Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM kuficha maovu yake!

Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM kuficha maovu yake!

Udini tena acha nijiendee zangu mie hapa hakuna cha kuchangia
 
Dr, The super special one ! He always answer kwa vitendo na facts !
 
Peace, whatever it takes. I couldn't care less who was the president. I just want to be able to live and let others live. If one policy doesn't work, there should always be room for change. Nothing man-made is perfect, including systems, policies and institutions. What works for one person may not work for another. It's a matter of looking for the best way forward that works for us, not following blindly in other's footsteps or being stuck in outdated politics. Dr W Slaa is the one to take us forward.
 
Mleta mada naona hapa kapindisha maelezo yake kama Anne Makinda na Jobb Ndugai wanavyopindisha sheria za Bunge hapa kamsema Jakaya Kikwete,Kati ya Kikwete na Dr Slaa(PHD)nani muanzilishi wa udini hadi leo umetapakaa nani kaahidi MAHAKAMA YA KADHI kama sio Kikwete na CCM yake.Wote tukumbuke kuwa nchi yetu haina DINI sasa hili la kuwaambia watu wa dini moja kuwa mtapata MAHAKAMA YA KADHI imetoka wapi??Kaka/dada ulioleta hii mada naomba sana tena kwa heshima na taadhima ukarudie tena kuleta mada au niseme hebu ipitie upya urekebishe au nikupe akiba ya maneno badala ya DR kuwa mdini hebu muweke Kikwete na CCm.Pole sana kama ulilipwa hiyo dhambi yako utajiju njaaa ni nomaaaaa
 
Kuna watu kila siku hawalali wanawaiza chadema inavyowachachafya.Pamoja na dini zetu tushirikiane kuondoa watu hawa wenye kupika maneno yasiyo na maana kwa watanzania.
Wameshindwa kuumiza kichwa namna ya kudhibiti wizi wa mali za umma, namna ya kuinua huduma za afya, maji, elimu, kilimo kwa watanzania.Dr Slaa hana wakufananisha naye na ndiye Rais wa Tanzania 2015
 
kenge wewe unayefikiria kwa ku2mia ------ we mdini namba moja kama unamwogopa dr tafuta njia nyngne.
 
Wadini ni nyie ccm mbona mpo kimya na harakati za waislam ilihali wanavitenda vya wazi vinavyoonyesha udini na mnakaa kimya kwa JK si alikua anapiga kampeni misikitini. Kwa taarifa yako wakristo ndo wengi kuliko waislamu. Mbona rais ni mwislamu acheni propaganda zenu. Dr hana la kujibu kwani hiyo si hoja ya chama wanaoelewa cdm wanajua slaa ni wa style gani. We umeona hilo tu mbona mnasema kapola mke kakimbia upadri hajatetereka ukweli utabaki palepale

Mkuu sina uhakika kama umesoma thread yote kuanzia mwanzo hadi mwisho, naamini kwa dhati ungelisoma yote, usingelimshukia mtoa mada namna hii. Heading imekupotosha. Kazi kweli kweli, nimeamini watz wengi hatusomi contents, tunaishia kwenye heading tu.
 
Mleta mada naona hapa kapindisha maelezo yake kama Anne Makinda na Jobb Ndugai wanavyopindisha sheria za Bunge hapa kamsema Jakaya Kikwete,Kati ya Kikwete na Dr Slaa(PHD)nani muanzilishi wa udini hadi leo umetapakaa nani kaahidi MAHAKAMA YA KADHI kama sio Kikwete na CCM yake.Wote tukumbuke kuwa nchi yetu haina DINI sasa hili la kuwaambia watu wa dini moja kuwa mtapata MAHAKAMA YA KADHI imetoka wapi??Kaka/dada ulioleta hii mada naomba sana tena kwa heshima na taadhima ukarudie tena kuleta mada au niseme hebu ipitie upya urekebishe au nikupe akiba ya maneno badala ya DR kuwa mdini hebu muweke Kikwete na CCm.Pole sana kama ulilipwa hiyo dhambi yako utajiju njaaa ni nomaaaaa

Hili ni tatizo la kuelewa na kutafsiri. Sasa hiki ni kiswahili, kinatupa shida kabisa kuelewa, je ingelikuwa kidhungu? Kazi kweli kweli, kaka soma maandishi ya mleta mada vyema na tafsiri, usiishie kwenye heading tu, content ni tofauti sana na heading, sijui, lakini mm nimeelewa vyema sana. Mleta mada amemsifia Dr Silaa kwa kutokuwa mdini na siyo kwamba amemponda kuwa ni MDINI. Uelewa unatofautiana sana.
 
Toka alipotangazwa kugombea nafasi ya urais kwa ticketi ya CHADEMA, na kipindi chote cha Kampeni mpaka mpaka uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kufanyika, matokeo kutangazwa na mpaka leo hii, ziliibuka shutuma nyingi sana kwamba DR SLAA ametumwa na kanisa kusimika mfumo kiristo katika serikali yetu.

