William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Wananchi wengi wa Same wanakabiliwa na magonjwa ya saratani
30 Aug 2007
By ITV Habari
Wananchi wengi wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wanakabiliwa na tatizo la magonjwa ya saratani ya matumbo na kichocho kutokana na ukosefu wa maji salama.
hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na mbunge wa Same Mashariki mhe. Anne Kilango Malecela wakati akipokea msaada wa mashine tatu za kusukuma maji kutoka kampuni ya simu za mkononi ya tigo.
Mhe. Anne Malecela amesema katika kukabiliana na tatizo hilo anaendesha kampeni yenye lengo la kuhakikisha kuwa asilimia 65 ya wananchi katika wilaya hiyo wanapata maji salama ifikapo mwaka 2010.
Kwa upande wake meneja masoko wa kampuni ya Tigo bw. Kelvin Twissa amesema kampuni yake itaendelea kutoa mchango wake katika huduma mbali mbali za jamii.