Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Amesema wananchi wanatakiwa kuiachia mahakama ambayo ndio chombo cha haki.

“Katika masuala yaliyoko mahakamani ninaona kwanza kuna sura inatumika, kwenda kule Mahakamani kama sehemu ya siasa kitu ambacho mimi sikubaliani nacho.

“Hivyo sijaenda kwa kuwa ni kitu ambacho sikubaliani nacho, sikubaliani na principal ambayo inatumika, mnaenda kule kisha mnaanza kujipiga picha na mpo kwenye mitandao, hiyo ni siasa, mimi sichezi hizo siasa.

“Mimi nikiamua kumtembelea Mbowe nitaenda nyumbani kwake, sitaki kufanya kitendo cha Mbowe kuwa gerezani kuwa siasa, kama ni kumuombea nitauombea kwa nafsi yangu.

“Niliudhika tangu siku ya kwanza na yale maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema Mbowe siyo gaidi?

“Wanatakiwa kuachia chombo cha haki kitoe maamuzi siyo wananchi.

“Lakini sina chuki na Mbowe wala sina uadui, nimeshakutana na Mbowe mara kadhaa airport, tukakumbatiana, tukabadilishana namba japo hakuna aliyempigia mwenzake,” anasema DK SLAA.

Source: MwanaHalisi

Free.jpg

 
Dr. Slaa ni Moja ya watu wanaochukizwa na wananchi kumtetea Mbowe: amedai anakwazika akisikia watu wanasema Mbowe Siyo Gaidi huku akitaka mahakama iachwe ifanye kazi yake.

Wakati akiumizwa na wapenda haki kusimamia haki ameshindwa kueleza anajisikiaje anaposikia Watu wa chama chake CCM wakisema adharani kwamba Mbowe ni Gaidi kinyume kabisa na status ya kesi mahakamani.

Kwa wanaopenda haki nadhani Dr. Slaa amepuliza kipenga Cha watu kumkera zaidi na zaidi Kwa kutamka Mbowe Siyo Gaidi.
 
Huyu mzee aache wanaoenda waache waende bora kama hawavunji sheria ingekuwa kinyume cha sheria serikali ingepiga marufuku watu wasiende.

Yeye anakereka nini akae kwa kitulia wenye huruma na Mbowe wataenda kumtia moyo kutokana na situation anayopitia kipindi hiki yeye abaki nyumbani na familia yake aponde raha. Eboo!
 
Katibu Mkuu Mstaafu wa CHADEMA, Dkt. Wilbrod Slaa ambaye mpaka sasa pengo lake ndani ya chadema halijazibika ameamua kuwaondolea uvivu wafuasi wa chadema wanaoingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai Mbowe si Gaidi.

Kwenye mahojiano maalum Nguli huyo wa siasa na Mbobezi wa siasa za upinzani ameshangaa Wanachadema wanavyolifanya suala la Mahakama kama suala la kisiasa na hasa wanaposhinikiza majaji kufanya maamuzi ya upande wao.

"Mimi huwa sizunguki niliuzika tangu siku ya kwanza nilipoona maneno kuwa Mbowe si Gaidi wao (chadema) ni kinani mpaka waseme Mbowe si gaidi tena katika suala ambalo liko Mahakamani " Amesema Dkt. Slaa.

Kauli hii nzito ya Dkt. Slaa inastahili kupongezwa na kila mtu anayepigania na kulinda uhuru wa Mahakamana Tanzania na Dunia nzima, ni aibu kwa mtu yeyote kuingilia uhuru wa Mahakama.

Wanasiasa aina ya Dkt. Slaa hasa kutokea upinzani huwa wanakuaga wachache sana kwa sababu ya uwezo wao wa kueleza ukweli, ndiyo maana mpaka sasa bado hajatokea ndani ya chadema kila siku wanafanya kazi ya kubadilisha Makatibu Wakuu.
IMG-20220228-WA0015.jpg


Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom