Dodoma: Askari Polisi auliwa na raia

Dodoma: Askari Polisi auliwa na raia

R.I.P askari wetu ila mtuhumiwa asakwe na akikamatwa auwawe na yeye.
 
Hii nchi ina matatizo mengi sana, ila kama IGP unasoma hii chukua hatua, sifuraishwi na nilichokisoma hapa hata kidogo. Haiwezkani Polisi ameuawa halafu watu wanashangilia hata kama ni asilimia ndogo, hii inaonyesha kuwa kuna tatizo kwenye jamii yetu na linatakiwa kupatiwa ufumbuzi sasa hivi, IGP tusaidie kutenganisha jeshi lako na siasa, fanyeni kazi kitaalamu zaidi kuliko kutumika zaidi, wananchi walitakiwa kumsaidia polisi na sio kukimbia baada ya polisi kuuawa.

Kwa wataalamu wa saikolojia, huyu jamaa definitely alikuwa kichaa, kwanini alitaka kumuua mtoto wake mdogo? Jamii ilimsaidia namna gani? Kwanini polisi alienda na watu wawili kwenye mji kama dodoma wenye watu wengi? Kwanini polisi alipigiwa simu kama yeye binafsi bila kumshirikisha mkuu wa kituo? Mtendaji Kata alishindwa hata kuchukua majirani waliompigia simu wakaenda nao? Kwanini walimuacha akimbie baada ya kumuua polisi?

Kuna maswali mengi zaidi ya majibu, polisi ndio maana wanatembea wawili wawili ilikuwaje akaaenda peke yake? Mtendaji kwanini hakupiga simu polisi badala yake akampigia mwenyewe binafsi? Tuache kufanya kazi kwa mazoea tuwe tunafuata safety measures tulizowekewa, taratibu zilizoainishwa zifuatwe maana hata kama ni emergence huwezi kujua tatizo unaloenda kutatua litaspill kiasi gani!

Watu walisema hii nchi watu wote ni vichaa, lakini wengine wakaja na kubisha kuwa hakuna vichaa, hii nchi watu wako frastrated sana kiasi cha kupoteza conscious mind

Nimependa post yako,,,,!!
Na kwa tukio la jana hayo maswali yako yanatoa mwanga mzuri.

Askari alikua ni msimamizi wa polisi jamii na mara nyingi alikua anaacha namba yake ya simu karibu kila ofisi ya mtaa.

Hivyo baada ya kupokea taarifa juu ya tukio hilo Mtendaji wa Mtaa aliona ni rahisi zaidi kumpigia simu huyu askari kuliko kupiga simu Central Polisi maana huwa wanachelewa sana kufika eneo la tukio na kwakua Askari aliyeuawa alikua anatumia piki piki ya polisi akaona ni rahisi sana Kamanda Jose kufika eneo la tukio.

Binafsi nimeumia sana maana huyu askark alikua ni rafiki yangu sana,,,,,!!!
 
Tunaomba utueleze vizuri, mtuhumiwa wa kitu gani na alikuwa na uhusiano gnai na wananchi na nini kilichotokea hadi wananchi wakaanza kumfanya hivyo?

Ni jambo la huzuni sana. Ccm inatupeleka kubaya sana. Wananchi wanakuwa na uchungu na serikali kiasi cha kuwa na uadui n achuki kubwa namna hii? Nani aliwaamrisha wampige yule askari? Aliwakosea nini? Jamani ccm acheni upumbavu. Mnaua Tanzania Yetu.

binafsi imenisikitisha ... Pumzika kwa amani soja
 
Kwanini aende kukamata mtuhumiwa peke yake? Harufu ya rushwa kama si maslahi binafsi au kutaka sifa mbele ya bosi. Haiingii akilini, kwa nn aendepeke yake? Na je alikuwa kazini?
Please dont be judgemental. collect your facts first before implying that corruption and personal gain was the motive that this poor askari responded fast on the request from the local govt leader.
 
