DMO Iramba aikashifu serikali ya Magufuli mbele ya Jafo

DMO Iramba aikashifu serikali ya Magufuli mbele ya Jafo

Mkuu,mtoa mada ametumia tafsida!ameandika kinyume!
Mkuu labda kiswahili kinanipiga chenga.

"DMO alijikita zaidi kuonyesha uhaba wa pesa za dawa na motisha kwa watumishi wa afya,pia uhaba wa watumishi."

Hayo maneno ndiyo kashfa nisaidie mkuu?
 
Kwanza tupo busy n wakandarasi n ndege ikifika January 2017 labda tutaangalia pesa kupeleka kwenye Dawa km itakuwa n umuhimu wa izo dawa
 
Mleta mada alijua akiweka heading halisi haitabamba... Kajiongeza kimtindo
 
nakubali watz uwezo wetu was Akili mdogo, kuelewa mambo madogo, mleta Uzi alimaanisha kitendo cha MTU yeyote kueleza mabungufu ya selikali ni kuikashifu, kwani tumeaminishwa hii ni serikali takatifu

Mimi nimemuelewa mleta mada kuwa serikali ya sasa haipend kuelezewa kwa ubaya,inapenda kusifiwa,sasa MDO kusema ule ukweli ni kama uchochez,ukumbuke Ummy Ticha alikanusha kitu kinchofanana na MDO
 
Mahitaji ya dawa na vifaa tiba kwa watanzania kwa siku moja gharama yake ni zaidi ya maradufu ya bei ya hizo ndege. Na ni kwa siku moja tu. Ni karibu na gharama ya kulisha chakula watanzania. Ni kitu ambacho hakiwezekani. Ni jukumu la kila mwananchi kujinunulia mwenyewe huduma hizo badala ya kutegemea kuletewa na serikali. Maduka binafsi ya dawa hayajawahi kuishiwa dawa. Sasa kelele za nini?

Unataka kusema kuwa nikienda hospital niende na CT SCAN YANGU,kitanda changu,xray yangu,
 
Kwamba bajet imepitishwa July had sept hela hazijaenda.Na makusanyo yanatajwa kuwa yanaongezeka kila mwezi,
 
Dawa za nini. Kachimbeni mizizi mnywe mbona babu zenu zamani walikunywa miti shamba na walipona? Hapa kazi tu mlifikiri lelemama viwanda haviwezi kuja kwa kuendekeza mambo madogomadogo kama haya.

Suala la afya sio dogo,unless unajoke
 
Akiongea mbele ya Naibu Waziri Selemani Jafo,Mganga Mkuu wa Iramba ametoa taarifa kuwa hawajapokea fedha za Madawa toka July 2016!

DMO alijikita zaidi kuonyesha uhaba wa pesa za dawa na motisha kwa watumishi wa afya,pia uhaba wa watumishi.

Amesema serikali ijitahidi kuleta pesa kwa wakati ili kuwezesha huduma.

Hii ni kuikashifu serikali ya JPM ambayo imefunja rekodi Afrika Mashariki na kati ya kukusanya mapato kiasi cha kununua ndege mbili kwa mpigo kwa keshi.
Kaamua liwalo na liwe!
 
Yaan kwenye huu uzi ndio sehem ya kuchambua iQ za watz. Yaan wameshindwa kabisa nini lengo la mleta habar, daa Tz yangu. Mleta mada kaweka kichwa kama kile sababu katika serikali hii ukiisema ukweli serikali ya JPM unawekwa ndani. Na ndio maana anasema ni uchochozi. Mbona yule mtangazaji aliwaambia chakula hamna mkamtia ndani??

Hapa kaongea kwa fumbo kuwasimanga !!!

Wamemuelewa vibaya,kumbe mleta mada anamaanisha MDO kasema kitu ambacho wakubwa hawapend kisemwe
 
Wananchi mkiumwa mjitetemeshe wenyewe kujitibu. Muelewe kuwa magonjwa hayaletwi na serikali wala CCM! Msisubiri serikali iwahudumie maana haina fedha. Pia msikae kulalamikalalamika tu bali mfanye kazi!
Na madokta wa mitishamba mjini wamewapiga burn..shida sana hii nchi
 
Kuna wale waliambiwa wapige mbizi kama hawana nauli, wengine waliambiwa wanye barabarani kinyesi kitajeuka lami

Bado tu hamjakoma sasa mnalalamika dawa suburini jibu mtalipata
 
Back
Top Bottom