Sikubaliani na Profesa Janabi

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Mwili una mifumo imara ya kutambua mapungufu na mahitaji yake.

Kwa hiyo jaribio lolote la kuuelekeza (to dictate) mwili nini cha kufanya ni kuharibu miitikio ya kimaumbile.

Mwili hutoa viashiria mbalimbali unapokuwa na mahitaji ama mapungufu;

1. Kiu.........maji.
2. Njaa....chakula.
3. Miayo....uchovu.
4. Usingizi... Mapumziko.
N.k.

Kwahiyo kula unaposikia njaa, kunywa maji unaposikia kiu, nenda haja kubwa unapobanwa na haja..

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.

Hujawahi kusikia madaktari wakishauri watoto walale masaa 8+, watu wazima masaa 6+, watu wasibane mkojo muda mrefu, watu wapumzike vya ktosha kupunguza uchovu, n.k?

Sasa kwanini unapokuwa na uhitaji wa chakula iwe nongwa?

Sikubaliani na Prof. Janabi kuhusu nadharia yake ya mahusiano ya kisukari na vyakula. Ninachokiona ni kwamba wazungu wanataka kutuhamishia kwenye mfumo mpya wa maisha. Ni hao hao wazungu ndiyo walikuja na nadharia ya milo 4 kwa siku, sasa wanaipiga vita. What a contradiction!

Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni
 
Janabi anazungumza kulingana na uzoefu WA wagonjwa anaowatibu.

Overweight na obese based disease ni vitu serious.

Vyakula tunavyokula ni salama?
Ni natural?

Au mbegu za maabara zenye side effects tele.

Mbolea je ni natural?

Hakuna side effects za madawa?

Unasemaje ukisikia njaa Tu ule kumbe tunakula vyakula vyenye sumu nyingi?
 
Kwa nyumbani Tanzania, ukiondoa hawa kuku wa haraka haraka, vyakula vyetu bado ni organic sana.

Kwahiyo madhara yatokanayo na vyakula kwetu bado.

Hii Dunia kuna maeneo vyakula wanavyokula usiombe!

Ni matakataka tupu
 
Janabi anazungumza kulingana na uzoefu WA wagonjwa anaowatibu...
Overweight na obese based disease ni vitu serious...
Umenena vema mkuu, kuna issue ya madawa haiongelewi sana lkn ndiyo chanzo cha magonjwa mengi sana hapa nchini.

Kuna tatizo kwenye prescription, matumizi, uhifadhi, na usalama wa dawa. Bado tuko nyuma sana ktk maeneo haya.
 
Mbona maelezo yako yanalandana na maelezo ya Prof Janabi?

Yeye anasisitiza watu waache kula hovyo. Wale pale wanapohisi njaa. Maji wanywe pale wanapohisi kiu. Si kwa sababu ni saa saba ni muda wa lunch basi unaenda kubugia hata kama husikii njaaa.

Jioni imefika, mwili hauhitaji tena chakula kwa kiwango kikubwa. Kula chakula kidogo subiri kidogo kisha kapumzike. Watu wanakula chapati 3, maharage ya nazi, maji lita moja, juice glass moja, matunda, alafu anaenda kulala.

Ukiuliza, eti shughuli ipo usiku. Akilala ni kujamba tu puup, shuuu, triiii, popompoo. Shughuli yenyewe kimoja chali.

Anachokosea kwa mbali Prof Janabi ni kushindwa kuweka bayana kuwa kuna makundi kutokana na majukumu yao wanapaswa kula kiwango cha chakula chenye wanga. Wafyatua matofali, wajenga madaraja na barabara na kupasua magogo, si sawa na watu wanaokaa mezani kuzungusha makalio.

Kila kundi lipate chakula kulingana na mahitaji ya mwili kwa muda husika.

Atakuja kijana wa hovyo mshamba_hachekwi aseme mimi ni Chawa.
 
Janabi anazungumza kulingana na uzoefu WA wagonjwa anaowatibu.

Overweight na obese based disease ni vitu serious.

Vyakula tunavyokula ni salama?
Ni natural?

Au mbegu za maabara zenye side effects tele.

Mbolea je ni natural?

Hakuna side effects za madawa?

Unasemaje ukisikia njaa Tu ule kumbe tunakula vyakula vyenye sumu nyingi?
Acha kula sasa tukusikie! Infwakti mnashabikia ujinga!
 
Kwa nyumbani Tanzania, ukiondoa hawa kuku wa haraka haraka, vyakula vyetu bado ni organic sana.

Kwahiyo madhara yatokanayo na vyakula kwetu bado.

Hii Dunia kuna maeneo vyakula wanavyokula usiombe!

