Dodoma: Wanafunzi 17 wadaiwa kutimuliwa baada ya kugomea somo lililofutwa na Serikali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1695734662906.png

Wanafunzi 17 wanaodaiwa kusoma kozi ya Afya ya Jamii (Community Health) katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (Decca) ambayo ilifutwa tangu mwaka 2019 wameiomba Serikali kuwapatia sehemu ya kuishi wakati wakisubiri hatima yao baada ya kufukuzwa na uongozi wa chuo hicho.

Wanafunzi hao wamedai kufukuzwa na chuo hicho juzi baada kugomea mtihani wa mwisho wa kozi hiyo ambayo wameeleza hautawasaidia kupata ajira kwani hawatambuliki kwa sababu hawajasajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).

Mpaka sasa wanafunzi 7 wametumiwa nauli na familia na kurudi nyumbani huku 10 wakiwa wamehifadhiwa na jamaa zao sehemu mbalimbali.

Mmoja wa wanafunzi hao Buhuli Nassoro amesema baada ya kufika muhula wa tatu walianza kuulizia namba zao za usajili wa Nacte lakini walizungushwa kwa kuambiwa hata namba za usajili wa kozi nyingine hutolewa karibu na kipindi cha mitihani ya kuhitimu.

“Kila siku tukiulizia wanasema muda bado na baada ya hapo wakaghairisha na kusogeza mbele wakidai kuna maandalizi mengine lakini tulimfuata Mkuu wa Chuo ambaye alisema hana majibu ya kutupa hivyo tumsubiri msemaji mkuu wa Chuo ambaye alikuwa Dar es Salaam,”amesema Nassoro.

Hata hivyo Nassoro amesema baada ya kutoridhika na majibu hayo waliamua kwenda Ofisi za Wizara ya Afya ambapo waliambiwa kozi hiyo imefutwa tangu mwaka 2019.

Grace Massawe amesema Septemba 21 walifukuzwa chuoni hapo na kusababisha kulala nje kutokana na wengi kutokea nje ya Mkoa wa Dodoma.

“Kwakweli imeniuma kwasababu nimetoka Zanzibar mpaka hapa nikijua nakuja kusoma ili nipate cheti changu na niendelee na Diploma lakini mwisho wa siku ndo imekuwa kama hivi na gharama nyingi tumetumia ikiwemo ada zaidi ya 3 milioni,”amesema Grace.

Akiongea huku akiangua kilio Nyamati Namamba amesema walimuuliza Mkurugenzi kuhusu kusajiliwa Nacte na mara kwa mara alikuwa akiwaahidi kuwa watasajiliwa katika mtihani wa mwisho lakini haikuwa kama ilivyotarajiwa na sasa wamekata tamaa kuhusu kesho yao.

Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu sakata hilo, Mkurugenzi wa Chuo hicho Kamuli Gombo amesema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo mpaka mamlaka husika itakapotoa uamuzi wa yeye au wanafunzi hao ndiyo wamekiuka utaratibu.

Hata hivyo, Gombo amekiri kuwafukuza chuoni wanafunzi hao kwa madai ya kukosa nidhamu kwa kuvuka mipaka na kufanya maandamano haramu kinyume na miiko ya chuo hicho.

MWANANCHI
 
Serikali ilikuwa wapi hadi hao matapeli wanasajili wanafunzi
Wasimamizi wa vyuo hivi waliopewa dhamana na serikali ukiwaona wanaendesha Benz na Range usishangae maana pesa wanazopata ni zao la ukiukwaji wa taratibu huko vyuoni.
Kuna vyuo wanaongoza kwa kutoa mlungura na wanafanya mambo ya kihuni sana
 
Aisee tunamajanga
 
Waziri wa Elimu tunakuomba uingilie hili jambo haraka ili kuondoa huu uhuni unaofanywa na wamiliki wa vyuo vilivyojaa mitaani kama utiriri kuvuna mamilioni ya pesa za wanafunzi wanazolipa kama ada kwa kozi zisizotambulikana na mamlaka husika.
 
View attachment 2763053
Wanafunzi 17 wanaodaiwa kusoma kozi ya Afya ya Jamii (Community Health) katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (Decca) ambayo ilifutwa tangu mwaka 2019 wameiomba Serikali kuwapatia sehemu ya kuishi wakati wakisubiri hatima yao baada ya kufukuzwa na uongozi wa chuo hicho.

Wanafunzi hao wamedai kufukuzwa na chuo hicho juzi baada kugomea mtihani wa mwisho wa kozi hiyo ambayo wameeleza hautawasaidia kupata ajira kwani hawatambuliki kwa sababu hawajasajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).

Mpaka sasa wanafunzi 7 wametumiwa nauli na familia na kurudi nyumbani huku 10 wakiwa wamehifadhiwa na jamaa zao sehemu mbalimbali.

Mmoja wa wanafunzi hao Buhuli Nassoro amesema baada ya kufika muhula wa tatu walianza kuulizia namba zao za usajili wa Nacte lakini walizungushwa kwa kuambiwa hata namba za usajili wa kozi nyingine hutolewa karibu na kipindi cha mitihani ya kuhitimu.

“Kila siku tukiulizia wanasema muda bado na baada ya hapo wakaghairisha na kusogeza mbele wakidai kuna maandalizi mengine lakini tulimfuata Mkuu wa Chuo ambaye alisema hana majibu ya kutupa hivyo tumsubiri msemaji mkuu wa Chuo ambaye alikuwa Dar es Salaam,”amesema Nassoro.

Hata hivyo Nassoro amesema baada ya kutoridhika na majibu hayo waliamua kwenda Ofisi za Wizara ya Afya ambapo waliambiwa kozi hiyo imefutwa tangu mwaka 2019.

Grace Massawe amesema Septemba 21 walifukuzwa chuoni hapo na kusababisha kulala nje kutokana na wengi kutokea nje ya Mkoa wa Dodoma.

“Kwakweli imeniuma kwasababu nimetoka Zanzibar mpaka hapa nikijua nakuja kusoma ili nipate cheti changu na niendelee na Diploma lakini mwisho wa siku ndo imekuwa kama hivi na gharama nyingi tumetumia ikiwemo ada zaidi ya 3 milioni,”amesema Grace.

Akiongea huku akiangua kilio Nyamati Namamba amesema walimuuliza Mkurugenzi kuhusu kusajiliwa Nacte na mara kwa mara alikuwa akiwaahidi kuwa watasajiliwa katika mtihani wa mwisho lakini haikuwa kama ilivyotarajiwa na sasa wamekata tamaa kuhusu kesho yao.

Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu sakata hilo, Mkurugenzi wa Chuo hicho Kamuli Gombo amesema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo mpaka mamlaka husika itakapotoa uamuzi wa yeye au wanafunzi hao ndiyo wamekiuka utaratibu.

Hata hivyo, Gombo amekiri kuwafukuza chuoni wanafunzi hao kwa madai ya kukosa nidhamu kwa kuvuka mipaka na kufanya maandamano haramu kinyume na miiko ya chuo hicho.

MWANANCHI
WAENDE MAHAKAMANI WATAPATA HAKI YAO. WASICHELEWA ASIJE KUWA AFFECTED NA TIME LIMITATION TO INSTITUTE A CASE
Writ of Habeas Corpus:.

Writ of Mandamus:

Writ of Prohibition:

CHAGUA IPI ITAWAFAA
 
Back
Top Bottom