Hata mimi nimeipenda hiyo. Sasa hivi ni hivyo tu. Kwanza sasa hivi vijana ni kujipanga kuwasaka askari wanaokaa mitaani. Make wao wamegeuka wafuasi wa kutumikia mafisadi na kutuona raia kama siyo watu.

Sera ya CUF ndo inayopaswa kutumika. (Jino kwa Jino) Kova anapotoa Mafisadi wanapotoa amri ya kupiga raia basi nasi tujiandae kujibu. Jino kwa jino ndo litatuokoa raia



!
!
hawa ni kuwasaka mmoja mmoja kitaani kisha tunazaa nao. Raia tuko wengi kuliko wao, tukiamua kuwashikisha adabu watashika tu. Wanalala katika nyumba zetu, wanakunywa katika baa zetu, mademu zao tuko nao kitaa yaani yuna kila nafasi ya kuwafanyia kitu mbaya.
 
Ni mtaa wa kituo cha daladala Kiitwacho Maabara, Chang'ombe Dodoma siku ya jana tar 04 Wednesday 2015 mida ya saa tano asubuhi. Nikiwa maeneo hayo chanzo chake ni kwamba; kijana mmoja ambae ameoa na ana mtoto mchanga, mtoto wake mwenye umri usiofikia mwaka mmoja, kijana huyu alitaka kumpiga mtoto wake ambae ana umri wa chini mwaka mmoja, huyu kijana alikuwa akimning'iniza mtoto kichwa chini miguu juu, mama wa huyo mtoto ambaye ndiye mke wa huyo jamaa akaamua kupiga simu polisi ili aombe msaada maana huyo mume wake anamuogopa sana. Yule kijana kabla polisi hawajaja aliamua kuingia ndani ya chumba chao na kujifungia akiwa na mtoto huyo, lengo la kufanya hivyo halijulikani kama alitaka kumuua mtoto au lah, polisi wawili wakafika hapo nyumba, polisi mmoja alikuwa ameshika bunduki na mwingine alikuwa hana ndipo wakaambiwa kuwa yule kijana yupo ndani amejifungia na mtoto, ktk kuanza kufungua mlango wakagundua kuwa mlango umefungwa kwa ndani, basi yule mke wa huyo jamaa akawaruhusu wavunje mlango ili waingie wamtoe mtoto, askari ambae alikuwa hana silaha (bunduki) akakanyaga mlango na hatimae mlango ukafunguka, ulipofunguka tu yule askari ambae hana silaha akaingia ndani kabla ya kumaliza kuingia jamaa akampa panga la uso, yule askari akaanguka chini alipoanguka yule jamaa akaendelea kumkata na hatimae akamkata mpaka kwenye koromeo mpaka mauti ikamkuta. Yule jamaa akatoka na panga nje tena panga likiwa linadamu za binadam, yule jamaa akakimbia. Haya yote yanafanyika yule askari ambae alibaki nje ndiye aliyekuwa ana siraha na hakuweza kufanya chochote mpaka mtuhumiwa alipokimbia. Nasikia yule jamaa amekamatwa, wale wanaosema uchunguzi unaendelea Mungu awasaidie sana. Mtoto hakufa jamani, samahani kama hamtaelewa
 
Mhhh, shetani kazini. Haya matukio yanatisha...si wanasiasa, si raia wote wameona kumwaga damu ya mwingine ni dili. Hii pia inachangiwa na hizo movie zenu za mauaji mnazoangalia.
 
Mitaa hii ilipotokea tukio jana, upande wa juu yake mitaa ya Njia Panda Ya Nkuhungu kuna dada tangu amelala jana hajaamka mpaka leo, yaani amefariki maiti wameikuta ndani. Kinachoendelea nadhan watu wa upelelezi wamefika tayari, ila hii mitaa sio mizuri kwa maisha ya kuishi watu wanyonge
 
Mitaa hii ilipotokea tukio jana, upande wa juu yake mitaa ya Njia Panda Ya Nkuhungu kuna dada tangu amelala jana hajaamka mpaka leo, yaani amefariki maiti wameikuta ndani. Kinachoendelea nadhan watu wa upelelezi wamefika tayari, ila hii mitaa sio mizuri kwa maisha ya kuishi watu wanyonge

Kuna kituo cha polisi mitaa hiyo???!!
 
