Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM kuficha maovu yake!

Dkt. Slaa: Udini ni propaganda ya CCM kuficha maovu yake!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,254
*Asema unaibuliwa kufunika udhaifu wa uongozi

Na Tumaini Makene

TATIZO la udini unaodaiwa kuwepo nchini umeelezewa kuwa ni propaganda inayotumika kuficha udhaifu wa kiuongozi ili wananchi waache kujadili mambo ya msingi ya taifa, ikiwemo chama kilichoko madarakani kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa miongo mitano iliyopita.

Imeelezwa kuwa wananchi wa Tanzania wanaendelea kuishi kwa amani, upendo na mshikamano bila kujali tofauti zao za kidini, hivyo viongozi nchini wametakiwa kuacha kuwagawanya Watanzania kwa manufaa yao ya kisiasa.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa alipokuwa akisoma tamko la Kamati Kuu (CC) juu ya hali ya siasa nchini na masuala mengine ya kitaifa katika nyanja mbalimbali.

Dkt. Slaa alisema kuwa CC ya CHADEMA imeazimia kuwahimiza viongozi wa dini zote hapa nchini kuendelea kukemea maovu yoyote katika jamii bila woga wala upendeleo kwani hilo ni jukumu lao la msingi.

"Kamati kuu imesikitishwa na propaganda zinazoendelezwa na viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi, hususan Rais Kikwete, kuhusu kuwepo kwa mfarakano wa kidini hapa nchini. Kamati Kuu imezingatia kuwa wananchi wa Tanzania wameendelea kuishi kwa amani, upendo na mshikamano mkubwa bila kujali tofauti zao za kidini.

"Kamati kuu imezingatia kuwa viongozi wa juu wa CCM na hasa Rais Kikwete, wameamua kuficha udhaifu wake wa kiuongozi chini ya zulia la udini ili wananchi waache kujadili mambo ya msingi ya taifa hili, ikiwemo kushindwa kwa CCM kutekekeza ahadi ambazo imekuwa ikizitoa katika miongo mitano iliyopita," alisema Dkt. Slaa na kuongeza;

"Hivyo basi kamati kuu imewahimiza wananchi wa dini zote hapa nchini kuendelea kuishi kwa amani na mshikamano na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii, bila kujali tofauti zao za dini, ukabila wala itikadi ya siasa.

"Kamati Kuu imewataka viongozi wa juu wa CCM na hasa Rais Kikwete kuacha kuchochea mgawanyiko wa dini hapa nchini kama njia ya kuficha udhaifu wake wa uongozi...imewahimiza viongozi wa dini zote hapa nchini kuendelea kukemea maovu yeyote nchini bila woga wala upendeleo kwani hilo ni jukumu lao la msingi."

Ushirikiano wa vyama

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa aliyesoma tamko hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari, alisema kuwa CC ya chama hicho ilitafakari juu ya umuhimu wa ushirikiano wa vyama vya siasa ili kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini na kumuagiza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli kwa kuhusisha wabunge wa CHADEMA pekee.

"Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, kamati kuu imezingatia kuwa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

"Na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za muungano na kwa kuwa vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge vimo katika ushirikiano na CUF, Kamati Kuu imeona kuwa CHADEMA haiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo," alisema Dkt. Slaa.

Akifafanua hatua hiyo, Dkt. Slaa alisema kuwa ni vigumu kwa CHADEMA kuwa na ushirikiano wa CUF, wakati kiko serikalini, kikitimiza majukumu ya kiserikali pamoja na chama kilichoko madarakani sasa, CCM, hivyo ni vigumu kushirikiana na wapinzani ambao tayari ni sehemu ya utawala.

Akizungumza juu ya uwezekano wa CHADEMA kushirikiana na vyama vingine vilivyoungana na CUF katika kile kinachoitwa kamati ya wabunge wa upinzani wasiokuwa katika kambi rasmi, Dkt. Slaa alisema kuwa vyama hivyo navyo vimekuwa sehemu ya watawala kwa sababu vimeungana nao kupitia CUF.

"Sasa kwa mfano tukiazimia kitu kinachopingana na serikali, Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye Makamu wa kwanza wa Rais huko Zanzibar unategemea atakubaliana nacho ili apingane na serikali, hivi vyama vingine navyo tayari vimeshakuwa sehemu ya watawala maana wameamua kushirikiana na CUF katika kamati yao."
 
