Dkt. Wilbroad Slaa atumia lugha kali dhidi ya Rais Samia

Naandika Rashda binti Zunde✍️

Watanzania amkeni, Watanzania amkeni tupinge watu kama hawa wanaotusi viongozi wa nchi hadharani. Tuungane kukemea vitendo kama hivi huu ni udharirishaji wa Rais wetu, huwezi kutoka hadharani kusema "hoja za rais ni za kipumbavu".

Wote tunajua kwamba Rais Samia Suluhu ameweka wazi dhamira yake ya kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana na tayari mchakato umeanza, hivi awamu gani iliwasikiliza chadema kama sio hii ya Mama Samia ?

Mchakato wa Katiba si wa siku moja, serikali imeshaanza mchakato, mmeshirikishwa, na sasa ni kutoa elimu kwa wananchi jambo ambalo serikali tayari ilishaweka wazi kwamba zaidi ya 50% ya Watanzania hawajui kuhusu katiba hivyo ni lazima wapatiwe elimu.

Lazima kila Mtanzania aelewe nini kinaenda kufanyika na ndicho serikali inachofanya, sasa wewe Slaa unavyokuja kusema kwamba hoja za Rais Samia Suluhu ni za kipumbavu umekosea sana, ni dhahiri kwamba hujafuatilia nini kinaendelea umekurupuka.

#mamaanafanikisha uhuru wa maoni lakini sio kutoka hadharani kumtusi kiongozi wako wa nchi, Slaa kaa chini tafakari kabla ya kuzungumza mbele za watu. Unajidharirisha kila siku na ndio maana umevuliwa ubalozi sababu huna hadhi na hakuna balozi mwenye tabia kama zako.

Mchakato wa kutoa elimu ya Katiba mpya unaendelea?! Tangu lini mmeanza kuwaonea huruma wananchi?! Mbona hamkutoa elimu ya IGA kati ya DPw na Tanganyika kwa wananchi kabla ya kusign ili waweze kuilewa na kujua nini Kiko ndani ya hiyo IGA? Badala yake mkasign kimyakimya hadi ilipotufikisha hapa tulipo.
Leo mnajinasibu kutoa Elimu ya Katiba Kwa wananchi wakati mnajua kabisa uundwaji wa Katiba hupitia hatua ya kuchukua maoni ya wananchi kabla ya drafting?! Kwenda zako huko.
 
Una uhakika kama wewe upo macho kweli!
Kuna viashiria vingi kuwa wewe umelala usingizi wa "pono"
 
Mchakato wa kutoa elimu ya Katiba mpya unaendelea?! Tangu lini mmeanza kuwaonea huruma wananchi?! Mbona hamkutoa elimu ya IGA kati ya DPw na Tanganyika kwa wananchi kabla ya kusign ili waweze kuilewa na kujua nini Kiko ndani ya hiyo IGA? Badala yake mkasign kimyakimya hadi ilipotufikisha hapa tulipo.
Leo mnajinasibu kutoa Elimu ya Katiba Kwa wananchi wakati mnajua kabisa uundwaji wa Katiba hupitia hatua ya kuchukua maoni ya wananchi kabla ya drafting?! Kwenda zako huko.
Rushwa hufanya watu kuwa vipofu!
CCM imekuwa; kipofu, kiziwi, kiwete na ukichaa sababu ya rushwa
 
Naandika Rashda binti Zunde[emoji3578]

Watanzania amkeni, Watanzania amkeni tupinge watu kama hawa wanaotusi viongozi wa nchi hadharani. Tuungane kukemea vitendo kama hivi huu ni udharirishaji wa Rais wetu, huwezi kutoka hadharani kusema "hoja za rais ni za kipumbavu".

Wote tunajua kwamba Rais Samia Suluhu ameweka wazi dhamira yake ya kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana na tayari mchakato umeanza, hivi awamu gani iliwasikiliza chadema kama sio hii ya Mama Samia ?

