Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM kuficha maovu yake!

Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM kuficha maovu yake!

kama unafanya kampeni muda wake bado,subiri 2015 ndio uanze kumsifia huyo mtu wako mwenye tabia chafu ya kunyanganya watu wake zao,je akiwa rais si itakuwa balaa zaidi?
 
Kwako ni nani ?Ni Mungu wako nini?
Kwangu ni Mh rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,na tunamshukuru mungu anamalizia kipindi chake cha pili cha utawala ingawa wachache wenye wivu hawataki lakini mungu ndio ameshapanga iwe hivyo.
 
kama unafanya kampeni muda wake bado,subiri 2015 ndio uanze kumsifia huyo mtu wako mwenye tabia chafu ya kunyanganya watu wake zao,je akiwa rais si itakuwa balaa zaidi?
Baelezee hao
 
kama unafanya kampeni muda wake bado,subiri 2015 ndio uanze kumsifia huyo mtu wako mwenye tabia chafu ya kunyanganya watu wake zao,je akiwa rais si itakuwa balaa zaidi?

Vipi, ushamsikia mzee wako anamlalamikia nini?
 
Ninayo picha yake kubwa inayotumiwa kama picha rasmi ya raisi ametambulishwa kama Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete hivyo yeye mwenyewe anajitambua kama ndg
Tuletee na ya padre Slaa akiwa ndani ya joho lake.
 
Mkuu, kwa kichwa hicho cha habari utawaingiza wengi mkenge kama tayari unavyoshuhudia hapo juu walivyokuja mbio wakakuta sio wakaanza kuporomosha matusi (maneno mbofu mbofu).

Mkuu Komeo

Kabla sijakuandikia na vitu vingine ukiachilia mbali hilo la Konja, Zanzibar, soma stori zifuatazo, kwa uchache;

Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM
*Asema unaibuliwa kufunika udhaifu wa uongozi


Na Tumaini Makene


TATIZO la udini unaodaiwa kuwepo nchini umeelezewa kuwa ni propaganda inayotumika kuficha udhaifu wa kiuongozi ili wananchi waache kujadili
mambo ya msingi ya taifa, ikiwemo chama kilichoko madarakani kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa miongo mitano iliyopita.


Imeelezwa kuwa wananchi wa Tanzania wanaendelea kuishi kwa amani, upendo na mshikamano bila kujali tofauti zao za kidini, hivyo viongozi nchini wametakiwa kuacha kuwagawanya Watanzania kwa manufaa yao ya kisiasa.


Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa alipokuwa akisoma tamko la Kamati Kuu (CC) juu ya hali ya siasa nchini na masuala mengine ya kitaifa katika nyanja mbalimbali.


Dkt. Slaa alisema kuwa CC ya CHADEMA imeazimia kuwahimiza viongozi wa dini zote hapa nchini kuendelea kukemea maovu yoyote katika jamii bila woga wala upendeleo kwani hilo ni jukumu lao la msingi.


"Kamati kuu imesikitishwa na propaganda zinazoendelezwa na viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi, hususan Rais Kikwete, kuhusu kuwepo kwa mfarakano wa kidini hapa nchini. Kamati Kuu imezingatia kuwa wananchi wa Tanzania wameendelea kuishi kwa amani, upendo na mshikamano mkubwa bila kujali tofauti zao za kidini.


"Kamati kuu imezingatia kuwa viongozi wa juu wa CCM na hasa Rais Kikwete, wameamua kuficha udhaifu wake wa kiuongozi chini ya zulia la udini ili wananchi waache kujadili mambo ya msingi ya taifa hili, ikiwemo kushindwa kwa CCM kutekekeza ahadi ambazo imekuwa ikizitoa katika miongo mitano iliyopita," alisema Dkt. Slaa na kuongeza;


"Hivyo basi kamati kuu imewahimiza wananchi wa dini zote hapa nchini kuendelea kuishi kwa amani na mshikamano na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii, bila kujali tofauti zao za dini, ukabila wala itikadi ya siasa.


