taratibu zingine?
8. Alifanya kazi hiyo ya ukaguzi kwa muda gani?
9. Alitumia method gani kufanya uhakiki?
10. Tanesco ilimpataje mkaguzi huyu? Wangapi waliapply?
11. Je Tanesco ipo tayari kutoa ripoti ya mkaguzi huo?
12. Wakati wa ukaguzi Tanesco iliwakilishwa na nani? Na Dowans pia na nani?
13. Je mtaalamu huyo amewahi kuifanyia kazi yeyote Tanesco au Dowans before?
Well I know some of you might think we are now going in circles on this SAGA.
Lakini vijiswali hivi ni rahisi na vinaweza kujibiwa na Idris au mtaalam yeyote wa Tanesco aliyehusika na mchakato huu in just 10 mins tena bila hata kusoma mahali for any smart kiongozi. Cha msingi hapa na nia ya maswali haya ni kujiridhisha na kamchakatohaka kanakoonekana kujustfy ununuzi wa mitambo hii.
Pia kuna hili la mitambokuwa mipya na eti mingine imetembea masaa 400 tu. Ikumbukwe kuwa mitambo in this new tecnlogical era hauijaji kwa time based bali condition based. That applies kwenye hili la kwamba mitambo hii haitakuwa overhualed in 13 yrs. Nikiwa kama muhandisi hii sentensi naona imekaa kisiasa zaidi kwani overhauling pia ni condition based and not time based. How do you sell me an equipment and tell me it won't be overhauled in so many yrs? Nchofahamu hapa huyu jamaa atakuwa alikuwa nazungumzia PM (Preventive maintenance) ambayo inaweza kuwa say kuna za daily, monthly, yearly na labda hiyo ya say after every 5 or 10 or even 20 yrs fungua hiki au kile angalia pale na hapa. Hii ni staili ya zamani ya maintenance. You don't have to just overhaul a machine et kwa sababu imetembea masaa 100, 000. (Anyways anayehitaji ziada ya hii I am ready to debate ). Ninachoshangazwa hapa ni how huyu mkaguzi ali come up na hiyo miaka 13 -tena kwa mtambo iliyotumika?
Haya yote yanakuja just because historia ya kampuni hii formely known as Richmond ina utata. Tanesco pia ni watata, serikali ni watata. Hivyo basi kuna kila haja Tanesco itoe press release ya kuelezea mtaalam huyu namaswali hapo juu. Si mnakumbuka hata Richmond waliatuambia wamekubaliana na Pratt and Whitney kushirikiana kuzaisha zile 100 MW? of which they any written doc to support that. Sasa hili la mtaalamu mjerumani tunaaminije kirahisi rahisi? Tunamuaminije kirahisi rahisi Dr. Idris wakati ana questionable credibility? Tunaiaminije Tanesco kirahisi rahisi wakati imekuwa ikitudisapoint thousands of times?
bado naunga mkono hoja ya zitto kushauri tununue mitambo kama tanesco walivyoshaurii.usiku wa jana nilibahatika kuangalia itv channel,sina kawaida ya kusearch tv za bongo mara kwa mara,lakini jana niliipata bila kutarajia.tumeskiliza taarifa ya habari, na kipindi kilichofuatia kikiendeshwa na stephen chuwa ambaye ndiye mwenyewe alikiandaa.hakika nilijawa na hofu jinsi wabunge na spika wao walivyokuwa wanatupiana mpira kuhusu mitambo ya dowans na tanesco.manunuzi , ununuzi,kanuni ,kazi na sheria na kamati za bunge!!!
Tena nikaona pale ikulu bwana s.rweyemamu na ufafanuzi wa alichosema kikwete.jamani kuna ubabaishaji gani wa kiasi hicho?kila mmoja analo jambo la kuongea? Hatuna utaratibu wa kuendesha serikali,mamlaka,na vyombo vyake.wana-jf nisaidieni hapa!!
bado naunga mkono hoja ya zitto kushauri tununue mitambo kama tanesco walivyoshaurii.
