Ngwanashigi Gagaga
JF-Expert Member
- Mar 10, 2017
- 430
- 300
JPM, ni mkweli anaaminika. Kajenga msingi wa uchumi, najua atatuongezea mshahara.Mgombeawa Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amesema sasa ni wakati wa kujali maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania.
Amesema kwa miaka mitano aliyoongoza ameweza kufanya nchi ifike uchumi wa kati wa chini na hivyo kwa miaka mitano inayofuata ataanza kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Amesema hauwezi kuongeza mishahara wakati hauna hela ya kuongeza mishahara. Aidha amesema hao wanasema kuhusu kuongeza mishahara hawajawahi kutawala.
Amesema wengine vyama vyao wameshindwa hata kujenga ofisi za vyama vyao. Amesema kuzungumza ni rahisi kuliko vitendo.