"Kamati Kuu imewataka viongozi wa juu wa CCM na hasa Rais Kikwete kuacha kuchochea mgawanyiko wa dini hapa nchini kama njia ya kuficha udhaifu wake wa uongozi...imewahimiza viongozi wa dini zote hapa nchini kuendelea kukemea maovu yeyote nchini bila woga wala upendeleo kwani hilo ni jukumu lao la msingi."


Ushirikiano wa vyama


Kwa mujibu wa Dkt. Slaa aliyesoma tamko hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari, alisema kuwa CC ya chama hicho ilitafakari juu ya umuhimu wa ushirikiano wa vyama vya siasa ili kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini na kumuagiza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli kwa kuhusisha wabunge wa CHADEMA pekee.


"Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, kamati kuu imezingatia kuwa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.


"Na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za muungano na kwa kuwa vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge vimo katika ushirikiano na CUF, Kamati Kuu imeona kuwa CHADEMA haiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo," alisema Dkt. Slaa.


Akifafanua hatua hiyo, Dkt. Slaa alisema kuwa ni vigumu kwa CHADEMA kuwa na ushirikiano wa CUF, wakati kiko serikalini, kikitimiza majukumu ya kiserikali pamoja na chama kilichoko madarakani sasa, CCM, hivyo ni vigumu kushirikiana na wapinzani ambao tayari ni sehemu ya utawala.


Akizungumza juu ya uwezekano wa CHADEMA kushirikiana na vyama vingine vilivyoungana na CUF katika kile kinachoitwa kamati ya wabunge wa upinzani wasiokuwa katika kambi rasmi, Dkt. Slaa alisema kuwa vyama hivyo navyo vimekuwa sehemu ya watawala kwa sababu vimeungana nao kupitia CUF.


"Sasa kwa mfano tukiazimia kitu kinachopingana na serikali, Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye Makamu wa kwanza wa Rais huko Zanzibar unategemea atakubaliana nacho ili apingane na serikali, hivi vyama vingine navyo tayari vimeshakuwa sehemu ya watawala maana wameamua kushirikiana na CUF katika kamati yao."


Mchakato wa katiba mpya


Juu ya suala la mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, CC ya CHADEMA ilipinga utaratibu wa uundwaji wa tume ya rais katika uundaji wa katiba mpya, ikisema si njia sahihi kwa upatikanaji wa katiba mpya yenye utashi, matakwa na mahitaji ya wananchi wa Tanzania, badala yake imeunga mkono utaratibu wa kutumia bunge katika kutengeneza na usimamia mchakato wa kuelekea kupatikana kwa katiba mpya.


Hivyo, mbali ya kuipongeza sekretarieti ya kamati kuu hiyo kwa kumwagiza Bw. John Mnyika (Mbunge wa Ubungo) kuandaa na kuwasilisha hoja binafsi inayolitaka bunge kuandaa sheria kuratibu mchakato wa katiba mpya, imewapongeza pia wadau mbalimbali wa demokrasia nchini kwa kudai mchakato wa nchi kuwa na katiba mpya.


"Kamati Kuu imejadili na kutafakari kwa kina maoni ya wadau mbalimbali juu ya mchakato unaofaa katika kupata katiba mpya na kuzingatia kuwa njia sahihi ni ile itakayowashirikisha wananchi kikamilifu na kwa dhati bila kujali tofauti zao za kisiasa, dini, umri, elimu, kabila wala jinsia zao,' alisema Dkt. Slaa.


Mauaji ya Arusha


Dkt. Slaa alisema kuwa CC ya CHADEMA imeiagiza sekretarieti ya CHADEMA kuendeleza harakati za kudai haki za wananchi wa Jiji wa Arusha kwa njia za kisiasa.


Pia iliwapongeza Bw. Freeman Mbowe, Dkt. Willibrod Slaa na Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema kwa juhudi zao za kuepusha shari na kutoa uongozi wa kisiasa "baada ya viongozi wa serikali ya CCM kuwatelekeza wananchi kwa kipindi chote cha matatizo ya Arusha."


"Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya wananchi watatu wasio na hatia kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi kufuatia vurugu zilizosababishwa na jeshi hilo katika harakati za kuzuia maandamano halali na yenye baraka zote za Kamanda wa Jeshi la Polisi wilayani Arusha.


"Kamati kuu imeskitishwa na uvurugwaji wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha kulikofanywa na mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi na serikali yake...kamati kuu imewapa pole ndugu wa wafiwa wa vurugu za Arusha, wananchi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla.


Mbali ya kutoa pole, pia imewaagiza madiwani wa CHADEMA katika halmashauri ya jiji hilo kuendelea kuingia katika vikao vya baraza la halmashauri kuwawakilisha kikamilifu wananchi waliowachagua, lakini huku wakitumia nafasi yao kufanikisha uchaguzi wa meya.


Umeme, Gesi na malipo ya Dowans


Katika masuala hayo, Dkt. Slaa alisema "kamati kuu imeskitishwa na kupanda holela kwa bei ya nishati muhimu ya umeme na gesi, pamoja na kushindwa kwa serikali ya CCM katika kuwekeza kikamilifu katika sekta ya nishati hapa nchini.


"Kamati kuu imesikitishwa na kufadhaishwa sana na uamuzi wa CCM na serikali yake kuridhia kuilipa kampuni hewa ya Dowans fedha za walipa kodi wa Tanzania zipatazo sh. bilioni 94 pamoja na kwamba kampuni hii ilikwishaharamishwa na bunge kwa niaba ya wananchi...imetambua kuwa sakata la Dowans ni mwendelezo wa vitendo vya kifisadi ndani ya CCM na serikali yake."


Alisema kuwa mbali ya kuwahimiza wana CHADEMA, wabunge na wananchi kwa ujumla kuendelea kupinga kwa nguvu zote malipo ya Dowans, CC ya chama hicho pia imeiagiza sekretarieti yake kuanza maandalizi ya maandamano ya nchi nzima kupinga ongezeko la bei ya umeme, gesi na kuilipa Dowans, yatakayoanzia jijini Mwanza, Februari 24, mwaka huu.


Alisema CC imewaelekeza viongozi wa CHADEMA kuendelea kuwahamasisha wananchi kupinga kwa njia mbalimbali za kisiasa na kisheria malipo ya Dowans na ufisadi mwingine nchini, huku ikiwapongeza wanaharakati wa masuala ya kiraia kwa ujasiri na moyo wa kizalendo wa kufungua kesi kupinga malipo hayo.


"Kamati kuu imeiasa Serikali ya CCM kutokuona aibu kutekeleza sera za CHADEMA zilizofanyiwa utafiti kuhusu namna ya kujenga na kuimarisha sekta ya nishati ya umeme na gesi hapa nchini ili nchi yetu iondokane na tatizo la kudumu la umeme."


Matokeo ya Kidato cha nne


Dkt. Slaa alisema kuwa kutokana na nusu ya watahiniwa wote kutofaulu mitihani, huku asilimia 11.5 pekee kati ya waliotahiniwa wakipata daraja la I,II na III, ambapo karibu asilimia 90 ya wanafunzi hawataweza kuendelea na masomo ya elimu ya juu, CC ya CHADEMA imeyatangaza matokeo hayo kuwa ni janga la kitaifa.


Mbali ya kusema kuwa vijana hao hawataweza pia kupata ajira ya uhakika, kamati kuu ya CHADEMA imesema kuwa matokeo hayo mabaya yamesababishwa na sera dhaifu za Serikali ya CCM zenye kulenga kughilibu wananchi kwa ajili ya mafanikio ya kisiasa kwa kukazia wingi wa majengo ya shule badala ya ubora wa walimu na shule.


