Dkt. Philip Mpango akutana na Naibu Waziri Mkuu wa Singapore, Heng Swee Keat

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,198
16 November 2021
Singapore

MCI Photo 3

Naibu waziri mkuu Mh. Heng Swee Keat akiwa na Dr Philip Mpango makamu wa rais wa Tanzania.(Picha kwa hisani ya wizara ya TEHAMA Singapore).

Makamu wa Rais wa Tanzania Dr Philip Mpango yupo nchini Singapore kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi The Bloomberg New Economy Forum unaofanyika kuanzia tarehe 15 mpaka 20 ya mwezi November 2021 2021 New Economy Forum | Bloomberg New Economy

Mh. Dr Philip Mpango alitumia fursa hiyo kukutana na Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Mh. Heng Swee Keat. Katika mazungumzo hayo Waziri Mkuu wa Singapore alimuelezea jinsi nchi hiyo ilivyofaidika kiuchumi kupitia shughuli za bandari kubwa ya Singapore ambayo ndiyo imechangia kwa sehemu kubwa kuifanya nchi hiyo kuwa tajiri.

Bandari ya Singapore inapokea na kuhudumia meli 400 kwa mpigo katika siku moja na hivyo ni mojawapo ya bandari kubwa kibiashara duniani Why is Singapore port so successful? A look at world’s top shipping centre . Asilimia 90(%) ya biashara ya kimataifa mizigo yake yote inatumia huduma za meli na bandari. Tanzania nayo inataka kujipanua na kuwa mshirika mkubwa wa huduma ya meli na bandari kwa ukanda waAfrika ya Mashariki na nchi za maziwa makuu huku pia ujenzi wa bandari kubwa Bagamoyo, utaifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya huduma za bandari duniani.

Naibu Waziri Mkuu wa Singapore ambaye pia ni waziri anayeshughulika kuratibu sera za kiuchumi wa nchi hiyo ameelezea kuwepo nafasi ya kukuza zaidi mashirikiano ya kiuchumi baina ya Singapore na Tanzania pia jinsi ya kufungamanisha uchumi wa nchi hizi mbili zilizo na bahari, mfano kupitia biashara ya bandari.

The fourth annual Bloomberg New Economy Forum will convene on November 16-19, 2021 in Singapore, facilitating face-to-face discussions among world leaders in plenary sessions and intimate breakouts.​


Covid-19 held a mirror to society’s biggest problems, from climate change to inequality, forcing humanity to grapple with their consequences. But there is hope. Even as the pandemic still rages, the success of groundbreaking mRNA vaccines, the acceleration of the digital economy during lockdowns, and a focus on government spending to save lives and improve livelihoods demonstrate that humankind is capable of taking on — and overcoming — great challenges. Breakthroughs are possible. In science and technology, we’ve entered a new age of discovery.

Call on Deputy Prime Minister and Coordinating Minister for Economic Policies Heng Swee Keat by Vice President of the United Republic of Tanzania Dr Philip Mpango​

16 November 2021​

MCI Photo 1

Photo Credit: Ministry of Communications and Information, Singapore

The Vice President of the United Republic of Tanzania, Dr Philip Mpango, called on Deputy Prime Minister and Coordinating Minister for Economic Policies Heng Swee Keat today. Vice President Mpango is on a visit to Singapore from 15 to 20 November 2021 to attend the Bloomberg New Economy Forum.

During the meeting, Deputy Prime Minister Heng and Vice President Mpango reaffirmed the warm relations between Singapore and Tanzania, and discussed recent developments in both countries. They also exchanged views on the potential for further bilateral economic collaboration and the integration of regional economies

READ MORE : 20211116 Tanzania VP Call on DPM Heng
 
Safi sana dr mpango! Piga kazi baba, tunakutegemea. Wale wanaosema mama anaxafiri mwenyewe tu bila kupisha wasaidizi wake wako kimyaàaaaa, km hawauoni huu uzi
 
853e4c31af96b15d19e5cec0d658b09e.png

Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Philip Mpango jana Novemba 16 amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Heng Swee Keat mazungumzo ambayo yamefanyika Shenton way Nchini Singapore ambapo Dr. Mpango amemkaribisha Tanzania na kumueleza jinsi Tanzania imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji pamoja na ufanyaji biashara.

Katika mazungumzo hayo Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Heng Swee Keat amesema nchi yake ilichukua hatua mbalimbali ili kufikia maendeleo ya haraka ikiwemo kutunga sera imara zisizobadilika mara kwa mara pamoja na kuweka sheria zinazolinda biashara na uwekezaji bila kusahau kuwekeza zaidi katika elimu hasa katika kupata Walimu bora na kuweka mkazo katika elimu ya ufundi.

Makamu wa Rais Dr. Mpango yupo nchini Singapore kushiriki mkutano wa jukwaa la majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ) wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo muelekeo mpya wa kiuchumi baada ya athari za covid 19 pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.
 
Hawa jamaa wameshazurura sana huko nje. Shida kubuni hatuwezi, hata copy and paste imetushinda.
 
17 November 2021
Singapore

Two-Speed Global Recovery: the Dangers of a Widening Rich-Poor Gap




Bloomberg's Shery Ahn discusses with H.E. Dr. Philip Isdor Mpango, Vice President of the United Republic of Tanzania, Tharman Shanmugaratnam, Senior Minister, Republic of Singapore, Dan Schulman, President and CEO, PayPal and Elizabeth Rossiello, CEO and Founder, AZA Finance.

An outpouring of stimulus is narrowing wealth inequalities within rich countries, but poorer countries with low vaccination rates are falling further behind -- and may end up on a permanently lower growth trajectory. A generation of kids in the developing world may never fully catch up on missed classes. Now, rising food and energy prices are exacerbating hunger among the world’s most vulnerable populations. Rich countries should adjust their trade policies to support the emerging world. Meanwhile, there’s an urgent need to finance growth in countries left behind. Will multilateral institutions take the lead by offering risk capital? Will private sector lenders follow?

Source : Bloomberg New Economy
 
18 November 2021
Singapore

Dr Philip Mpango azipigia chapuo bandari za Tanzania kushirikia na Singapore



Makamu wa rais wa Tanzania, Mh. Dr Philip Mpango akazia bandari za Tanzania hasa Dar es Salaam iwe kitovu na kituo kikuu cha biashara na shughuli za bandari ukanda wa Afrika.

Kufikia azma hiyo wataalam wa Singapore wameombwa kufika Tanzania na kutumia uzoefu wao wa shughuli za bandari kutambua wapi bandari za Tanzania zinaweza kuongeza ufanisi wake, kuondoa mapungufu na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu wa KiTanzania waliopo ktk bandari zetu za Tanzania na Zanzibar .

Source : Presenter Jimmy


FAHAMU SHUGHULI ZA MAMLAKA YA BANDARI ZA TANZANIA - TPA :

 
View attachment 2013828
Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Philip Mpango jana Novemba 16 amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Heng Swee Keat mazungumzo ambayo yamefanyika Shenton way Nchini Singapore ambapo Dr. Mpango amemkaribisha Tanzania na kumueleza jinsi Tanzania imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji pamoja na ufanyaji biashara.

Katika mazungumzo hayo Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Heng Swee Keat amesema nchi yake ilichukua hatua mbalimbali ili kufikia maendeleo ya haraka ikiwemo kutunga sera imara zisizobadilika mara kwa mara pamoja na kuweka sheria zinazolinda biashara na uwekezaji bila kusahau kuwekeza zaidi katika elimu hasa katika kupata Walimu bora na kuweka mkazo katika elimu ya ufundi.

Makamu wa Rais Dr. Mpango yupo nchini Singapore kushiriki mkutano wa jukwaa la majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ) wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo muelekeo mpya wa kiuchumi baada ya athari za covid 19 pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mpaka mwaka 1964, Singapore ilikuwa maskini sana; tulikuwa kiwango kimoja. Walipoanza kujenga Uchumi wao hawakuwa na mchezo; wala rushwa walikuwa wakipata adhabu kali sana, wachafuzi wa mazingira walikuwa wanchapwa viboko hadharani on the spot. Ukiweka strictness za namna hiyo Tanzania, utasikia malalamiko sana.
 
Back
Top Bottom