Dodoma: Aliyekuwa akisafirisha Mirungi afariki dunia wakati akijaribu kuwakimbia Polisi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mkacha Mohamed (35), mkazi wa Soya wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kuanguka na pikipiki akiwa na mwenzake wakiwakimbia Polisi wa Kibaya waliokuwa kwenye doria kijiji cha Namelock.

Vijana hao walikuwa wanasafirisha shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi bunda 250 sawa na kilo 119.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili Septemba 17, 2023 katika kijiji cha Namelock Kata ya Namelock Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amethibitisha kutokea tukio hilo na kumtaja marehemu huyo kuwa ni Mkacha Mohamed, aliyekuwa amepakia mwenzake aliyejulikana kwa jina la Nasibu Yahaya (23) ambaye yeye amenusurika kifo.

"Marehemu Mkacha Mohamed Mkacha (35) ndiye aliyekuwa dereva wa pikipiki iliyopata ajali hiyo ambayo pia alibeba abiria huyo na shehena ya madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Pikipiki hiyo ilipasua tairi ya mbele wakati wakifukuzana na askari Polisi wa Kibaya ambao waliokuwa kwenye doria baada ya kuhisi kuwa watu hao walikuwa wamebeba magendo na waliposimamishwa na Askari hao hawakusimama ndipo wakaanza kufukuzana kisha pikipiki yao kupasua tairi na kuanguka na kusababisha kifo hicho," amesema ACP Katabazi.

Amesema mwenzake aliyekuwa amepakiwa nyuma, hakuumia na hana hata mchubuko lakini dereva alipoteza maisha hapo hapo na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

"Mwili wa marehemu amehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Kiteto na Nasibu Yahaya Bakari (23) aliyekuwa amebebwa kwenye pikipiki hiyo hakuumia na anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kiteto kwa upelelezi zaidi," amesema.

Aidha Kamanda Katabazi amesema madawa hayo ya kulevya yalikuwa yanasafirishwa kwenda Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma kwa usafiri wa pikipiki aina Sinoray ambayo haikuwa na namba za za usajili.

Imeelezwa kukamatwa kwa watu hao kumetokana na taarifa za kiintelejesia ambapo askari hao walikuwa nazo awali kuwa kuna vijana wanafanya shughuli hiyo na polisi kuweka mtego na kufanikisha wakiwa kwenye doria

ACP Katabazi ametoa wito kwa wananchi haswa vijana kuacha kufanya biashara haramu ambazo zinahatarisha maisha yao na kwamba huenda leo hii kijana huyo angekuwa hai na anaendelea na shughuli za maendeleo ya jamii.

"Hawa walikuwa wanawakimbia askari Polisi wakijua kuwa wanatenda kosa, wangekuwa hawajatenda kosa wasingepatwa na ajali hiyo iliyosababisha kifo," amesema ACP Katabazi.

MWANANCHI
 
Sinaroy inajua kukimbia sema tairi liliwasaliti tu
Hilo tairi nalo,sjui lilikuwa limechoka maana kesi za kupasuka ni nadra sana

Ndo maana nikiwa kwenye pikpik huwa sipend kukimbia sana maana huwa nafikiria zaidi vp kama pikpik ikipata shida hasa ya cheni
 
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Mkacha Mohamed (35), mkazi wa Soya wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kuanguka na pikipiki akiwa na mwenzake wakiwakimbia Polisi wa Kibaya waliokuwa kwenye doria kijiji cha Namelock.

Vijana hao walikuwa wanasafirisha shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi bunda 250 sawa na kilo 119.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili Septemba 17, 2023 katika kijiji cha Namelock Kata ya Namelock Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amethibitisha kutokea tukio hilo na kumtaja marehemu huyo kuwa ni Mkacha Mohamed, aliyekuwa amepakia mwenzake aliyejulikana kwa jina la Nasibu Yahaya (23) ambaye yeye amenusurika kifo.

"Marehemu Mkacha Mohamed Mkacha (35) ndiye aliyekuwa dereva wa pikipiki iliyopata ajali hiyo ambayo pia alibeba abiria huyo na shehena ya madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Pikipiki hiyo ilipasua tairi ya mbele wakati wakifukuzana na askari Polisi wa Kibaya ambao waliokuwa kwenye doria baada ya kuhisi kuwa watu hao walikuwa wamebeba magendo na waliposimamishwa na Askari hao hawakusimama ndipo wakaanza kufukuzana kisha pikipiki yao kupasua tairi na kuanguka na kusababisha kifo hicho," amesema ACP Katabazi.

Amesema mwenzake aliyekuwa amepakiwa nyuma, hakuumia na hana hata mchubuko lakini dereva alipoteza maisha hapo hapo na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

"Mwili wa marehemu amehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Kiteto na Nasibu Yahaya Bakari (23) aliyekuwa amebebwa kwenye pikipiki hiyo hakuumia na anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kiteto kwa upelelezi zaidi," amesema.

Aidha Kamanda Katabazi amesema madawa hayo ya kulevya yalikuwa yanasafirishwa kwenda Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma kwa usafiri wa pikipiki aina Sinoray ambayo haikuwa na namba za za usajili.

Imeelezwa kukamatwa kwa watu hao kumetokana na taarifa za kiintelejesia ambapo askari hao walikuwa nazo awali kuwa kuna vijana wanafanya shughuli hiyo na polisi kuweka mtego na kufanikisha wakiwa kwenye doria

ACP Katabazi ametoa wito kwa wananchi haswa vijana kuacha kufanya biashara haramu ambazo zinahatarisha maisha yao na kwamba huenda leo hii kijana huyo angekuwa hai na anaendelea na shughuli za maendeleo ya jamii.

"Hawa walikuwa wanawakimbia askari Polisi wakijua kuwa wanatenda kosa, wangekuwa hawajatenda kosa wasingepatwa na ajali hiyo iliyosababisha kifo," amesema ACP Katabazi.

MWANANCHI
hili la kufukuzana ta pikipiki wakati wa mzee wa 'watapata tabu sana' RPC MUROTO, polisi walishauriwa kujizuia kufukuza wahalifu wenye bodabada hasa pale wanapojiridhisha juu ya uhalifu wao kupitia taarifa za kiintelijensia walizonazo.
na kwakeli kwa kiasi kikubwa vifo vya aina hii vimepungua kwa kiasi kikibawa wilayani humo.

Jambo hili limepoteza maisha ya vijana wengi mno hususana kwenye wilaya tajwa alikotoka huyo marehemu muhalifu.
anyway kawsababu hao askari ni wa kiteto labda hawakua na utaratibu au angalizo hilo.

R.I.P Kijana.......
 
Ukute askari wala hawakujua mambo ya mirungi ila waliona pikipiki haina plate namba wakataka kuikamata.
 
si taarifa inasema askari walikua na taarifa ya kiintelijensia kuhusu magendo hiyo na waliweka mtego
 
  • Thanks
Reactions: Tsh

Similar Discussions

Back
Top Bottom