Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,941
- 6,860
Kiswahili kinaeleweka vizuri kabisa Mkuu, 'uwakilishi' ni neno lisilo tata.
Wasomi kweli mna kazi. Kama linaeleweka vizuri, kigugumizi cha nini? Kwa vile unasema hili ndilo jukumu kubwa la mbunge basi ungeliweka wazi! Ninavyokuelewa mimi niliyekwepa umande ni kuwa kazi ya mbunge ni kukaa bungeni kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake. Yeye ni mtu wa kutimiza hesabu na si kingine.
Ni haki ya mwananchi kumuuliza Mbunge juu ya masuala ya maendeleo kwani ndiyo mwakilishi wao. Kinachokataliwa hapa ni kumuona Mbunge ndiye aliyepaswa kuleta maendeleo au kuona kwamba mhusika namba moja ni Mbunge kwa lugha rahisi kumuona Mbunge ndiye kipaumbele (answerable) badala ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Tanroads (ktk barabara), Mamlaka za Maji safi na maji taka (kwenye miji) nk.
Kumpatia uwajibikaji huu mbunge ni kujenga Taifa linalowategemea wanasiasa badala ya kuwategemea wataalam.
Mhusika namba moja wa matatizo ya wananchi katika jimbo lake yenye utatuzi kitaifa ni mbunge.
Mbunge (na diwani na Rais) ndiyo viongozi pekee walio answerable moja kwa moja kwa mpiga kura. Hawa wasipo-deliver mwananchi anaweza kuonyesha kutoridhika kwake kwa kuwanyima kura zake. Wakiwepo wa kutosha, waheshimiwa kibarua kinaingia mchanga. Ndiyo maana pale huyo unaemwita mtendaji anapoteleza au asipo tekeleza wajibu wake, mwananchi ana haki ya kum-pressurise mbunge wake ili nae awasukume watendaji. Si wananchi wote wana access na hao watendaji wakuu kama aliyokuwa nayo mbunge.
Wabunge wanapewa ofisi katika majimbo yao na usafiri wa kutembelea jimbo lao ili wananchi waweze kuwafikia kiurahisi na yeye mwenyewe kuwafikia wananchi wake kiurahisi.
Kuna mwenzangu alinyimwa viza ya kwenda marekani ambako alialikwa na rafiki yake alie raia wa huko. Alipomwambia rafiki yake, yeye akamwandikia seneta wake, ambae akawasiliana na State Department, viza ikapatikana!
Tofauti na unavyosema, kudai kuwajibika kutoka kwa wabunge wetu ndiko kutakakofanya wataalam wetu wawajibike zaidi.
bangusilo anayohaki ya kuhoji, anayetoa matusi anakosea na amekosa ustaarabu. Bangusilo anakosea kuweka mategemeo pekee kwa Mbunge, anaendeleza dhana ya kujenga Taifa la wanasiasa. Hapo ndo kosa lilipo.
Bangusule hajatukana mtu. Bangusule kama mpiga kura ana haki na wajibu wa kumwandama mbunge wake pale anapoona kuwa amekosea. Mbona anaposifiwa hamlalamiki kuwa hizo sifa za kujenga barabara zingeenda kwa CEO wa Tanroad? Hapana. Anapomsukuma mtendaji akatimiza wajibu wake ana haki ya kusifiwa. Vile vile anapoonekana kushindwa kuwasukumiza watendaji ( na wananchi) ana haki ya kukosolewa. Yote haya ni sehemu ya territory yake.
....kwa upande wangu niko interested na hii mada kwani nimeishi kwa kipindi fulani pale same...zamani hizo.....hata juzi juzi nilikuwa pale wilayani i.e. Same.....trust me kwa juhudi anazofanya yule mama huwezi ku-justfy kum-blame Kilango eti kwa watu wamefeli vile au eti kwa kuwa mashambani watu hawawajibiki ipasavyo............kama ni juhudi hizo za ku-mobilze resources........huyu mama vilevile anazifanya........so whats the fuss here!.........au ndio politics as usual....attack your opponent......and you guys joined the game blindly.......huh!
Mkuu, Ogah. Kama nilivyomjibu Nziku, kukosolewa si attack. Ishu alizozileta Bangusule zina umuhimu kama hizi nyingine ambazo mbunge amefanikiwa. In fact, watu kama Bangusule wanawafanyia favour wabunge hawa kwa ku-highlight pale ambapo anaona pana mapungufu. Mbunge makini, badala ya kukasirika, angeenda kuchungua na kufanyia kazi tuhuma hizi.
Matatizo yetu tuna kaugonjwa ka kupenda. Bangusule amewasema wabunge wawili lakini watu wanamuona Kilango peke yake!
Nchi yetu itafika mbali kama sote tutaanza desturi ya kukubali criticism. Si kila anae ku-criticize ni adui wako. Au ana agenda ya siri. Na sisi wananchi tuanze kudai wale tunaowapa kura zetu wawajibike katika kila nyanja iliyomo katika jimbo letu. Tusiridhike na haya maendeleo ambayo basically ni photo-op kwa ajili ya wabunge wetu. Tuendelee kudai watupe uongozi katika kutatua matatizo yetu yaliyosalia. Ndiyo kazi waliyoiomba. Ndiyo kazi tuliyowapa.
Amandla........