"Kamati kuu imeitaka Serikali ya CCM isione aibu kutekeleza sera za elimu za CHADEMA zilizoainishwa katika ilani yake ya mwaka 2010, na imeunda timu maalumu ya wataalam wa elimu kwa ajili ya kutafiti kwa kina sababu za matokeo mabaya ya kidato cha nne na kutoa mapendekezo yake kwa kamati kuu," alisema Dkt. Slaa.
 
Ninayo picha yake kubwa inayotumiwa kama picha rasmi ya raisi ametambulishwa kama Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete hivyo yeye mwenyewe anajitambua kama ndg
Huyu Mingoi anataka jamaa yake aitwe Mheshimiwa Rais Doctor!teh teh teh!
 
Last edited by a moderator:
Raia Mpotevu haliwezi kumwita Mh Rais ndugu Kikwete


Mpaka hapo umejionyesha kwamba wewe ndiye punguani,aliyeagiza aitwe ndugu Jakaya Kikwete
ni yeye mwenyewe Rais wewe ni nani hata ushindane na hili,ushabiki bila elimu wala ujuzi"
 


Mkuu Komeo

Kabla sijakuandikia na vitu vingine ukiachilia mbali hilo la Konja, Zanzibar, soma stori zifuatazo, kwa uchache;

Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM
*Asema unaibuliwa kufunika udhaifu wa uongozi

Mkuu nashukuru kwa kunikumbusha maandiko haya. Tatizo wapo watu wapenda vyeo vya upendeleo ndio wameshaona jinsi ya kutoka ni kumtukana Dr Slaa. Ndio maana nikasema kichwa cha habari kinawavuta watukanaji halafu wanakuta hakuna uwanja wa matusi.
 
Bado hatumfahamu labda uwe unamaanisha Mh Rais Dr Jakaya M Kikwete rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ( Chaguo la mungu).

Tumia akili wewe nenda hata leo picha hata iliyoko pale Ikulu imeandikwa Ndugu Jakaya"
 
Mpaka hapo umejionyesha kwamba wewe ndiye punguani,aliyeagizwa aitwe ndugu Jakaya Kikwete
ni yeye mwenyewe Rais wewe ni nani hata ushindane na hili,ushabiki bila elimu wala ujuzi"
Ushabiki wa kukalili mambo matokeo yake ni kuumbuka!
 
Mingoi kwani kumuita mtu NDUGU umemkosea heshima?Mbona enzi za Nyerere walikuwa wanaitwa wandugu?Au ulitaka aitwe Mtukufu Rais?Mtukufu ni Mungu tu.Sijaona ubaya wa Rais Jakaya Kikwete kuitwa ndugu kwani hajavunjiwa heshima ndugu yangu Mingoi.Unisamehe kama nitakuwa nimekukwaza kwani wakati mwingine ukweli hushinda uongo.
 
Maji taka haya!!!!!! ulikuwa chooni wakati unapost hii thread???!!!!

ukweli ni kwamba hiyo ndio mbinu mbovu iliyotupatia watawala wa serikali tulionao sasa na hiyo dhambi ndio inayowatafuna serikali na mkuu wa nchi ndio maana hawezi kuwaambia chochote ndugu zetu waislam wanaoleta choko choko ya kuvuruga umoja wa watanzania kwa sababu aliwatengeneza yeye mwenyewe!!!!!!
 
Tumia akili wewe nenda hata leo picha hata iliyoko pale Ikulu imeandikwa Ndugu Jakaya"
Soma maneno yote yaliyoandikwa kwenye hiyo picha wewe unatumia visigino kufikiri.Ukoo wa Kikwete ni mkubwa uankuja na story lazima utenganishe hata kwa vyeo sasa unapotaja ndugu Kikwete wengine tunafahamu zaidi Selemani na Yusufu.
 
Back
Top Bottom