Mbunge Anne Kilango Malecela tunaomba utekeleze ahadi uliyoahidi kipindi cha uchaguzi kukiunganisha kijiji cha Lugulu na umeme wa REA

kunguu

Member
Jan 4, 2024
17
9
Mbunge wa same mashariki anne kilango malecela wakazi wa kijiji cha lugulu chenye vitongoji Vinne ambavyo ni lugulu,masheni, Ramu, na mkondogwe tunaomba utekeleza ahadi yako ulioahidi kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2005, 2020, ,pia mwaka 2020 ulituhakikishia utapambana ili kuhakisha kijiji cha Lugulu kinaunganishwa na umeme WAREA, Wananch wanalalamika sana kuhusu ahadi hii kushindwa kuitekeleza kwa mda mrefu.

Shule ya SECONDARY LUGULU imepatiwa computer ila wanafunzi na waalimu hawawezi kunufaika na msaada huu wa computer kama hakuna umeme, tunaomb ahadi hii itekelezwe ili wanafunzi na waalimu waweze kunufaika na computer hizi

Naibu waziri mkuu na Waziri wanishati Doto Mashaka Biteko, Mkuu Wakoa kilimanjaro ,Mkuu wa wilaya ya same, Meneja WAREA kanda ya kaskani Tunawamba wakazi wa kijiji cha lugulu tupatiwe umeme maana ahadi hii yakuunganishiwa umeme kijiji hiki cha lugulu imekua ya miaka mingi bila utekezaji.

Rais na Mama yetu SAMIA SULUHU HASSANI amewaamini sana nakuwapa zamana kumsaidia ili kutatua kero zinazowakabili wanachi, tunaomba kero hii ya kuunganishwa na umeme WAREA muifanyie kazi ili kuepuka malamiko ya wananchi Wa LUGULU
 
Back
Top Bottom