Inaumaaa sanaaaaa
MD wa tanesco ni sehemu ya bodi kwa hiyo natumai mapendekezo aliyoyatoa anawakilisha bodi yake pia.Mbona tunaambiwa bodi ya Tanesco imekataa. Hiyo Tanesco ambayo wewe (na Mh. Zitto) mnaitungumzia ni ipi? Au ya Dr Rashid? Bodi ndiyo iko responsible kwa maamuzi ya Tanesco.
MD wa tanesco ni sehemu ya bodi kwa hiyo natumai mapendekezo aliyoyatoa anawakilisha bodi yake pia.
...pia kwa taarifa tuu mtendaji mkuu ndo bottom line mhusika mkuu wa success au failure za organization yake kwani yeye ndo mtaalamu zaidi ya bodi....
hapa jamani kwa sasa SIASA imetawalaaa zaidiiiiii...
pia kwa taarifa tuu mtendaji mkuu ndo bottom line mhusika mkuu wa success au failure za organization yake kwani yeye ndo mtaalamu zaidi ya bodi....
Hii nadhani ni Corporate Governance mpya!
bado naunga mkono hoja ya zitto kushauri tununue mitambo kama tanesco walivyoshaurii.
Hii imetusaidia tena kujua upeo wa viongozi wetu(bunge na serikali) kwa mapana zaidiii.
Kuna upuuzi mkubwa hapa unaendekezwaaaa bila kujali heshima ya wananchi wanaoweka watu madarakani...
Wote sasa wanafanya show down...... Ujinga mtupuuuu
mpaka sasa kamati ya nishati, wizara na ikulu hawajitambuiiiii.....cheap popularity..
Inaumaaa sanaaaaa
Nimekuwa nikosoma na kufuatilia sehemu kubwa ya taarifa kuhusiana na kinachoitwa "kauli ya Zitto" kuhusiana na sakata la mitambo ya Dowans.
Tatizo nililoliona na ambalo wajumbe wengi wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma ambayo Zitto ni Mwenyekiti wake wanaliona. Tatizo lenyewe ni lile la taarifa za kwamba kamati imebariki/inashinikiza/inataka mitambo ya Dowans inunuliwe. Wajumbe wote akiwamo Zitto hawajasema LAZIMA mitambo ya Dowans inunuliwe.
Kabla ya kueleza maelezo ya wajumbe wengi wa kamati niliobahatika kuzungumza nao, niweke wazi kwamba Zitto ni Mwenyekiti (anayeongoza vikao) na kuwa Mwenyekiti (si Mwenyekiti Mtendaji) maana yake ni kufanya kazi kwa vikao na kauli zako zinazingatia vikao. Kama hivyo ndivyo tujadili KAMATI.
KAMATI ya POAC (Kamati ya Zitto) imefanya vikao vyake na katika kikao kimoja wapo walikutana na Tanesco katika kupitia hesabu za shirika hilo na kuangalia matatizo yao ya kifedha. Kama kawaida Tanesco ya Dk Rashid ikapenyeza kwa umakini mkubwa matatizo yake ya kifedha na tatizo la ongezeko la mahitaji ya umeme huku kukiwa na upungufu wa uzalishaji baada ya Dowans kutimuliwa na kadhalika.
Maelezo ya Tanesco yakawagusa wajumbe wa POAC na wakaona ni vyema wakapata maoni ya wenzao wa Kamati ya Nishati na Madini (ya kina Mwakyembe) na kwamba wakaweka wazi katika maazimio yao kwamba kuna umuhimu kwa Tanesco kusaidiwa na serikali katika kununua mitambo mipya hata ikibidi kununua ya Dowans kwa sharti la kuzingatia sheria. Ikiwamo sheria ya manunuzi ya 2004. Kwa makini kabisa kamati imesema, "haijabariki ununuzi wa mitambo ya Dowans" na kwamba kamati ya POAC wala ya Nishati na Madini hazina mamlaka ya kuidhinisha wala kuzuia manunuzi ya Tanesco.
