Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,590
- 8,718
Mjadala umeisha?
umeisha kwa kumaliza na baba yao sitta kwenye taarifa ya habari ...ameongea copy and paste ya mwakyembe...si wako kambi moja????....hakiya mungu wanamtega kikwete wote hawa kina mwakyembe na sitta et al upande huu...na upande huu CHADEMA wanapuliza puliza halafu baaadaye haoooooo wanajiweka kando wanawaachia moto wao...
patamu hapo ..tuingie mmwaka 2010 na giza tororo.....hakuna anayemtakia kikwete jema kati yao........maaana nasikia arusha na mwanza tayari wanakula mgawo....na hapo hapo utafiti uliotolewa leo kule singida unasema asilimia 98 % ya wakaazi wa vijijini tanzania hawana umeme....
lakini kama kweli tunawadai dowans bilioni 10 .....hawajalipa ..na kama serikali inakosa bilioni 58 za kodi...basi tuikamate na kuitaifisha hiyo mashine ya dowans ...TRA nao walishaukamata mtambo wa AGREKO wanawadai kodi......si pesa zetu jamani....!!!...economy of scales...
Gazeti la Raia Mwema liliandika wiki chache zilizopita kwamba Richmond/Dowans inadaiwa na Serikali/TANESCO kiasi cha shilingi 23 billioni na kama sikosei TANESCO walifungua kesi juu ya hili deni. Cha kushangaza katika kupigia debe ununuzi wa mitambo hiyo hili deni la 23 billioni halizungumziwi kabisa, labda Dowans wamecheza ndiyo maana hilo deni halitajwi kabisa katika hichi kizungumkuti.
Alaa! Baada ya kumsikiliza Sitta na Mwakyembe sasa nimeelewa kwa nini Slaa na Zitto wamenunua ajenda ya Dowans dhidi ya Shelukindo. Kumbe kweli hii ni Operesheni Sangara. Dili ni kufufua ishu ya Richmond bila kuinyanyulia bango Tanesiko ya 'Dakta wa Vijisenti' ili 'Vilongola' walioponea chupuchupu nao pia waingie kitanzini. Si unakumbuka aliyekuwa Waziri Mkubwa alisema nini wakati analalama kuwa 'amedhalilishwa sana' , 'amesononeshwa sana' na 'amefedheheshwa sana'? Alisema hivi: 'Put in on the table, who is Richmond', yaani, 'Iweke wazi mezani, Richmondi ni nani'? Operesheni Sangara ya Dowans-Richmond ya Zitto-Slaa ikifanikiwa basi ukweli wote utawekwa mezani. Hapo ndipo nchi itatikisika hasa. Ole wetu. Namalizia kwa nukuu hii ya Mwalimu Nyerere kutoka kwenye ukurasa wa 46 wa kitabu chake cha 'Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania':
"Narudia: Kumbadili Waziri, hata Waziri Mkuu, si jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa, na Nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa Rais wa Nchi bila kuitikisa Nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa. Maana watu wengine wananong'ona nong'ona kuwajibika kwa Rais kana kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika kumchukulia hatua Rais wa Nchi ni mkasa na balaa kwa Nchi yoyote ile. Ndiyo maana tunatakiwa kuwateua na kuwachagua Marais wetu kwa uangalifu mkubwa; na ndiyo maana wakishachaguliwa, wanatakiwa wajiheshimu na kuwa waangalifu sana" - JKN, 1994
Mwenye sikio na asikie Mwalimu anacholiambia Taifa. Mungu Ibariki Tanzania. Wabariki viongozi wake. Amina.
PM hakuna kitu kuhusu ZITTO, ameshaingia mkenge na mimi binafsi ile blank support niliyokuwa natoa kwa Dr. Slaa na kina Zitto naiamishia kuanzia leo kwa Dr. Mwakyembe, Mama Kilango na Seleli.
Zitto tulikuwa naye hapa for almost 4 days tukimpa mambo ya jikoni na mikorogo itakayotokea, lakini katupuuza na kututukana.
Sasa kweli ukimpa hayo mahojiano mtu ambaye hajui Tanzania, ukamuambia guess yupi ni kutoka chama cha upinzani, si atapick Dr. mwakyembe??
Dr. Mwakyembe hapa anatetea maslahi ya nchi na sisi wananchi, na Zitto anatetea maslahi ya Dowans, simple as BLACK and WHITE.
Halafu Mh. Zitto usipende kuchanganya mambo kwa kumention tu vitu unavyoambiwa eti serikali inakosa bilioni 58 watu wa migodi kwenye mafuta wanayotumia kwenye private generator zao, je kisa ni sababu hatujanunua mitambo ya Dowans au kisa ni misamaha ya kijinga serikali inayotoa na jie bunge kuridhia??? Unafikiri hata kukiwa na umeme, watu wa migodi watatupa generator zao au watatumia hiyo loophole ya tax refund kwenye mafuta ya hizo generator??? Give me a break!!!
huu mchezo bado mbichi...nia za kina zitto na mwakyembe ni tofauti na wote ...mwisho wake hautabiriki..ila itabidi serikali ya kikwete itafute njia muafaka kivyake ..tena inayofuata utaratibu ili tusiingie gizani....akinunua mitambo kina mwakyembe wanampiga bao...tukiingia gizani ..CHADEMA wanapiga bao...
kwa kifupi kwa kikwete ugali moto ...mboga moto!!!!
subiri utakuja kuniambia..
mimi binafsi ile blank support niliyokuwa natoa kwa Dr. Slaa na kina Zitto naiamishia kuanzia leo kwa Dr. Mwakyembe, Mama Kilango na Seleli.
Dr. Mwakyembe hapa anatetea maslahi ya nchi na sisi wananchi, na Zitto anatetea maslahi ya Dowans, simple as BLACK and WHITE.
........leo hii katufanya MABWEGE.......damn!
Mwakyembe kachemsha sana....na hasa pale anapozungumzia "operation Snagara" na pia kuhusu "Posho"........sikutegemea hii toka kwake.......nilitgemea angetuchambulia vipengele vya sheria za manunuzi (yeye akiwa mwanasheria) pamoja na kutupa facts zengine ambazo wananchi hatuzijui kuhusiana hii saga........leo hii katufanya MABWEGE.......damn!
Mimi nimemsikiliza tena. Yeye kasema kuwa licha ya hali ya uzalishaji umeme kuwa nzuri etc, bado kuna upungufu wa kama 150 na huu ni lazima ujazwe. Hayo uliyoyasema kuwa hakuna ulazima kwa kweli sijayasikia. In fact anasisitiza kuwa mitambo hii ya Dowans inaweza kutuvusha hapo hivi sasa ili tusiingie gizani. Urgument kuwa nakisi hiyo imekuwepo siku zote haimaanishi kuwa iendelee kuwepo na isishughulikiwe kwa haraka.
lakini kama kweli tunawadai dowans bilioni 10 .....hawajalipa ..na kama serikali inakosa bilioni 58 za kodi...basi tuikamate na kuitaifisha hiyo mashine ya dowans ...tra nao walishaukamata mtambo wa agreko wanawadai kodi......si pesa zetu jamani....!!!...economy of scales...