Ni matakataka tupu
Organic sana? Tafsiri yako ni ipi?

Tanzania haswa Dar es Salaam, vyakula wanavyokula vina sumu kwa kiwango kikubwa. Mboga mboga na viungo vinapigwa viua wadudu leo, kesho vinachumwa na kuuzwa sokoni.

Mbolea zinatumika zenye kushurutisha mmea ukue kwa haraka ili mkulima auze apate fedha.

Sijui ni nchi gani upo, ila nchi za Ulaya wapo serious sana katika kuzingatia afya za walaji. Mpaka kwenda kwa walaji chakula hupitia katika hatua kadhaa za uthibiti.

Mara kibao Watanzania wenzako unaodai bado wanakula vitu organic, wanaomba kusafirisha vyakula haswa mboga mboga kwenda nje. Ni wachache sana wanafaulu, why? Kwa sababu vyakula hivyo vinakosa sifa ya kuliwa na binadamu.
 
Umenena vema mkuu, kuna issue ya madawa haiongelewi sana lkn ndiyo chanzo cha magonjwa mengi sana hapa nchini.

Kuna tatizo kwenye prescription, matumizi, uhifadhi, na usalama wa dawa. Bado tuko nyuma sana ktk maeneo haya.
Sidhani kama anazungumzia madawa hayo
 
Mwili una mifumo imara ya kutambua mapungufu na mahitaji yake.

Kwahiyo jaribio lolote la kuuelekeza (to dictate) mwili nini cha kufanya ni kuharibu miitikio ya kimaumbile.

Mwili hutoa viashiria mbalimbali unapokuwa na mahitaji ama mapungufu;

1. Kiu.........maji.
2. Njaa....chakula.
3. Miayo....uchovu.
4. Usingizi... Mapumziko.
N.k.

Kwahiyo kula unaposikia njaa, kunywa maji unaposikia kiu, nenda haja kubwa unapobanwa na haja..

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.

Hujawahi kusikia madaktari wakishauri watoto walale masaa 8+, watu wazima masaa 6+, watu wasibane mkojo muda mrefu, watu wapumzike vya ktosha kupunguza uchovu, n.k?

Sasa kwann unapokuwa na uhitaji wa chakula iwe nongwa?

Sikubaliani na prof. Janabi kuhusu nadharia yake ya mahusiano ya kisukari na vyakula. Ninachokiona ni kwamba wazungu wanataka kutuhamishia kwenye mfumo mpya wa maisha. Ni hao hao wazungu ndiyo walikuja na nadharia ya milo 4 kwa siku, sasa wanaipiga vita. What a contradiction!

Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni
Dr Janabi ni super specialist kwenye internal medicine.

Vipi kuhusu wewe dume jike una wasifu gani kuhusu masuala ya afya ili tuache kumsikiliza Prof Janabi tukusililize wewe dume jike wa JF?
 
Mwili una mifumo imara ya kutambua mapungufu na mahitaji yake.

Kwahiyo jaribio lolote la kuuelekeza (to dictate) mwili nini cha kufanya ni kuharibu miitikio ya kimaumbile.

Mwili hutoa viashiria mbalimbali unapokuwa na mahitaji ama mapungufu;

1. Kiu.........maji.
2. Njaa....chakula.
3. Miayo....uchovu.
4. Usingizi... Mapumziko.
N.k.

Kwahiyo kula unaposikia njaa, kunywa maji unaposikia kiu, nenda haja kubwa unapobanwa na haja..

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.

Hujawahi kusikia madaktari wakishauri watoto walale masaa 8+, watu wazima masaa 6+, watu wasibane mkojo muda mrefu, watu wapumzike vya ktosha kupunguza uchovu, n.k?

Sasa kwann unapokuwa na uhitaji wa chakula iwe nongwa?

Sikubaliani na prof. Janabi kuhusu nadharia yake ya mahusiano ya kisukari na vyakula. Ninachokiona ni kwamba wazungu wanataka kutuhamishia kwenye mfumo mpya wa maisha. Ni hao hao wazungu ndiyo walikuja na nadharia ya milo 4 kwa siku, sasa wanaipiga vita. What a contradiction!

Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni
Ila kweli jogging ama kukimbia inaleta madhara ikifanywa bila utaratibu... Mzee Bayi na wanariadha wengine wastaafu wanasumbuliwa sana na miguu hasa kwenye magoti. Kama unafanya jogging jitahidi sana kula bamia au chochote kile kitachosaidia kupata lubricant kwenye miguu hasa magotini. Wale wanaosema wamekimbia zaidi ya 5km wanajihatarisha sana.
 
Mkuu ni kwa namna gani bamia inaweza kuleta lubricant kwenye Joints , nataka kujifunza
 
Mbona maelezo yako yanalandana na maelezo ya Prof Janabi.