Kituo cha polisi hakuna, polisi wenyewe wanaogopa sana hii mitaa maana inasemekana tangu zamani waharifu wa Mkoa wa Dodoma ndiko wanakotokea huku. Ukiwa Dodoma mjini ukiwaambia watu kuwa unatokea Chang'ombe wanakaa mbali na wewe. Yaani polisi wetu wamekuwa wavaaji wa zile uniform tu basi, kazi yao haionekani kabisa siku hizi
 
Kituo cha polisi hakuna, polisi wenyewe wanaogopa sana hii mitaa maana inasemekana tangu zamani waharifu wa Mkoa wa Dodoma ndiko wanakotokea huku. Ukiwa Dodoma mjini ukiwaambia watu kuwa unatokea Chang'ombe wanakaa mbali na wewe. Yaani polisi wetu wamekuwa wavaaji wa zile uniform tu basi, kazi yao haionekani kabisa siku hizi

Inasikitisha kama hali iko hivyo, ila hili la polisi kuogopa huo mtaa (kama kweli) mbona kama ni habari ya kufedhehesha sana???!!!
 
Huyo askari alikuwa na toy? only in Tanzania
 
!
!
hawa ni kuwasaka mmoja mmoja kitaani kisha tunazaa nao. Raia tuko wengi kuliko wao, tukiamua kuwashikisha adabu watashika tu. Wanalala katika nyumba zetu, wanakunywa katika baa zetu, mademu zao tuko nao kitaa yaani yuna kila nafasi ya kuwafanyia kitu mbaya.

unajielewa usemayo? amani kuvuruga rahisi ila kurudisha si mchezo ndugu.... ebu tafakari tena afu upost ndug yangu..... umenisikitisha sna na kauli yako
 
tatzo raia wanajichukulia sheria mkononi na polisi wanaingilia kaz ya mahakama, kwahyo wote n wakosaj kisheria. tafakarini chukue hatua... hakka hakuna damu itakayomwagika iwe ya raia au polisi ambayo haitalia ardhini.
 
Huyo askari alikuwa na toy? only in Tanzania

humjui huyu askari ndo maana wasema....... kifo haina mwenyewe kinawafika hata makomando wa jeshi tena kizemmbe zembe tu. askari huyu nilikua namjua vzur sana tena alikua shupavu na mpenda haki na usawa. watu wengi walimpenda na walipenda sana mshirikisha mambo ya kijamii. alikia karibu sana na jamii na nishamuona akifanya kazi bila kuchoka. basi tu ni alizawadiwa uhai mfupi maana akuna binadamu kwa nguv zake anaweza jiongezea uhai
 
Marehemu akiwa kafanyiwa unyama huo
 

Attachments

  • 1423123906926.jpg
    1423123906926.jpg
    57.6 KB · Views: 160
  • 1423123926794.jpg
    1423123926794.jpg
    77.7 KB · Views: 151
Kituo cha polisi hakuna, polisi wenyewe wanaogopa sana hii mitaa maana inasemekana tangu zamani waharifu wa Mkoa wa Dodoma ndiko wanakotokea huku. Ukiwa Dodoma mjini ukiwaambia watu kuwa unatokea Chang'ombe wanakaa mbali na wewe. Yaani polisi wetu wamekuwa wavaaji wa zile uniform tu basi, kazi yao haionekani kabisa siku hizi

changombe ni mtaa wa vibaka .. Majambazi wamo bungeni na wanaishi mitaa ya Uzungungi na Area D ...
 
Back
Top Bottom