Mchakato wa Katiba si wa siku moja, serikali imeshaanza mchakato, mmeshirikishwa, na sasa ni kutoa elimu kwa wananchi jambo ambalo serikali tayari ilishaweka wazi kwamba zaidi ya 50% ya Watanzania hawajui kuhusu katiba hivyo ni lazima wapatiwe elimu.

Lazima kila Mtanzania aelewe nini kinaenda kufanyika na ndicho serikali inachofanya, sasa wewe Slaa unavyokuja kusema kwamba hoja za Rais Samia Suluhu ni za kipumbavu umekosea sana, ni dhahiri kwamba hujafuatilia nini kinaendelea umekurupuka.

#mamaanafanikisha uhuru wa maoni lakini sio kutoka hadharani kumtusi kiongozi wako wa nchi, Slaa kaa chini tafakari kabla ya kuzungumza mbele za watu. Unajidharirisha kila siku na ndio maana umevuliwa ubalozi sababu huna hadhi na hakuna balozi mwenye tabia kama zako.

Tufunge mjadala nafikiri huu mkataba nipeni mimi niufuatilie ninyi wengine endeleeni na kazi zenu nikieleweshwa mimi kwenu itakuwa Rahisi kuelewa
Ngojeni Mrejesho toka kwangu haya mkaendelee na kazi zenu mpate chochote kitu mkono uende kinywani haya mambo ya mkataba sijui umefanyeje niachieni nitamaliza sintofahamu hii Soon[emoji122]
 
Hi wizara ya mambo ya ndani apewe kichaa mmoja mwaka tu inatosha. Hawa mbwa baada ya miaka 60 ndio wanataka kujifananya wanauchungu sana, walikuwa wapi miaka yote... Mama Samia acha kuwachekea hawa huruma zako sio sehemu yake hii, sisi tunaonya tu hawa sio wa kufumbia macho fyekaaaa huko.
 
Neno upumbavu au mpumbavu limetajwa mara 99 kwenye kitabu cha Biblia

Kwenye Quran neno upumbavu limeonekana mara 7

Sasa neno "upumbavu" ni tusi imekuwaje likaandikwa kwenye vitabu tukufu ambavyo raisi hutumia kuapia?
 
Naandika Rashda binti Zunde✍️

Watanzania amkeni, Watanzania amkeni tupinge watu kama hawa wanaotusi viongozi wa nchi hadharani. Tuungane kukemea vitendo kama hivi huu ni udharirishaji wa Rais wetu, huwezi kutoka hadharani kusema "hoja za rais ni za kipumbavu".

Wote tunajua kwamba Rais Samia Suluhu ameweka wazi dhamira yake ya kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana na tayari mchakato umeanza, hivi awamu gani iliwasikiliza chadema kama sio hii ya Mama Samia ?

Mchakato wa Katiba si wa siku moja, serikali imeshaanza mchakato, mmeshirikishwa, na sasa ni kutoa elimu kwa wananchi jambo ambalo serikali tayari ilishaweka wazi kwamba zaidi ya 50% ya Watanzania hawajui kuhusu katiba hivyo ni lazima wapatiwe elimu.

Lazima kila Mtanzania aelewe nini kinaenda kufanyika na ndicho serikali inachofanya, sasa wewe Slaa unavyokuja kusema kwamba hoja za Rais Samia Suluhu ni za kipumbavu umekosea sana, ni dhahiri kwamba hujafuatilia nini kinaendelea umekurupuka.

#mamaanafanikisha uhuru wa maoni lakini sio kutoka hadharani kumtusi kiongozi wako wa nchi, Slaa kaa chini tafakari kabla ya kuzungumza mbele za watu. Unajidharirisha kila siku na ndio maana umevuliwa ubalozi sababu huna hadhi na hakuna balozi mwenye tabia kama zako.

