Dkt. Slaa: Wapo viongozi walichaguliwa kwa uchaguzi unaopatikana Tanzania tu

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Dkt. Slaa amesema wabunge wa CCM baadhi walichaguliwa kwa uchaguzi unaopatikana Tanzania tu, yaani uchaguzi wa kupita bila kupingwa, moja ya madhara ya kuwepo kwa jambo hilo ni kuzalisha idadi kubwa ya wabunge ambao ni wa chama kimoja (CCM).

Kuwepo kwa wabunge wengi wa chama kimoja bungeni kunapunguza au kuondoa kabisa ufanisi na dhima ya kuwepo kwao bungeni kwani wanakuwa na deni la kulipa kwa waliofanikisha kuwepo kwao na ivyo kuunga mkono kila kitu bila kuhoji, kwa akili ya kawaida tu unawezaje kumpinga mtu anayekuweka mjini? Huwezi lazima ukubali hata kama unaona anazingua.

Hili la kupita bila kupingwa ni moja ya kitu cha kushangaza kwa uchaguzi uliopita matokeo yake mikataba na mambo mengine yanapita tu kwa kura za ndiooooooo bila hata kuhojiwa.
 
Sitawapa salamu nimechafukwa

Dkt. Slaa anaeleza kwamba Mahakama ilishatengua ubunge wa wabunge waliopita bila kupingwa ikiwepo Waziri Mkuu.

Anasema hana imani na Bunge kwa sababu lina wabunge wasiotambulika kikatiba. Kwa sababu Mbunge wa Ruhangwa ni batili maana yake nchi haina Waziri Mkuu halali.

Dr. Slaa kachefukwa mno
 
Sitawapa salamu

Dr. Slaa anaeleza kwamba Mahakama ilishatengua ubunge wa wabunge waliopita bila kupingwa ikiwepo Waziri Mkuu.
Anasema hana imani na Bunge kwa sababu lina wabunge wasiotambulika kikatiba.
Kwa sababu Mbunge wa Ruhangwa ni batili maana yake nchi haina Waziri Mkuu halali.

Dr. Slaa kachefukwa mno
Yupo sahihi ila sasa ni nani wa kwenda kumtoa pale kitini PM wa mchongo!?
 
Back
Top Bottom