La kushangaza huu udini JK na CCM yake wameubuni baada ya uchaguzi huu wa 2011 lakini mwaka 2005 mambo yalipokuwa yakiwaendea vizuri hatukuusikia huu udini.................................ni dhahiri udini ni mtaji wa kisiasa wa CCM kutufanya tusihoji hivi JK alishindaje uchaguzi wa 2010 na wakati sisi hatukumchagua?

TISS na NEC itabidi wayajibu maswali haya ya kimsingi......................................................
 
na huu ndio ukweli wenyewe,Hongera mzee slaa naamini mungu ametupatia mkombozi wa taifa hili,
 
chama makini kwa watu makini wenye hoja makini. big up dr (PHD) Slaa & CDM, keep up the good work.
 
La kushangaza huu udini JK na CCM yake wameubuni baada ya uchaguzi huu wa 2011 lakini mwaka 2005 mambo yalipokuwa yakiwaendea vizuri hatukuusikia huu udini.................................ni dhahiri udini ni mtaji wa kisiasa wa CCM kutufanya tusihoji hivi JK alishindaje uchaguzi wa 2010 na wakati sisi hatukumchagua?

TISS na NEC itabidi wayajibu maswali haya ya kimsingi......................................................

Nadhani ni sahihi kusema kuwa uchaguzi wa mwaka 2010 ulitawaliwa na udini kwa vile mwaka 2005 hatukuona nyaraka mbalimbali toka madhehebu mbalimbali yanayowaasa waumini juu ya sifa za viongozi wanaofaa.
 
Nadhani ni sahihi kusema kuwa uchaguzi wa mwaka 2010 ulitawaliwa na udini kwa vile mwaka 2005 hatukuona nyaraka mbalimbali toka madhehebu mbalimbali yanayowaasa waumini juu ya sifa za viongozi wanaofaa.

nyaraka zinatokana na vacuum(ombwe) ya elimu ya uraia,govt yetu haitaki kutoa elimu ya uraia wanaogopa eti watu watelevuka.so si vibaya kama dini zikisiidia kufanya hivo,ila matamko ya akina yakhe yamekaa kichochezi hivi anway wanatumiwa kwa kujua au bila kujua,ni kazi ya CCM na Uhasama wa taifa
 
Toka alipotangazwa kugombea nafasi ya urais kwa ticketi ya CHADEMA, na kipindi chote cha Kampeni mpaka mpaka uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kufanyika, matokeo kutangazwa na mpaka leo hii, ziliibuka shutuma nyingi sana kwamba DR SLAA ametumwa na kanisa kusimika mfumo kiristo katika serikali yetu.

Hali ilifikia mbaya sana, baada ya mpaka Ndugu Kikwete kutoa maelezo katika Bunge letu yaliyomaanisha kwamba watu walipiga kura kwa misingi ya kidini, mwingine ni Naibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, huku akitambua vyema kwamba muelekeo wa kauli kama ya Ndugu Kikwete haukuwa na nia njema kwa Chama chake, nae alipata kutoa kauli ya namna hiyo, na zote zikimaanisha kwamba watu walimpigia kura dr slaa kutokana na ukirsto wake.

Hapa kuna vitu viwili, mtu kupiga kampeni zenye misingi ya udini na watu kupiga kura kwa misingi ya udini.
Kama Taifa hatuhitaji kupata kiongozi ambaye ameingiwa na upumbavu wa kutafuta nafasi ya kutuongoza kwa kupiga kampeni na kutegemea kupata ushindi kwa kutumia udini, na ninaamini kabisa kwamba mpiga kura yeyote makini hawezi kukubaliana na mpumbavu wa namna hiyo.

Swala la mtu kupiga kura kwa misingi ya kidini, hili ni gumu sana kukabiliana nalo, labda mtu wa namna hii aende mbele zaidi na kuanza kumpigia debe mdini wake, hivyo hili ni tatizo la kijamii ambalo tunapaswa kushirikiana kukabiliana nalo,lakini si sawa hata kudogo kudai uchaguzi uligubikwa na udini kwa kuwaangalia wapiga kura,

Ni upumbavu pia mtu kutumia nafasi yake kuwashawishi watu kumpigia kura mgombea fulani, kama ilivyo upumbavu kwa mmliki wa kampuni kuwalazimisha au kuwashawishi wafanyakazi wake kutokana na mahusiano yao kumpigia kura mgombea fulani, vivyo hivyo ni upumbavu kwa kiongozi wa dini kuwaelekeza waamini anaowaongoza kumpigia kura mtu mwenye imani kama yao.

