Tundu Lissu aoneshwa gari lake lililomiminiwa risasi, ahesabu matundu ya risasi ashangaa aliponaje

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,741
218,330
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, Jeshi la Polisi Dodoma leo hatimaye limemuonyesha Tundu Lissu gari lake lile lililotunguliwa na risasi zisizo na idadi kwa lengo la kumuua.

Tundu Lissu akiwa mbele ya polisi , amehesabu upya matundu ya risasi alizomiminiwa na watu waliotumwa kumuua ambapo hesabu hiyo imefikia zaidi ya 30!

Akiwahutubia polisi hao kwenye kituo chao , ameonyesha kushangaa kwamba ilikuwaje pamoja na lundo hilo la risasi hizo akatoka akiwa anapumua, amewaambiwa polisi hao kwamba siku chache zijazo atakuja kulichukua gari lake.

Tunatoa shukrani kwa jeshi la Polisi kwa kumuonyesha Lissu Gari lake, japo ni kwa kuchelewa.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa , Jeshi la Polisi Dodoma leo hatimaye limemuonyesha Tundu Lissu gari lake lile lililotunguliwa na risasi zisizo na idadi kwa lengo la kumuua .

Tundu Lissu akiwa mbele ya polisi , amehesabu upya matundu ya risasi alizomiminiwa na watu waliotumwa kumuua ambapo hesabu hiyo imefikia zaidi ya 30 !

Akiwahutubia polisi hao kwenye kituo chao , ameonyesha kushangaa kwamba ilikuwaje pamoja na lundo hilo la risasi hizo akatoka akiwa anapumua , amewaambiwa polisi hao kwamba siku chache zijazo atakuja kulichukua gari lake .

Tunatoa shukrani kwa jeshi la Polisi kwa kumuonyesha Lissu Gari lake , japo ni kwa kuchelewa .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
safi sana na asije akarudia Tena kuleta ujuaji kwenye mambo ya watu
 
Leo ndio ameliona ,zile picha mlizokuwa mahesabu eti risasi 18 mara 36 mara 40 ulikuwa mnazitoa wapi na je Lisu hakuziona ?

USSR
 
Inasemekana wafyatuaji risasi wote walishauwawa. Angalia iyo picha chini jinsi walivyochanganyikiwa na kuanza kuigiza. Ningependa kujua ni nani aliyetoa ilo wazo waigize kijinga hivyo. Watu wazima wanafanya Mambo ya ajab, aibu na kukera. Hata hivyo ilikuwamepanic.View attachment 2615673View attachment 2615669

View attachment 2615669
Nimeona jezi zimeandikwa Lugalo
Kwani Lissu alipelekwa Lugalo baada ya tukio Dodoma?
Ni kama siku ile kamanda Mkuu wa mambo yote alikuwa Dar sasa hapa alikwendaje kumwona mgonjwa?
 
Hakustahili kuumizwa kiasi kile muda mwingine tuangalie familia yake watoto wake wanaumia kiasi gani wakijua baba yao kaumizwa kwaajili ya mambo ambayo hata wangekaa kimya yasingewadhuru. Mm ndio maana namkubali sana kikwete hakua na hayo mambo ya visasi japo nae alikua na njia zake ila sio kama za jpm alifanya kitu kibaya sana
 
Nimeona jezi zimeandikwa Lugalo
Kwani Lissu alipelekwa Lugalo baada ya tukio Dodoma?
Ni kama siku ile kamanda Mkuu wa mambo yote alikuwa Dar sasa hapa alikwendaje kumwona mgonjwa?
Mkuu baada ya lissu kupigwa risasi na kupona. Wakastage ilo tukio kwenye hizo picha. Eti watu wajue kulikuwa na kikundi cha maharamia wanafyatulia watu risas. Yani move ya kisengee
 
Inasemekana wafyatuaji risasi wote walishauwawa. Angalia iyo picha chini jinsi walivyochanganyikiwa na kuanza kuigiza. Ningependa kujua ni nani aliyetoa ilo wazo waigize kijinga hivyo. Watu wazima wanafanya Mambo ya ajab, aibu na kukera. Hata hivyo ilikuwamepanic.View attachment 2615673View attachment 2615669

View attachment 2615669
Acha upotoshaji. Magu hakwenda kumuona Lissu pia Lissu hakupelekwa DAR. Aliondokea Dodoma kuelekea Nairobi. Anyway, kama wauaji na wao waliuwawa ni habari njema.
 
Anapokuwa hataki maridhiano alitaka hayo yaliyompata yawe yanaendelea au anamaanisha nini?
 
Back
Top Bottom