Dokta Janabi aweke mfumo nzuri wa taarifa za tahadhari za afya..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Niseme kuwa hizi taarifa anazozitoa mara Kwa mara kuhusu tahadhari mbalimbali za afya ...ni nzuri Sana lakini pia zinaibua maswali mbalimbali..
Ni vizuri Dkt Janabi au Muhimbili kama Taasisi waweke mfumo nzuri wa taarifa......ili mtu akihitaji source iwepo...na asitokee mtu akapotosha ..hizo taarifa....

Taarifa ambazo nyingi zinatufikia kww njia ya clips za dakika chache kwenye social media zinaleta maswali mengi na hata kuzua taharuki....


Mfano aliposema kunywa maji mengi ni hatari Kwa afya ...hii taarifa umekuja leta mshtuko Kwa watu wengi.....Kwa sababu madaktari Wengi Kwa miaka mingi wamekuwa wanasisitiza watu kunywa maji mengi...na hata kusema yasipungue Lita 2 Kwa siku.....sasa tafsiri ya maji mengi yanayofaa kiafya ni ipi? Na maji mengi ambayo ni hatari Kwa afya ni ipi???..
Tafiti zipi zimehalalisha kipi?
Zimefanyika wapi?
Hatari hizo kwa mujibu wa mtaalam yupi?..

Nafikiri Hili na mengine yanahitaji majibu ya kina ....

Nashauri kiwepo na website ama ya kwake binafsi dokta Janabi au ya Taasisi ya kujibu maswali mbalimbali...yanayojitokeza...

Juzi nimeona la pilau na soda...nimejiuliza kama ni taarifa genuine .na kama nna maswali niyapeleke wapi?...kwanini pilau?
Na sio biriani?kwanini soda na sio juice yeyote ya kiwandani?

Je maji ya kiwandani je?

Vyakula vingine na soda?

Haya na maswali mengine binafsi nafikiri iwepo platform sahihi ya watu tupate majibu......vinginevyo hizi taarifa zitakuwa zinaleta taharuki na zinatoa mwanya wa watu wengine kupotosha...
 
Capture.PNG
 
  • Kicheko
Reactions: rr3
Issue nyingine ni banters ambazo zilianzia huko X (zamani Twitter) baada ya yeye kutoa ushauri wa kiafya ambao ulionekana ni mgumu kufatwa, sio kila unachoona ni kweli kakisema yeye.
 
Issue nyingine ni banters ambazo zilianzia huko X (zamani Twitter) baada ya yeye kutoa ushauri wa kiafya ambao ulionekana ni mgumu kufatwa, sio kila unachoona ni kweli kakisema yeye.
Yes lakin akiweka mfumo mazuri angalau itakua rahisi...mfano website yake official
 
Back
Top Bottom