Tabby
Mimi naomba tutenganisha siasa na mambo mazito kama haya. Mimi naamini kabisa kinachotendeka sasa hivi ni jamabo zito sanaaaaa. Haijatokea hata siku moja wananchi wakamwua askari kikatili hivyo.
Hiyo siyo jadi na mila za Watanzania. Kuna kitu kikubwa sana kipo kinakuja na kitafika. Serikali inatakiwa iwe makini sana na mwendelezo wa vitu vinavyotokea sasa hivi.
Kwa mawazo yangu kinachotokea sasa hivi ni mwendelezo wa mtandao wa kuuawa kwa askari na kupokonya silaha kule Geita(? sikumbuki vizuri ni mwaka jana lilitokea), Tanga, Ikwiriri, na juzi juzi Morogoro. Polisi vilevile wamepigwa mabomu kule Songea mara kadhaa.
Huu ni mwanzo wa ngoma, inakuwa lele baadaye inakomaa. Boko Haram walianza kwa kuwaua Wakristo makanisani sasa wanawaua Waislamu wenzao.
Beware Tanzanians. Beware. Something is coming your way.