Dodoma yaporomoka kimapato, yawa ya mwisho

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,636
6,261
Halmashauri ya jiji la Dodoma mwaka Jana robo kama hii ilikuwa ya kwanza Kwa ukusanyaji Kati ya majiji yote, mwaka huu yawa ya mwisho. Na kimkoa yawa ya pili toka chini, kulikoni?

Nini kimeshusha mapato kiasi hicho? Je wawekezaji wameondoka?

Hata viwanja bei imeshuka kulikoni?

Msigwa Kesho alitolee ufafanuzi.
 
Ukimsikiliza anavyoongea huku akijifanya mtu makini na asiyependa mawaaa hakika utadhani huyu sasa ndiye kiongozi kumbe wapi?!

Jiji la Dodoma limekuwa la mwisho katika ukusanyaji maduhuli hali iliyoshtua mno kwa sababu kwa takribani miaka miwili Jiji lile limekuwa kinara wa kukusanya mapato katika wadaa wa Majiji.

Vilevile Jiji lile limeshika nafasi ya pili kutoka mwisho katika wadaa wa kimkoa.

Hii ni aibu kubwa mno kwa Antony!
 
Halmashauri ya jiji la Dodoma mwaka Jana robo kama hii ilikua ya kwanza Kwa ukusanyaji Kati ya majiji yote,mwaka huu yawa ya mwisho. na kimkoa yawa ya pili toka chini, kulikoni? Nini kimeshusha mapato kiasi hicho? He wawekezaji wameondoka? Hata viwanja bei imeshuka kulikoni? Msigwa Kesho alitolee ufafanuzi.
Wewe uliamini Propaganda za Mwendazake kuwa Dodoma ilikuwa ya kwanza? Shituka Jiwe alikuwa Molongo sana.
 
Dodoma haijawahi kuongoza kimapato ya nchi, Serikali ya awamu ya tano ilikuwa ikidanganya umma ili kuvutia wawekezaji waende kuwekeza Dodoma baada ya serikali kuhamia kule. Na ni kweli hivi sasa inazidi kuporomoka, baada ya Uongozi wa Mama Samia kuonyesha dhahiri, Macho na akili zao ni Dar.
 
Ukishauza viwanja prime areas, unabaki kusubiri pajenge utoze kodi ya majengo. Then pahamiwe na watu uanze kutoza kodi za mapato.
Hii itachukua 10 to 20 years.
Zile data za mapato mwaka jana, siyo mapato endelevu, ni kama msingi tu.
Na kama watu watahodhi hizo ardhi, basi labda miaka 30 ijayo.
 
Dodoma haijawahi kuongoza kimapato ya nchi, Serikali ya awamu ya tano ilikuwa ikidanganya umma ili kuvutia wawekezaji waende kuwekeza Dodoma baada ya serikali kuhamia kule. Na ni kweli hivi sasa inazidi kuporomoka, baada ya Uongozi wa Mama Samia kuonyesha dhahiri, Macho na akili zao ni Dar.
Na sasa unaambiwa hata thamani ya ardhi kwa Dodoma imeshuka sana!!!
 
Ukimsikiliza anavyoongea huku akijifanya mtu makini na asiyependa mawaaa hakika utadhani huyu sasa ndiye kiongozi kumbe wapi?!

Jiji la Dodoma limekuwa la mwisho katika ukusanyaji maduhuli hali iliyoshtua mno kwa sababu kwa takribani miaka miwili Jiji lile limekuwa kinara wa kukusanya mapato katika wadaa wa Majiji.

Vilevile Jiji lile limeshika nafasi ya pili kutoka mwisho katika wadaa wa kimkoa.

Hii ni aibu kubwa mno kwa Antony!
RC ni wa mkoa mzima na siyo mkurugenzi wa Dodoma jijiji
 
Baada ya Kushangilia ukusanyaji ni vema tukachunguza zaidi kazi zinafanywa na haup mapato
 
Dodoma pale ukiondoa Bunge na UDOM hamna kitu, mji vumbi tupu, hali ya hewa hovyo, maji chumvi, ukichimba shimo la choo mita tano unakutana na mkondo wa maji...ni matatizo matupu.

Binafsi siwezi kuwekeza Dodoma.
 
Ukimsikiliza anavyoongea huku akijifanya mtu makini na asiyependa mawaaa hakika utadhani huyu sasa ndiye kiongozi kumbe wapi?!

Jiji la Dodoma limekuwa la mwisho katika ukusanyaji maduhuli hali iliyoshtua mno kwa sababu kwa takribani miaka miwili Jiji lile limekuwa kinara wa kukusanya mapato katika wadaa wa Majiji.

Vilevile Jiji lile limeshika nafasi ya pili kutoka mwisho katika wadaa wa kimkoa.

Hii ni aibu kubwa mno kwa Antony!
Mtaka ni RC wa Mkoa sio mkurugenzi wa Jiji ,acha kukurupuka.

Harafu hiyo ni miezi 3 tuu ya kwanza kuna miezi 9 inakuja.

La mwisho kwa asilimia ila sio kwa Pato ghafi yaani physical money.

Dume jike wivu utakumaliza
 
Dodoma pale ukiondoa Bunge na UDOM hamna kitu, mji vumbi tupu, hali ya hewa hovyo, maji chumvi, ukichimba shimo la choo mita tano unakutana na mkondo wa maji...ni matatizo matupu.

Binafsi siwezi kuwekeza Dodoma, never ever.
Kumbe kuna maji,sasa kolasi ya jangwa nayo bado unaiimba?
 
Sababu kubwa ya Jiji la Dodoma kuwa na mapato makubwa miaka niwili iliyopita ilikuwa ni uuzaji wa viwanja uliofanywa na jiji baada ya kuinvest kwenye upimaji wa viwanja vingi kipindi cha vuguvugu la kuhamia Dodoma, Kwa sasa viwanja vingi vimekwisha/asilimia kubwa vimeshalipiwa! Wamerudi kwenye vyanzo vya mapato vya siku zote ambapo kwa hilo jiji la Dodoma bado hawawezi kucompete na majiji ya DSM, ARSH, MWZ, na MBEYA!! Kifupi Dodoma iliharakisha tu kuwa jiji na mikurupuko ya kipenzi chako ila bado haistahili!! Acha kuwachukia binadamu wenzako na kuwawazia mabaya muda wote
 
Back
Top Bottom