BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, leo ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Mh. Lissu la tarehe 7 September 2017.
Mh. Lissu aliambatana na mgombea mwenza wake Mh. Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.
Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Mh. Lissu alisema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.
Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Mh. Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.
Aidha, SACP Muroto alimweleza Mh Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.
Mh. Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.
Mh. Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Mh. Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.
Imetolewa leo Alhamis, Agosti 27, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano