Dowans: Another Richmond in making?

Nashauri tu,tukitaka kuwa na consistent Debate,we must avoid childish speculation.

Kwanini tutangulize hisia za mtu kununuliwa? kwa mtindo huu,hatuwezi kuwa na mjadala wenye tija.Let us just dwell katika debate
 

yaani umepigilia msumari.
Kuna haja gani sasa ya kuwa na upinzani,kwani nichague chadema wakati baba letu ccm lipo. Hawana madaraka wanahongwa, wakiwanayo itakuwaje. Harafu haweajui hata kujishusha. Haji hata hizo kazi anazodai anafanya nikwasababu tumemuweka juu.

Time will tell.

Hawasi wenzetu tena na naona bora washikilie msimamo wao tu maana hata wakibadilika tumeshawaona hawana maana.
 

Sasa Ngereja wakati akitoa azma yaserikari kununua hiyo mitambo chakavu alikuwa bado hajapata ushauri wa kamati ya bunge au?
 
I am really sad I have missed this very very interesting debate. However I believe there's more to this than meets the eye. If I were Zitto, I would try as much as I can to stay out of this fray. From afar I see a tsunami building and a fall-out that is inevitable - young Zitto might soon not have a leg to stand on. The key players are pushing him on while they stay on safe ground and he, to their delight, is dancing to their tune. They have been in this game for well almost two decades and this new young man is an exhilarating find in their search for freshness.

Dowans, Dowans, Dowans...who the heck is Dowans - reminds me of the Anglo Leasing of Kenya. It has no face yet it exists and enters into business contracts with the government of the United Republic of Tanzania worth billions. It reminds me of Kagoda - no face but draws billions from the Central Bank. Would Zitto bless Kagoda if it came to our rescue and offered us a panacea out of our predicament ? For someone from our own elective legislative assembly, to come out and support this relationship that smells like rotten fish, is itself degrading enough.

We are going to see a lot of these underhand dealings as we move closer and closer to 2010 - history has a bad habit of repeating itself !! Poor Zitto !!
 
Nimepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja kuhusu suala la ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme ambayo inauzwa na kampuni ya Dowans. Kuna mambo kadhaa ambayo bila ya shaka wengi wetu hatujayasoma kwenye magazeti au tumeyasoma akiwa amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Kwa sababu sisi hatutafuti habari kutoka nukuu za waliosikia au simuliwe tunakwenda moja kwa moja kwa wenye habari wenyewe. Usikose kijarida cha Cheche kesho na kusikiliza mahojiano hayo na Bw. Ngeleja na uone kama na wewe unaweza kushawishika na msimamo wa serikali.

Snapshots:

- Asema siyo lazima kununua mitambo ya Dowans, ni ulazima wa hali ya mahitaji iliyopo

- Asema Dowans ndiyo wametangaza tenda ya kuuza mitambo yao hivyo sheria ya PPRA inaingia kwa namna tofauti

- Arudia suala la kununua mitambo iliyotumika, asema siyo 'geni'

- Atolea mfano hali ya kiuchumi Marekani na jinsi serikali ya huko ilivyoingilia hali ya uchumi wake..

za zaidi sana...
 
Nashauri tu,tukitaka kuwa na consistent Debate,we must avoid childish speculation.

Kwanini tutangulize hisia za mtu kununuliwa? kwa mtindo huu,hatuwezi kuwa na mjadala wenye tija.Let us just dwell katika debate

Usiwalaumu.... Kuna cha zaidi ambacho watu hawajaki post humu??... Akili kichwani mwako kuchagua pumba na mchele. Waache waliokwisha fikia conclusion wajieleze. Watu wameshaumwa na nyoka. Si mara moja, wala mara mbili, wala mara tatu, mara nyingi tu!

Kukatwa PAYE ambayo ni almost 1/3 ya mshahara wako kila mwezi halafu hio hela yenyewe inaenda kunufaisha wezi wetu, lazima watu wakomae na viongozi wao.
 
Is being pragmatic means kununua zigo la lililiopatikana kifisadi? Kwa hiyo kamati yenu inakubaliana na ufisadi? Kisheria inakuwaje?

Zigo la kifisadi tena hao Dowand wanadaiwa na TANESCO/Serikali shilingi 23 billioni lakini hakuna anayezungumzia hili wameng'ang'ania tu kutaka serikali inunue tu hili zigo lilijaa utata wa hali ya juu. Hapa kuna mengi yatakayokuja kufichuka haiwezekani watu washupalie ununuzi wa mitambo hiyo hivi hivi tu.
 

ulipomuuliza kuwa, downs watatangazaje tenda ya kuuza mitanmbo amabayo inashikiliwa na serikali ili ije kuwa fidia pindi wakishindwa kesi waliyo fungua dhidi ya serikali kasema nini? Au na wewe maswali ayko leo yalikuwa ya kupangwa mzee.