Huyo mbwa azimwe iwe mfano,kusamehe kazi ya mungu,apelekwe na kundi lake wakapate msamaha
 
Napata hasira sana na serikali yetu kuwafumbia hawa watu macho, hapa ndio namkumbuka JPM hawa leo wangekuwa history. Usiruhusu watu kutaka kuleta uchochezi kutuharibia amani ya nchi, tukosoane lakini kwa staha. Leo anakuja huyo Mwambukusi sijui anasema yuko tayari kupigania kwa lolote hata kufa utasema alizaliwa jana, huko nyuma alikuwa wapi? kwani haya mambo yameanza leo? Serikali ni wakati sasa wakupitisha maamuzi magumu kwa mustakabali wa nchi yetu, kuna watu hawataki amani nchi hii.
Mnavyozungumzia hiyo Amani utafikiri dunia nzima ipo machafukoni kasoro Tanzania tu, nchi za wenzetu zina amani na zina maendeleo ila bado wananchi wana uhuru wa kuandamana,kufanya migomo na kutoa maoni yao kwa uhuru bila hofu. Sasa Tanzania kukosoa tu unaonekana ni adui wa serikali unaweza ukapewa hadi cheo ili kunyamazishwa mdomo achilia kupewa vitisho, maandamano yanazuiliwa yani serikali inataka watu wakae tu kimya au uwasifie basi.

Sasa hiyo Amani au upumbavu?
 
Ungehamia tu huko ukaandamane mpaka uchoke. Kosoa lakini sio kwa lugha ya kukashifu. Sasa tukianza kuandamana kama wanaharakati halafu kesho wengine wakitaka kuandamana na wengine mwisho wa siku tutakuwa kama bonanza mitaani. Fanyeni kazi, sasa tutaona hiyo siku atakayotoka kuandamana ndio ataita maje mmaaaaa.
 
Mnavyozungumzia hiyo Amani utafikiri dunia nzima ipo machafukoni kasoro Tanzania tu, nchi za wenzetu zina amani na zina maendeleo ila bado wananchi wana uhuru wa kuandamana,kufanya migomo na kutoa maoni yao kwa uhuru bila hofu. Sasa Tanzania kukosoa tu unaonekana ni adui wa serikali unaweza ukapewa hadi cheo ili kunyamazishwa mdomo achilia kupewa vitisho, maandamano yanazuiliwa yani serikali inataka watu wakae tu kimya au uwasifie basi.

Sasa hiyo Amani au upumbavu?
Kumbuka Serikali imechaguliwa na watu na ndio majority, wewe unashida subiri uchaguzi chagua unayemtaka. France wale watu wakitoka kuandamana wanawafanya nini? London walifanywa nini? kila jambo linaukomo wake wewe kama hupendi kuna watu wanapenda. Majority rule basi.
 
Turudi kwenye hoja kwani, baada ya mchakato na hoja za katiba pendekezwa, tunaanza upya tena au tunaendeleza tulipoishia, mzee ana hoja. Rais Samia ana akili sana, kwa vyovyote vile kwa muda uliobaki hatuwezi kupata Katiba Mpya kabla ya uchaguzi 2025, kinacheweza kufanyika ni malidhiano katika vipengele vya uchaguzi, lakini pia kuna uwezekano mkumbwa wa mchakato kuanza rasmi 2025, kwa maana hiyo kuweka kipindi cha mpito kufanya uchagizi wa katiba mpya kati ya mwaka 2027 au zaidi na Samia kuendelea kuwa Rais wa mpito hata bila uchaguzi, cha msingi hapa tunaomba kuwe na dhamila ya kweli ya serikali na hasa chama CCM kikubali kubadilika na kukubalii matokeo.
ninaamini amani ni nambli moja. Mama avumilie tu matusi hayavunji mfupa wote tunaishi na tunaishia kikubwa Utukufu kwa Bwana Mungu wetu.
 
Watu wamechafukwa sana sasa hivi kwa vitu ambavyo serikali inafanya.
 
Back
Top Bottom