Hali ilifikia mbaya sana, baada ya mpaka Ndugu Kikwete kutoa maelezo katika Bunge letu yaliyomaanisha kwamba watu walipiga kura kwa misingi ya kidini, mwingine ni Naibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, huku akitambua vyema kwamba muelekeo wa kauli kama ya Ndugu Kikwete haukuwa na nia njema kwa Chama chake, nae alipata kutoa kauli ya namna hiyo, na zote zikimaanisha kwamba watu walimpigia kura dr slaa kutokana na ukirsto wake.

Hapa kuna vitu viwili, mtu kupiga kampeni zenye misingi ya udini na watu kupiga kura kwa misingi ya udini.
Kama Taifa hatuhitaji kupata kiongozi ambaye ameingiwa na upumbavu wa kutafuta nafasi ya kutuongoza kwa kupiga kampeni na kutegemea kupata ushindi kwa kutumia udini, na ninaamini kabisa kwamba mpiga kura yeyote makini hawezi kukubaliana na mpumbavu wa namna hiyo.

Swala la mtu kupiga kura kwa misingi ya kidini, hili ni gumu sana kukabiliana nalo, labda mtu wa namna hii aende mbele zaidi na kuanza kumpigia debe mdini wake, hivyo hili ni tatizo la kijamii ambalo tunapaswa kushirikiana kukabiliana nalo,lakini si sawa hata kudogo kudai uchaguzi uligubikwa na udini kwa kuwaangalia wapiga kura,

Ni upumbavu pia mtu kutumia nafasi yake kuwashawishi watu kumpigia kura mgombea fulani, kama ilivyo upumbavu kwa mmliki wa kampuni kuwalazimisha au kuwashawishi wafanyakazi wake kutokana na mahusiano yao kumpigia kura mgombea fulani, vivyo hivyo ni upumbavu kwa kiongozi wa dini kuwaelekeza waamini anaowaongoza kumpigia kura mtu mwenye imani kama yao.

Nachokiona cha Ajabu kwa DR SLAA ni namna alivyokabiliana na changamoto hii, sababu sikupata kumsikia akitoa utetezi wa namna yeyote ile kupinga kwamba hana hurka za kidini, hasa kwamba hategemei kusimamia serikali yetu kwa misingi inayopendelea ukirsto au ukatoriki wale wala kukandamiza wakiristo wa madhehebu mengine au wananchi wenye imani tofauti au wapagani, mara zote aliomba wananchi kutokudanganywa na kuacha kusimamia misingi ya utaifa wetu.

Mtu wa kawaida, angeweza kueleza jinsi mahusiano yake na waislamu yalivyo mazuri na kutoa mifano ya waislamu alioshirikiana nao vizuri akiwa karatu na maeneo mengine, hakufanya hivyo, hakutafuta sympathy, aliendelea kusimamia misingi sahihi ya kupata uongozi katika Taifa letu.

Wonderfully, kumbe amekwishawahi kufanya kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza akakikubari kwa urahisi, kwamba akiwa kiongozi wa kanisa katoriki, huko nyuma, yeye dokta slaa, alisimamia watu wa eneo linaitwa kojani huko zanzibar kupata huduma ya maji ambayo wanayatumia mpaka leo, na anasema anauhakika kwamba, eneo hilo halina mkirsto hata mmoja isipokuwa waislamu tu. but he did it. Ajabu kabisa.

Cha Ajabu kwangu ni kwamba hakuona hata kidogo kama hii ni sababu ya kutafutia kura za waislamu wakati wa kampeni.

Mnyong'e Mny'ongeni, haki yake mpeni.
Wapo watu wanamtukana hapa kila siku, lakini hawajawahi kuchangia hata ujenzi wa Madrasa.

Source: Raia Mwema
mkuu kama si mahubiri ya kanisani basi slaa na wabunge wake wasingepata kura ambazo ziko bias kwa maeneo ya wakristo kama inavyoonekana, ukiondoa jimbo la Arfi na Zitto ambalo hata leo akihamia NCCR atahama nalo kama alivyofanya Kafulila. Ukubali usikubali, huo ndo ukweli. slaa mwenyewe analijua hilo na ndo maana baadhi ya maeneo yenye watu wa imani fulani hajawahi kanyaga maisha yake yote. safari ijayo asifanye hivyo. kuhusu kutoa msaada zenje ni njia tu za kupeleka ubatizo, kwani madhila waliyonayo wazenji leo pamoja na madawa ya kulevya, uchangu, mabaa na kadhali ni zawadi za wabara kupitia muungano.
 
nasikia wanalipwa kwa posts wanapigiana hesabu
Teh teh teh!hata kama wanalipwa hivyo haitamaliza umasikini wao,na CCM watawatumia kama kondomu,baadaye watatupwa kwenye dustbin!
 
Back
Top Bottom