Maelezo ya POAC hayajatofautiana na yale ya Kamati ya Nishati na Madini kwamba hata wao hawana mamlaka ya kuzuia manunuzi. Tofauti ya kamati hizi mbili ni kwamba ile ya POAC ilitaka kukaa pamoja na wenzao wa Nishati na Madini kujadiliana jinsi ya kuisaidia Tanesco kiushauri na ili wapate maelezo ya kuridhisha kuweza kuishauri serikali na ili kuzuia kutokea kwa matatizo yaliyotokea wakati wa Richmond. Suala la kununua au kutonunua ama kutaifisha mitambo ya Dowans lingekuja kujulikana baada ya kukaa pamoja.
Kuna matatizo makubwa matatu ambayo yamesababisha hali hii kufikia hatua ya kuanza kushambuliana na hata kuanza kuibuka kwa tuhuma dhidi ya wabunge husika akiwamo Zitto ambaye imefikia hata kutuhumiwa kuhongwa.
1. Tatizo la kwanza ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na Zitto mwenyewe kujiamini kupita kiasi na kuwaamini waandishi wa habari kupita kiasi. Amezungumza nao na kwa bahati mbaya sana (kwa kujua ama kutojua) waandishi hao wamepotosha kabisa kauli ya Kamati (si ya Zitto) kwa kusema kwamba kamati imebariki/inataka Dowans inunuliwe. Kamati haikusema hivyo.
2. Tatizo lingine ni lile la kauli kwamba kamati ya Nishati na Madini haijawasikiliza Tanesco, nalo limetokana na tafsiri ya baadhi ya waandishi. Maelezo ya wajumbe wa Kamati na Nishati na Madini ni kwamba wamewasikiliza Tanesco kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, ambaye alifika katika kikao cha Desemba 14, 2008. Kawaida waziri akiona amezidiwa ndipo huwaita wataalamu wake (Tanesco) kujieleza. Ngeleja alipomaliza kuwasilisha mbele ya uongozi wa Tanesco na Tanesco kutoka nje kuwaacha wabunge wajadili, Ngeleja angeweza kuomba Tanesco warudi wamsaidie, lakini aliridhika na kukubali. Waandishi wakaandika kwamba Kamati imeikatalia Wizara kununua mitambo. Kamati ya Nishati haijakanusha kama ambavyo kamati ya Zitto haijakanusha, kwa sababu ambazo naomba nizianike kwamba wanasiasa ni waoga sana kubishana na vyombo vya habari. Kimsingi hakuna kamati iliyokataa wala kubariki ununuzi wa mitambo ya Dowans.
3. Tatizo kubwa ambalo sasa limeguswa kiaina na baadhi ya wahusika akiwamo Zitto na Dk. Mwakyembe ni tatizo la kisiasa. Zitto amenukuliwa akisema kuna siasa za makundi, Mwakyembe akasema anaona kama operesheni sangara inaendelea. Hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa linaweza kubadili mjadala kutoka katika hoja za msingi na kuanza kwa SIASA. Kubadilika kwa hoja kutoka tatizo na kwenda kuwa SIASA.
4. Lakini pamoja na kuwa hoja si ya kisiasa, msingi wake unaweza kuwa wa kisiasa zaidi na kwamba Zitto kama mwanasiasa angepaswa kuangalia pia upande wa hatima yake kisiasa zaidi badala ya kutaka kuwa MAKINI kutenda HAKI kwa kutaka kusikiliza pande zote husika. Hilo linahitaji mjadala pekee kwa kuwa Zitto amekuwa na hulka ya kusikiliza hata wale ambao watu hawapendi kuwasikiliza. Hiyo ni hulka nzuri lakini ni HATARI SANA.
Kwa maoni yangu:
Suala la Dowans asili yake ni hoja tete ya Richmond ambayo ilisababisha kuenguliwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha (ambaye yuko kimya sana). Kuanguka kwa Waziri Mkuu ni hatua nzito katika historia ya nchi hii na kulisababisha kuvunjika kwa Baraza zima la mawaziri. Zitto alilumbana na Spika kuhusu hilo na Rais Kikwete alithibitisha maneno ya Zitto kwa kutangaza kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri.
