Dodoma: Tundu Lissu afuata gari lake lililoshambuliwa ofisini kwa RPC Muroto. Ashangaa hadi sasa hajahojiwa yeye na Dereva wake

thetallest, Sasa hapo kuna kiki gan mkuu? Yeye kaenda polisi ili wamuhoji ambapo polisi walisema hatoi ushirikiano yeye kaleta ushirikiano wewe unasema anataka kiki

Ulipaswa kumpongeza mkuu kwa ushirikiano wake wa polisi maana wale polisi iliyowaita wasiojulikana sasa inabidi wajulikane maana ushirikiano kwa pande zote mbili sasa unapatikana
Hii ni aibu kubwa kwa Jeshi la Polisi. Tukio la jinai kama hilo Leo miaka mitatu wako ofisini wanasubiri mtu kwenda kutoa maelezo? Duh!
 
..afande Sirro alisema wapelelezi wake wanamtafuta TL lakini hawajampata.

..sasa leo TL kaenda mpaka kituoni kilichowashinda kumkamata na kumhoji ni nini?
kumkamata na kumhoji 😲😲😲mbona me bado sielewi
Yy ndio victim akamatwe tena akili tuuuu😂😂😂😂
 
Hakuna kitu kina umiza kama unapofanya kitu watu wakufanyie kitu ili upate pakusemea then unakuta watu wamechuna.
1. Mapokezi Dar....... Police wala hawakumsumbua
2. Korona Tanzania..... Wala hakuna alie mjibu.
3. Kaanza kampeni mapema....... Watu kimyaaaaa
4. Kwenda police......... RPC angemkaribisha kabisa supu na chapati.

This time kiki zote zitakwama.....
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, leo ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Mh. Lissu la tarehe 7 September 2017.

Mh. Lissu aliambatana na mgombea mwenza wake Mh. Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.

Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Mh. Lissu alisema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.

Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Mh. Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.

Aidha, SACP Muroto alimweleza Mh Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.

Mh. Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.

Mh. Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Mh. Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.

Imetolewa leo Alhamis, Agosti 27, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Hilo gari linapaswa kuwekwa kwenye makumbusho (museum) kwa ajili ya historia ya vizazi vijanvyo.
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana
Unajua hapa unathibitisha tu kwamba uko tupu. Kinachofanywa na Lissu kinalivua nguo jeshi la polisi. Kwanza, ni aibu kwamba leo miaka mitatu tangu Lissu ashambuliwe polisi hawana statement yake ni aibu.

Polisi hawezi kuwa na utetezi wowote kwa sababu wao wenyewe ndio wenye wajibu wa kuwa walalamikaji kwenye suala hili la Lissu. Sasa kama hawana maelezo maana yake tangu jaribio lile la mauaji lishindwe hawajafanya jambo lolote!
 
Nashangaa hawajamkamata!! Mbona wanakuwa wema sana kwa Lissu tangu arudi.
kuna kitu ana kitafuta kumuongezea umaalufu anataka akikamatwa a trend kuongeza mob kitu ambacho kilisha onekana na kina puuzwa😂
 
Hakuna kitu kina umiza kama unapofanya kitu watu wakufanyie kitu ili upate pakusemea then unakuta watu wamechuna.
1. Mapokezi Dar....... Police wala hawakumsumbua
2. Korona Tanzania..... Wala hakuna alie mjibu.
3. Kaanza kampeni mapema....... Watu kimyaaaaa
4. Kwenda police......... RPC angemkaribisha kabisa supu na chapati.

This time kiki zote zitakwama.....
Wewe ulitaka akae kimya baada ya unyama na jaribio la mauaji?! Wewe utakuwa mtu katili sana hata kwa familia yako ndio washenzi wengi wa chama cha kijani walivyo.
 
kumkamata na kumhoji 😲😲😲mbona me bado sielewi
Yy ndio victim akamatwe tena akili tuuuu😂😂😂😂

..nimemsikiliza IGP ktk kipindi cha dakika 45 cha ITV.

..hiyo ndiyo picha ambayo IGP anataka iaminike huku mitaani.

..na anafanya hivyo akitegemea kuwa waTz wengi hawana mazoea ya kuhoji kauli za wakubwa wa serikali.

..na mbinu ya IGP kupoteza muda na kupotosha wananchi ktk suala hili.
 
thetallest, Sasa hapo kuna kiki gan mkuu? Yeye kaenda polisi ili wamuhoji ambapo polisi walisema hatoi ushirikiano yeye kaleta ushirikiano wewe unasema anataka kiki

Ulipaswa kumpongeza mkuu kwa ushirikiano wake wa polisi maana wale polisi iliyowaita wasiojulikana sasa inabidi wajulikane maana ushirikiano kwa pande zote mbili sasa unapatikana
Ni uhuru wa maoni huo mkuu wacha tu huyo aongee ugirigiri wake kadri wanavyoona inafaa
 
Bora Lissu ameenda polisi, hapo karudisha mpira kwa polisi na atatoa maelezo kwa muda sahihi kwake, polisi wasiendelee kusema Lissu anawakwepa kutoa maelezo, na baada ya hayo maelezo ya Lissu polisi itabidi waueleze umma wa watanzania uchunguzi wa shambulio dhidi ya Lissu umefikia wapi.
Amefuata gariiii, kwani ameeenda kuripoti tatizo lake la kushambuliwa??
Yeye ndo alitakiwa aulizie kwani gari lake liko vile? Au alipaswakuulizia kuhusu upelelezi wa kushambuliwa kwake kumeishia wapi.
 
Hahahah huyu mgonjwa amekuwa kitukp kweli sasa kajipeleka ana shangaa hawajamuhoji wakati hakuwepo na alisha sema kuwa wao ndio walimshambulia sasa sijui anataka wamuhoji nini wakati majibu anayo mkononi hahahaha mgonjwa bwana

Kwani umesahau kwamba polisi walisema hawawezi kufanya upelelezi hadi wamuhoji yeye na dereva sasa wameenda kuwambia wapo tayari kuhojiwa na tayari alishasema mtshukiwa wa kutaka yeye apigwe risasi ni nani kazi kwao sasa
 
Ati anashangaaa!!!.. kibaraka akumbuke ana kesi.. huyu ni hatari sana.. hata mwili wake.. hakukumbuka ya gari.. hadi kamaliza kukamilisha ubaraka wake aliotumwa na mabeberu.. hafai kuwa kiongozi wa nchi hii hata kwa sekunde moja.. tukisema ilikuwa mipango yao wenyewe.. bado munapiga kelele. Ati nini!!!😅😅😅😅😅

Magufuli 2020 💯
Pumba kbsa
 
Back
Top Bottom