Tutapenda tujue kabisa maswali uliyomuuliza na majibu yake vingine mchezo huu utakuwa unachezwa na watu wengi. Wenzio wametangulia inawezekana na wewe ukawa umefata, bila ya maswali uliyomuuliza, na majibu aliyotoa kuyaweka kwenye cheche hatutakuelewa.
 

mbona una wasiwasi, mimi siandiki maswali wala majibu yake, utasikia mwenyewe haya mambo ya kunukuliwa ndiyo niliyoyakwepa. Kama kuna maswali ya ziada baada ya wewe kusikia niandikie halafu tutamtafuta kumuuliza tena.
 
Mwana kijiji, kama na wewe unataka kuwa Zitto, sema mapema tukuachie JF yako. Hashawishiki mtu hapa.
 
Mwana kijiji, kama na wewe unataka kuwa Zitto, sema mapema tukuachie JF yako. Hashawishiki mtu hapa.

Maneno mengi ya nini jamani??,MMK=Zitto?,how?,MMK kafanya mahojiano na Ngeleja na yapo KLHN cha msingi ni kusubiri na kusikiliza what Ngeleja said badala ya kuanza kulialia kihivi...So let's wait and listen
 
mbona una wasiwasi, mimi siandiki maswali wala majibu yake, utasikia mwenyewe haya mambo ya kunukuliwa ndiyo niliyoyakwepa. Kama kuna maswali ya ziada baada ya wewe kusikia niandikie halafu tutamtafuta kumuuliza tena.

Mambo yamenavyokwenda katika issue ya DOWNS hatumuamini mtu sasa hivi. wanaliosababishia wasiwasi wa kutomwamini mtu bila shaka unawajua. wanatoa kauli tata kila wakati.
 

Kama wanataka kununua mtambo mmoja chakavu kwa Tshs 70 billion kwa nini wasinunua toka GE mitambo 2 mipya kwa gharama hiyo hiyo wangepata 200MW badala ya 100MW. GE wanazo mitambo mipya tayari kwenye stock. kwa nini wanang'ang'ania mtambo chakavu toka dowan. Na dowan siyo manufacture wa hii mitambo, GE ni manufacture na wangepata na warrant for 5 years plus commissioning for another 30 years. shipping cost ya 100MW toka USA mpaka Tanzania by ship line siyo zaidi ya US$100,000.00. Pia kusoma hakumaanishi kwamba unaelewa na kukifanyia kazi, Chenge from Harvard Law Shool, si unaona madudu anayoyafanya, Dr. Rashidi wote hawa ni wasomi wazuri, angalia njisi walivyoshikwa kama kuku.
 
Zitto umekwepa swali langu mara kadhaa. Ninakuuliza tena. Tukiweka pembeni siasa za kamati and all that, wewe kama informed representative utasimamia upande gani katika mjadala huu? Utaunga mkonoi ununuzi au lah? au bado hauna taarifa zinazokuwezesha kuwa na uamuzi?

Usipojibu this time sitakuuliza tena.
 
sasa huu ndiyo wasiwasi wenu.. ni kutokuwa open minded kama mtu hayuko tayari kushawishiwa. Mimi nimemsikiliza kwa kirefu na hajabadilisha msimamo wangu zaidi ya kuuthibitisha na kuuweka sawasawa.

Mtu makini atasema "i reserve my judgment hadi nimsikie" na baada ya hapo nitakuwa na picha ya kutosha kuweza kujua.

Wangapi wanajua kuwa Serikali haiwezi kutangaza zabuni au kuishindanisha Dowans katika suala hili kwa sababu habari zilizoripotiwa hazijaripotiwa kwa usahihi?
 
Zitto,
Naona uko hapa ndani. Je unaweza kutusaidia kwa haraka haraka huu utata? Mie nimefika sehemu sielewi nini hasa kinaendelea hasa ukisoma maelezo yako, Mwakyembe na Selelli. Utata mkubwa na sitaki kuhumu mtu kwa hili hadi nielewe maelezo ya wengi.
Hivi kwa nini kutotumia maelezo ya wengine kuwa kiwanda cha GE kina ma generator ambayo watu walikuwa wameagiza na sasa wamekwama kuchukua. Tunaweza kuchukua mpya kwa mikataba mizuri hasa ukichukulia kuwa USA wana haha kuuza bidhaa zao.
Itakuwa vema ukitujulisha kwa hili ili ambao tuna imani na wewe kuwa "hawajakununua" basi tuendeleze imani hiyo.
 


Kokolo, nakumbuka tulilizungumza hili na ulileta insight nzuri sana wakati tunazungumzia mambo ya UPS. Hadi hivi sasa nadhani tunachotakiwa kufanya ni kujenga hoja kuwa kupata mitambo mipya kutoka kwa watengenezaji ni bora na ina mantiki ya kifedha kuliko kununua toka kwa Dowans.
 

Suala la habari kutoripotiwa kwa ushaihi linawezekana(nina uhakika ndio hivy),maana baadhi ya waandishi wetu wa Tanzania tunawajua jinsi walivyo na uwaezo wa kupotosha habari/kupindisha ka malengo wanayoyajua wao...So let's wait and listen alichokisema Waziri Ngeleja
 

hii inaitwa hekima.
 
Wezi watupu hao.
Yani wametuibia mzunguko wa kwanza tena wanatuibia kwa mzunguko wa pili !! walai tena duu!!!!!!!!!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…