Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,810
- 11,980
Wabunge wawili wa Chadema, David Silende (Momba) na Peter Lijualikali (Kilombero) wamehudhuria bungeni leo licha ya chama chao kuwataka wabunge wake kutohudhuria vikao vya Bunge ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona
Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali,
Hivi karibuni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema kutokana na hali ya Corona kuwa mbaya, Kwamba wabunge wa Chadema walikubaliana kutohudhuria Bungeni na wamekubaiana kujeweka Karantini.
"Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia Bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma, niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa." alisema Bulaya.
Mbunge wa Momba kwa tiketi ya CHADEMA , Silinde Ernest David
Pia soma: Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2 - JamiiForums
Kufuatia wabunge wa CHADEMA kwenda Karantini, Spika Ndugai amshukia Mbowe kama mwewe - JamiiForums