Tukifuata ushauri wa professor Janabi tutaangamia kwa njaa

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,864
Wasalaam wakuu!

Kwanza kabisa Nakubaliana na ushauri wote wakitabibu kuhusu aina sahihi ya chakula na namna nzuri ya ulaji kutoka kwa Daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo professor mohamed Yakub Janabi.

Namimi baada yakumsikiliza na kuanza kufuatilia miongozo yake nikaamua kubadili aina yangu ya ulaji ili niendane na matakwa ya msomi huyu. Na sasa ni wiki ya 3 tangu nianze kufuatana na miongozo ya Janabi na nasema wazi kuwa nimenyoosha mikono juu , hii ni Baada ya kuzidiwa na njaa kisha kupata kizungu zungu na kuanguka ghafla ofisini.

Baadhi ya miongozo ya Professor huyu msomi

1.Kunywa bia moja masaa yasiyopungua mawili na usiongee wakati unainywa hiyo bia

2.kula mara moja tu, ukizidisha iwe mara mbili na chakula kisizidi ujazo wa kiganja cha mkono wako.

3. ugali ni hatari kwa afya ya moyo na unadumaza akili

4. Professor anasema yeye hajanywa juice ya aina yoyote miaka zaidi ya 15, lakini anasema tusile sukari, chumvi, nyama nyekundu, nyama nyeupe tule kwa kiasi kidogo sana , samaki wasio na magamba wanamafuta mbaya, lakini samaki wa maji chumvi nao ni tatizo kwa moyo. Janabi anaenda mbali nakushauri mboga zote za majani ziliwe zikiwa mbichi. "Kweli kisamvu nikitafune kikiwa kibichi professor?"

Literally ni kama professor Janabi yupo katika kampen ya #kataa chakula sababu anapingana na kila mlo uliozoeleka kwa WaTanzania. Nashauri asipuuzwe ila asitiliwe maanani sana.
 
Ushauri wowote wa jinsi ya kula chakula, jinsi ya kufanya mazoezi, jinsi ya kula dawa, na mambo mengine muhimu yoyote ya kiafya ya jamii, hautakiwi kutolewa kiujumla.

Ndiyo maana wenzetu baada ya kutoa ushauri, husisitiza sana suala la kwamba kila mtu yuko tofauti, usiufanyie kazi ushauri kabla ya kuongea na daktari wako.

Kila mtu ana tofauti, na hivyo, anaweza kuhitaji mbinu tofauti.

Mfano, mtu mwenye uzito uliozidi, anayefanya kazi ofisini, anayekaa sana kwenye kiti, mwenye gari, ambaye hana mizunguko mingi kwa siku, anaweza kuangaliwa na daktari wake akaambiwa aongeze mazoezi na kupunguza caloric intake na ushauri huu ukamsaidia.

Lakini, mtu ambaye yuko underweight, analima kwa kutumia nguvu kubwa sana siku nzima, ana mizunguko mingi, kazi yake tu ni sawa na mazoezi, inahitaji nishati kubwa sana, na yeye utamwambia apunguze kula na aongeze mazoezi? Hai make sense.

Dr. Janabi anapotoa ushauri, huwa anasisitiza watu waongee na madaktari wao kwanza kabla ya kupanga jinsi ya kula au kufanya mazoezi?
 
Ya janabi ni ya watu wa maisha ya AC ofisi nyumbani.
Na sio wauwa winga yaaani watembea kwa miguu kilometers zaidi ya kumi kwa siku ndo maisha ya wengi.
Sukari inajichoma yenyewe
Mkuu,

Kuna tofauti kubwa sana hapo kati ya maisha ya hao watu wa aina hizo mbili.

Kuna wengine wanahitaji kuzidisha kula hata zike daily caloric intake hawafikishi.
 
Uamuzi ni wako:

1000090097.jpg
 
Wasalaam wakuu!

Kwanza kabisa Nakubaliana na ushauri wote wakitabibu kuhusu aina sahihi ya chakula na namna nzuri ya ulaji kutoka kwa Daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo professor mohamed Yakub Janabi.

Namimi baada yakumsikiliza na kuanza kufuatilia miongozo yake nikaamua kubadili aina yangu ya ulaji ili niendane na matakwa ya msomi huyu. Na sasa ni wiki ya 3 tangu nianze kufuatana na miongozo ya Janabi na nasema wazi kuwa nimenyoosha mikono juu , hii ni Baada ya kuzidiwa na njaa kisha kupata kizungu zungu na kuanguka ghafla ofisini.

