Ujumbe kwa Dkt. Slaa: Uungwana ni kitendo, jitokeze ukamtembelee Freeman Mbowe

Ss Jr

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
577
450
Ni hivi karibuni ulisikika kwenye vyombo vya habari ukikasirishwa na watu wanaosema "Mbowe siyo Gaidi" ukakasirishwa na wafuasi waliokuwa wanahudhuria Mahakamani wakati kesi ya Mbowe na wenzake ikiendelea, mwisho ukasema swala la Mbowe ni Gaidi au siyo Gaidi iachiwe Mahakama.

Ni takribani siku 10 zimepita baada ya Mbowe kufutiwa kesi hiyo, lakini hatujakusikia ukitoa kauli yoyote baada ya DPP kuifuta kesi husika, ambapo ilidhihirika kwamba Mbowe siyo Gaidi.

Sasa ushauri wangu ni kwamba kama "Wahenga" walivyosema "Uungwana" ni kitendo, basi jitokeze ukamtembelee Mh Mbowe maana kumbuka umetoka naye mbali.

Kwanza: alikuteua kuwa Katibu mkuu wa Chama, hii inaonyesha alikupa heshima kubwa.

Pili: Akiwa Mwenyekiti wa Chama ukateuliwa kuwa Mgombea wa Urais mwaka 2010, hiyo ni heshima kubwa.

Tatu: Pamoja na yote hayo chini ya Mh Mbowe ukapata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hiyo ni heshima kubwa.

Nne: Tafakari kwanza heshima hiyo uliyopewa na Mbowe na Chama kwa ujumla mpaka Jina lako likawa maarufu, ni sahihi wewe kushindwa kwenda kumpa pole juu ya yaliyompata dhidi ya uonevu wa dola kweli?

Kumbuka ukiwa kwenye harakati na Mh Mbowe, vyombo vya dola vikafanya uonevu mbona ulikuwa unalaani? Viongozi au wanachadema wakikamatwa na kupelekwa Mahakamani, na wafuasi wakahudhuria kwenye kesi mbona ulikuwa huwakatazi na kusema tuiachie Mahakama?

Hicho unachokifanya siyo sahihi, ni wakati sasa wa kukutana na Mh Mbowe umpe pole huo ndiyo ubinadamu, kumbuka tangu upate uteuzi wa ubarozi Mh Mbowe hakuwahi kukushambulia kwa maneno yoyote, na kiukweli umaarufu wako umeshuka sana kwa watu tuliokuona kuwa uko mstari wa mbele kuelekea kutupeleka kwenye ukombozi.

Hivyo wewe kukutana na Mbowe itakujengea heshima kubwa sana, jiulize kama Mh Rais alikutana na Mh Mbowe baada ya kutoka gerezani hajafika hata nyumbani, akateta naye, wewe una jambo gani la chuki dhidi ya Mbowe? Kama uliamini Mh Mbowe ni Gaidi, Mahakama imethibitisha siyo Gaidi.

Kaeni Pamoja mtengeneze mstakabali mwema wa Taifa letu. Huu ndiyo ushauri wangu kwako Mh Slaa kwa leo, nikimalizia kwa maneno yale yale
"UUNGWANA NA KITENDO"

Nawasilisha!
 
Utawala wa Dictator yule ambao haukuwa na tofauti kubwa ki - mfano na ule wa J. Stalin, ulikuwa kama chujio.

Moja ya uchafu uliochujwa ni huyu Mzee, mnafiki, mzandiki, mzinzi, wakala wa shetani mnyonya damu za watu

Hapo hapo ni dhaifu kwa Mshumbuzi 💯
 
Mbowe ni gaidi na mahakama ilimkuta na kesi ya kujibu
Ebu thibitsha hayo unayosema, Mahakama kama ilimkuta na kesi ya kujibu kihalali kwa nini ilikubali kuifuta kesi? Kama una chuki na Mh Mbowe weka wazi, basi
 
Tangu nilipojua kuwa dr Slaa alitelekeza upadri, kisha akatelekeza watoto kwa sababu ya penzi la mke wa mtu na akavunja ndoa....niliacha kumwamini kabisa. Anachosema hakiko moyoni mwake kabisa.
 
Ni hivi karibuni ulisikika kwenye vyombo vya habari ukikasirishwa na watu wanaosema "Mbowe siyo Gaidi" ukakasirishwa na wafuasi waliokuwa wanahudhuria Mahakamani wakati kesi ya Mbowe na wenzake ikiendelea, mwisho ukasema swala la Mbowe ni Gaidi au siyo Gaidi iachiwe Mahakama...
Padre Mchonganishi huyo
 
20220313_050744.jpg
 
Back
Top Bottom