Dodoma: Mapokezi ya Alhad Musa Salum yazua Taharuki, Waislam Wamwandikia barua Mufti

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,487
2,739
Barua ya Wazi

Assalaam Alaykum,

Sheikh Mkuu, Mufti wetu wa Tanzania, nimeguswa kukuandikia barua hii ya wazi ama kwa kuhoji na kutaka ufafanuzi, ama kwa kushangazwa na nilichokiona.

Kama nilivyoshangazwa, nimefuatilia kwa ndugu zetu wengi katika imani, ama kwa hakika, tukio ninalolileta kwako limejenga taharuki kubwa kwetu waumini.

Nimeona video mtandaoni ikimwonesha aliyekuwa Sheikh wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akipata mapokezi ya ving'ora vya polisi na msafara wenye magari na pikipiki, mkoani Dodoma. Na kulakiwa na waumini kama Sheikh mwenye darja.

Sheikh wetu, tukio hilo limetengeneza mshangao mkubwa. Hayajapita majuma mawili tangu ulipomwondoa Alhad Mussa kuwa Sheikh wa Dar es Salaam. Inastaajabisha anatokeza na mapokezi makubwa.

Waislam wana maswali matano. Alhad Mussa anafikisha ujumbe gani? Anataka kumaanisha yeye ni mkubwa kuliko mamlaka ya Mufti aliyemtengua? Msafara wenye ving'ora na pikipiki iliyomsafishia njia, amepewa kama nani, ikiwa yeye kwa sasa ni maamuma? Polisi ni serikali, kwa mapokezi hayo, serikali inamuunga mkono Alhad Mussa dhidi ya Mufti? Waislam waliompokea na kumkirimu Alhad Mussa mithili ya kiongozi wa darja kubwa lengo lao ni nini?

Kwa maswali hayo, Sheikh wetu, Mufti Abubakar Zuberi, huna budi kutoka na kuzungumza na umma wa Waislam na hata wasio Waislam, ujibu maswali hayo ili Watanzania na mamlaka zake zitambue haki anazostahili Alhad Mussa na ambazo hastahili.

Hitimisho la kila mjadala ni kuwa kitendo cha Alhad Mussa kutengeneza mapokezi yale ni utovu mkubwa nidhamu kwa mamlaka ya Mufti. Amelikosea heshima Baraza la Ulamaa la Bakwata na uongozi wote wa juu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata).

Nakuangukia. Shime Sheikh, toka uongee na umma. Tujue nafasi ya Alhad Mussa. Alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani. Nafasi hiyo aliipata sababu alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sasa si Sheikh tena. Kwa nini ving’ora vya polisi na kumbatio la waumini tena msikitini?

Wabillahy Ttawafiq,

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakutu


MAULIDI KITENGE.jpg
 
Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Salum, ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki.

Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini.

Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito, yanasema hivi, KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe?
 
Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam , Musa Salum , ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki .

Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini .

Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito , yanasema hivi , KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU ? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe ?
Kwani nje ya cheo alichokua nacho hana hadhi yake binafsi ? Amepokelewa kama Musa Salum hajapokelewa kama Sheikh wa mkoa hizi complications nyingine hazina umuhimu sana. Mtu amekabidhi ofisi mnataka aishi kinyonge ?
 
Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam , Musa Salum , ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki .

Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini .

Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito , yanasema hivi , KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU ? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe ?
Wewe kibibi acha wivu hata wewe unaweza kuomba escort ya pikipiki za Polisi kwa malipo! Kwani huwa huoni GSM huwa ana escort ya Pikipiki za Polisi kila mara!!? Utakufa na wivu wa kike wewe Kibibi.
 
Back
Top Bottom