Wakuu poleni na kazi. Poleni na hekaheka za uchaguzi, huku CCM, kule CHADEMA, pale ACT Wazalendo na wengineo wengi kama Lipumba n.k.
Pesa pesa pesa! Mshahara Mshahara Mshahara! Ni topic nzito na zenye kelele sana kwa wafanyakazi hasa watumishi wa umma. Siku zote hulalamika hautoshi, mara mdogo, mara hawajapandishwa madaraja na mengineyo mengi.
Kuna mdau wa uhakika ananitonya kuwa , watumishi wa Serikali wataenda kusimamia na pia kupiga kura wakiwa wametuna kwenye wallet zao. Mshahara mnono unakuja siku mbili hizi sijazo.
Mshahara utapanda, madaraja yataongezwa na malimbilizo yatadumbukizwa kwenye accounts zao za mishahara.
Wakae chonjo.
Asante Mh. Rais.