Tukio hilo lilirudisha imani ya umma kwa vyombo vyote vya dola ambavyo walikwisha kupoteza imani navyo na kuona kwamba sasa kumbe hakuna aliye juu ya sheria. Bunge, wabunge, serikali zilipata heshima ndani na nje ya nchi. Sakata la Richmond likawa mtaji mkubwa wa kisiasa kwa wanasiasa ndani ya Bunge na hata kwa Rais. Wapinzani nao waliona kama ushindi kwao. Nchi ilichangamka na masuala mengine kama EPA na kesi za kina Mramba yakafuatia mkondo.
Sasa hivi, yeyote ambaye anathubutu kutaka kubadili HADHI ya Bunge kwa kuhalalisha kwa mlango wa nyuma maovu yaliyotokana na Richmond, atakuwa anairudisha nchi nyuma (si wanasiasa).
Jambo la msingi ni kuzingatia mambo yote ya msingi, ikiwa ni pamoja na kuangalia kwamba Dowans tunawadai bilioni 23, Dowans wametushitaki lakini pia ni kweli kwamba tuna tatizo la UMEME sasa? na Je, ni dharura? Tumejua lini tatizo? Nani awajibike kwa hili? Je, Sheria inasemaje ikiwa mtu amedanganya wakati wa manunuzi? munaendelea kufanya naye biashara? Je, hakuna mitambo mengine hata kwa bei ya ziada kidogo? Tusiponunua Dowans watapeleka wapi mitambo yao? wakinunua wafanyabiashara wengine (hao hao) watamuuzia nani umeme ikiwa tutakuwa na mitambo mipya?
TUZINGATIE: Rostam anamiliki 35% ya Vodacom, Dk. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom, Ngeleja alikuwa mtumishi wa Vodacom.
Huyo nae keshapoteza makali, hana kitu, kuanzia alivyoanza na kuleta uongo, kafuatia kushabikia kununua mtambo wa Dowans, halafu leo leo ahamasishe tukatae kununua mtambo huo!
Opportunists, anaangalia maslahi au fulani kasema nini. Kwa vile kamati ya Zitto ilisema mtambo ununuliwe, basi akaja na kistory eti mtambo ununuliwe kwa vile mwezi wa nne kutakuwa na uhaba wa umeme!
Zitto, Mwanakijiji denounced!
Jeuri ya sitta kuitingisha serikali inatoka wapi?? Je ni mtu makini mwenye misimamo isiyoyumba na kutaka kuona uhuru wa mihimili mitatu ya umma inaheshimiwaaa???
Au ni mwanasiasa aliyepofuka na siasa za muda mrefu na kujijengea himaya ya kutingisha wenzake(serikali) alioshiriki kwa karibu kuwafikisha (mtandao) hapo walipoo...
Kwa hili la richmond/dowans amekuwa kinara sana kuhakikisha serikali na wadau wake (fisadis) hawapati upenyoo...je ana ajenda ya siri??
Recta.
ni kweli tupu maoni yako ila sasa tufanyeje kuondokana na KAULI na KUTENDA?
Binafsi naunga mkono msimamo wa Zitto/Tanesco katika hili kwa sababu tuu wao wanatusaidia kutambua uwezo wa wengine (kamati ya nishati na spika) katika kubishana, umaarufuuu kwenye masuala muhimu...
naomba mwongozo...hivi suala la kamati mbili kutoleana/kujibizana katika vyombo vya habari, pia Spika anajibu kupitia vyombo hivyooo....ni SAHIHI??
Sikufurahia tabia ya Spika (muhimili wa umma) naye kuitisha press conference bila hata kuongea na hao wanaolumbanaaaa....kuna tatizo..
Tusisahau pia tabia ya spika kubwatukaaaaaaa...