Yeye anasisitiza watu waache kula hovyo. Wale pale wanapohisi njaa. Maji wanywe pale wanapohisi kiu. Si kwa sababu ni saa saba ni muda wa lunch basi unaenda kubugia hata kama husikii njaaa.

Jioni imefika, mwili hauhitaji tena chakula kwa kiwango kikubwa. Kula chakula kidogo subiri kidogo kisha kapumzike. Watu wanakula chapati 3, maharage ya nazi, maji lita moja, juice glass moja, matunda, alafu anaenda kulala.

Ukiuliza eti shughuli ipo usiku. Akilala ni kujamba tu puup, shuuu, triiii, shughuli yenyewe kimoja chali.

Anachokosea kwa mbali Prof Janabi ni kushindwa kuweka bayana kuwa kuna makundi kutokana na majukumu yao wanapaswa kula kiwango cha chakula chenye wanga. Wafyatua matofali, wajenga madaraja na barabara na kupasua magogo, si sawa na watu wanaokaa mezani kuzungusha makalio.

Kila kundi lipate chakula kulingana na mahitaji ya mwili kwa muda husika.

Atakuja kijana wa hovyo mshamba_hachekwi aseme mimi ni Chawa.
Wewe ni Dr wa mifugo au binadamu? Umeupiga mwingi. Big up
 
Mwisho wa siku tujifunze kujua miili yetu inahitaji nn.

Mwili wako sio sawa na wa janabi au sio sawa na wangu. Na ndio maana mm na wewe tunaweza kuumwa ugonjwa mmoja ila tukapewa dawa tofauti kutokana na reactivity ya miili yetu.

Nilishajaribu mambo mengi, hata hio Janabi anayosema pamoja na intermittent fasting, lkn nikaona haifanyi kazi kwangu. Ila nilishakua na boss ambae yeye intermittent fasting ni kama desturi kwake, na huwa anakiri inamsaidia hata kuwa productive.

Hivi hujawah kukutana na watu ambao dakika kadhaa baada ya kupata breakfast wanaanza kupata usingizi na uchovu, vile vile kuna watu bila breakfast siku nzima haiendi.

Kwa hio tujifunze kujua miili yetu inataka nn na kuenenda namna inavyotaka hasahasa kwenye swala la lishe na mazoezi.
 
Organic sana? Tafsiri yako ni ipi?

Tanzania haswa Dar es Salaam, vyakula wanavyokula vina sumu kwa kiwango kikubwa. Mboga mboga na viungo vinapigwa viua wadudu leo, kesho vinachumwa na kuuzwa sokoni.

Mbolea zinatumika zenye kushurutisha mmea ukue kwa haraka ili mkulima auze apate fedha.

Sijui ni nchi gani upo, ila nchi za Ulaya wapo serious sana katika kuzingatia afya za walaji. Mpaka kwenda kwa walaji chakula hupitia katika hatua kadhaa za uthibiti.

Mara kibao Watanzania wenzako unaodai bado wanakula vitu organic, wanaomba kusafirisha vyakula haswa mboga mboga kwenda nje. Ni wachache sana wanafaulu, why? Kwa sababu vyakula hivyo vinakosa sifa ya kuliwa na binadamu.

Ulaya gani unayosema wanazingatia afya ya walaji? Wako na vyakula tofauti lakini asilimia kubwa ni poison. Vyakula wanavyokula Tanzania Ulaya, chukulia mfano kuku tu, bei yake huwezi kugusa.

Kwenye maduka yao labda ununue matunda, mboga mboga na grains. Vingine vyote ni garbage
 
Kwa nyumbani Tanzania, ukiondoa hawa kuku wa haraka haraka, vyakula vyetu bado ni organic sana.

Kwahiyo madhara yatokanayo na vyakula kwetu bado.

Hii Dunia kuna maeneo vyakula wanavyokula usiombe!

Ni matakataka tupu
Vyakula organic ni vipi??
Vikiwa organic ukila bila utaratibu au mpangilio maalumu hupati kiribatumbo, vitambi au unyafuzi??
 
Janabi anazungumza kulingana na uzoefu WA wagonjwa anaowatibu.

Overweight na obese based disease ni vitu serious.

Vyakula tunavyokula ni salama?
Ni natural?

Au mbegu za maabara zenye side effects tele.

Mbolea je ni natural?

Hakuna side effects za madawa?

Unasemaje ukisikia njaa Tu ule kumbe tunakula vyakula vyenye sumu nyingi?
Vyakula natural vinakuaje?
Mbolea natural zinakuaje?
Kuna kitu ambacho hakina side effects??
 
Back
Top Bottom