Baadhi ya miongozo ya Professor huyu msomi

1.Kunywa bia moja masaa yasiyopungua mawili na usiongee wakati unainywa hiyo bia

2.kula mara moja tu, ukizidisha iwe mara mbili na chakula kisizidi ujazo wa kiganja cha mkono wako.

3. ugali ni hatari kwa afya ya moyo na unadumaza akili

4. Professor anasema yeye hajanywa juice ya aina yoyote miaka zaidi ya 15, lakini anasema tusile sukari, chumvi, nyama nyekundu, nyama nyeupe tule kwa kiasi kidogo sana , samaki wasio na magamba wanamafuta mbaya, lakini samaki wa maji chumvi nao ni tatizo kwa moyo. Janabi anaenda mbali nakushauri mboga zote za majani ziliwe zikiwa mbichi. "Kweli kisamvu nikitafune kikiwa kibichi professor?"

Literally ni kama professor Janabi yupo katika kampen ya #kataa chakula sababu anapingana na kila mlo uliozoeleka kwa WaTanzania. Nashauri asipuuzwe ila asitiliwe maanani sana.

Hivi nani kasema tunatakiwa kula mara tatu kwa siku? Ni makampuni sio Madaktari na ubongo unakumbuka na ndiyo maana unapata njaa. Lakini milo inatakiwa kula miwili tu. Saa nne au saa tano asubuhi na jioni kabla ya saa mbili. Baada ya chakula cha jioni kama ni chai au kahawa iwe ya rangi bila sukari wala maziwa mpaka asubuhi saa nne au saa tano yaani masaa 14-16 kila siku. Nimefanya hivi kwa miaka zaidi ya miwili sasa na madaktari wengi wanashauri hivi. Njaa ni akili yako tu ukishafanya wiki moja mwili unazoea. Usikofanya hivi hasa kuanzia 45 years unahatari ya kupata kisukari
 
Kumbe kushinda njaa inasaidia sana?!
 
Wasalaam wakuu!

Kwanza kabisa Nakubaliana na ushauri wote wakitabibu kuhusu aina sahihi ya chakula na namna nzuri ya ulaji kutoka kwa Daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo professor mohamed Yakub Janabi.

Namimi baada yakumsikiliza na kuanza kufuatilia miongozo yake nikaamua kubadili aina yangu ya ulaji ili niendane na matakwa ya msomi huyu. Na sasa ni wiki ya 3 tangu nianze kufuatana na miongozo ya Janabi na nasema wazi kuwa nimenyoosha mikono juu , hii ni Baada ya kuzidiwa na njaa kisha kupata kizungu zungu na kuanguka ghafla ofisini.

Baadhi ya miongozo ya Professor huyu msomi

1.Kunywa bia moja masaa yasiyopungua mawili na usiongee wakati unainywa hiyo bia

2.kula mara moja tu, ukizidisha iwe mara mbili na chakula kisizidi ujazo wa kiganja cha mkono wako.

3. ugali ni hatari kwa afya ya moyo na unadumaza akili

4. Professor anasema yeye hajanywa juice ya aina yoyote miaka zaidi ya 15, lakini anasema tusile sukari, chumvi, nyama nyekundu, nyama nyeupe tule kwa kiasi kidogo sana , samaki wasio na magamba wanamafuta mbaya, lakini samaki wa maji chumvi nao ni tatizo kwa moyo. Janabi anaenda mbali nakushauri mboga zote za majani ziliwe zikiwa mbichi. "Kweli kisamvu nikitafune kikiwa kibichi professor?"

Literally ni kama professor Janabi yupo katika kampen ya #kataa chakula sababu anapingana na kila mlo uliozoeleka kwa WaTanzania. Nashauri asipuuzwe ila asitiliwe maanani sana.
Huyu mzee atasema tuache kupumua maana hewa ina moshi wa viwanda
 
Hizi habari za madhara ya kulakula zinawahusu zaidi wenye uwezo wa kulakula chochote na muda wowote kwa kuwa wana hela za kutosha kulakula hovyohovyo na njaa hawaijui. Sasa wale wa kubangaiza kula mlo mmoja tu ni shughuli pevu madhara ya kulakula hovyohovyo watayapataje?
 
mnawezahisi profesa yuko serious kumbe yuko ktk kampeni ya kuzuia wageni nyumbani kwake😀😀😀.

fikiria huyu ni shemeji yako au baba yako mdogo,ukienda kwake utakaa siku ngapi🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom