Dkt. Mwinyi aondoa kodi ya sukari Zanzibar

Kufunga au kubadili ratiba ya kula toka mchana kwenda usiku

Kuna muda huwa nawaelewa sana wakatoliki na kwaresma yao ,Wao wanasisitiza matendo ya huruma na toba lakini sio kushinda njaa

Hivi kama unakula usiku kucha isipokuwa masaa kadhaa kuna shida?

Kuna wakati tuambiane ukweli,Unaacha kula mchana halafu unakula usiku kucha

Prof Janabi yeye tu anakunywa chai anakaa masaa ishirini na nne ,Wakati wa mfungo atakuwa anawasikitikia sana wanaovimbiwa usiku wa manane
Vimba na upasuke....kwa chuki zako
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo.

Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Jumbi na soko la samaki Malindi mkoa wa Mjini Magharibi leo katika ziara maalumu ya kutembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kuacha kupandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi badala yake kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Mwinyi ameisisitiza Taasisi ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki la Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.

Source - Swahilitimes
si mbaya ni kazi muzuri sana 🐒
 
Kufunga au kubadili ratiba ya kula toka mchana kwenda usiku
Kwa hiyo ulitaka tusile kabisa au?, unataka tufe na njaa nini.
Kufunga Kwa waislamu ni baada ya kuingia alfajiri ya kweli mpaka kuzama kwa jua, baada ya hapo kula unavyotaka na hapo bado kuna waislamu kibao hawafungi, hiyo ndio sheria aliyoweka Mwenyezi Mungu na yeye ndio atatulipa. Funga haijakusudiwa mtu ajikalifishe nafsi ndio maana kuna daku mda mfupi kabla ya kuingia alfajiri lakini pia kuna watu wanakula daku saa nne na hawali tena mpaka kuzama kwa jua.

Lakini kuna nchi wanafunga mpaka masaa 16 (inategemea na tilting of earth) Kwa sababu mchana unakuwa mrefu kuliko usiku, na wengine just saa 8 tu. Lkn kwa ukanda wetu wa Africa mashariki ni saa 12-13 huwa haibadiliki
 
Mkuu unafahamu historia ya unachokiamini au kwa kuwa Baba ni muislam au mkristo ukafuata tu

Hizi dini za uislam na ukristo ni dini za juzi tu ,zile za kihindi ni za zamani zaidi

Watu wanahubiriwa hadithi sema hadithi za mtume

Unafahamu maana ya hadithi?

Hata hawa walokole wakienda vatican kwenye makumbusho yao ndio watajua wanachokiamini kimetoka wapi?

Kumbukumbu za ukristo zipo vatican tena za uthibitisho sio za mchongo
Kumbukumbu za ukristo wanazo orthodox na sio vatican ya warumi,,,shina la kanisa lilianzia mashariki ya kati na kwa ulaya hapo uturuki na ugiriki ambako huko kote kanisa lao la asili ni orthodox na sio kanisa la warumi , wengi wamekalili vatican sababu warumi walisambaza kanisa lao na mengine ya magharibi kupitia ukoloni
 
Back
Top Bottom