Nachokiona cha Ajabu kwa DR SLAA ni namna alivyokabiliana na changamoto hii, sababu sikupata kumsikia akitoa utetezi wa namna yeyote ile kupinga kwamba hana hurka za kidini, hasa kwamba hategemei kusimamia serikali yetu kwa misingi inayopendelea ukirsto au ukatoriki wale wala kukandamiza wakiristo wa madhehebu mengine au wananchi wenye imani tofauti au wapagani, mara zote aliomba wananchi kutokudanganywa na kuacha kusimamia misingi ya utaifa wetu.

Mtu wa kawaida, angeweza kueleza jinsi mahusiano yake na waislamu yalivyo mazuri na kutoa mifano ya waislamu alioshirikiana nao vizuri akiwa karatu na maeneo mengine, hakufanya hivyo, hakutafuta sympathy, aliendelea kusimamia misingi sahihi ya kupata uongozi katika Taifa letu.

Wonderfully, kumbe amekwishawahi kufanya kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza akakikubari kwa urahisi, kwamba akiwa kiongozi wa kanisa katoriki, huko nyuma, yeye dokta slaa, alisimamia watu wa eneo linaitwa kojani huko zanzibar kupata huduma ya maji ambayo wanayatumia mpaka leo, na anasema anauhakika kwamba, eneo hilo halina mkirsto hata mmoja isipokuwa waislamu tu. but he did it. Ajabu kabisa.

Cha Ajabu kwangu ni kwamba hakuona hata kidogo kama hii ni sababu ya kutafutia kura za waislamu wakati wa kampeni.

Mnyong'e Mny'ongeni, haki yake mpeni.
Wapo watu wanamtukana hapa kila siku, lakini hawajawahi kuchangia hata ujenzi wa Madrasa.

Source: Raia Mwema
 
Mkuu, kwa kichwa hicho cha habari utawaingiza wengi mkenge kama tayari unavyoshuhudia hapo juu walivyokuja mbio wakakuta sio wakaanza kuporomosha matusi (maneno mbofu mbofu).
 
Wadini ni nyie ccm mbona mpo kimya na harakati za waislam ilihali wanavitenda vya wazi vinavyoonyesha udini na mnakaa kimya kwa JK si alikua anapiga kampeni misikitini. Kwa taarifa yako wakristo ndo wengi kuliko waislamu. Mbona rais ni mwislamu acheni propaganda zenu. Dr hana la kujibu kwani hiyo si hoja ya chama wanaoelewa cdm wanajua slaa ni wa style gani. We umeona hilo tu mbona mnasema kapola mke kakimbia upadri hajatetereka ukweli utabaki palepale
 
kuna nabii na mtume (kama anavyojiita mwenyewe) anadai 2015 tutakuwa na rais kijana.wanaompinga wanyooshe kidole.
Acha kuchezea wachungaji na dini ya kikristu,kwa ajili ya mapenzi yako kwa watu fulani yasiyokuwa tija kwa ukristu!
 
Yaani wewe ndiyo bure kabisa,unabishana na meleta mada wakati yeye ameinukuu habari hii kutoka gazeti la raia mwena na hakuongeze maneno yake!
Raia Mpotevu haliwezi kumwita Mh Rais ndugu Kikwete

 
acha kuchezea wachungaji na dini ya kikristu,kwa ajili ya mapenzi yako kwa watu fulani yasiyokuwa tija kwa ukristu!
sasa unachotaka kubisha hapa ni nini tena jamani? He! Basi bwana ngoja mimi nitoke.
 
Hao uliowata hapo hayupo hata mmoja. Namzungumzia Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete,na nadhani ni baba mzazi wa hao vijana.
Bado hatumfahamu labda uwe unamaanisha Mh Rais Dr Jakaya M Kikwete rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ( Chaguo la mungu).

 
Back
Top Bottom