hali ya maendeleo katika wilaya ya Same imedorora tangu Dr.Mathayo na Anna Kilango wachaguliwe kuwa wabunge wa same magharibi na same mashariki. hali ya ELIMU ni mbaya sana. wilaya ya same imeshika mkia katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na ule wa kidato cha nne. katika suala la KILIMO ule mradi maarufu wa kilimo cha umwagiliaji Ndungu una hali mbaya sana. kuna maradhi ya mpunga yameingia na wakulima hawana msaada wowote toka kwa mbunge wao Anna Kilango. milimani upande wa Dr.Mathayo ukataji MITI na uharibifu wa MISITU ambayo ni vyanzo vya maji umezidi kuongeza. BARABARA ya mkomazi-bendera-ndungu-gonja-kisiwani-same bado ni kero kubwa kwa wananchi.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuisifu wilaya yetu na kutuita "Wachina" wa Tanzania. nina hakika akifufuka leo na kushuhudia uongozi mbovu wa Dr.Mathayo na Anna Kilango, akaona na matokeo ya mitihani ya watoto wetu atageuza kauli yake na kutuita "VILAZA" WA KILIMANJARO.