Dkt. Kipilimba, sasa yatosha!

Dkt. Kipilimba, sasa yatosha!

Hilo deni la Steyn. Hata kwenye ripoti ya CAG ilikuwemo.

Kwa hiyo ni "ubabe na kiburi" ndicho kinachoimaliza serikali hii ya awamu ya tano
Na awamu nyingine walinipa awamu hii ndiyo ilitia ngumu
 
TISS ya leo imejaa vijana wa UVCCM, wasiojua lolote kuhusu intelligence wala miiko yake. Idara hii imegeuzwa kuwa ya kisiasa ili CCM itimize ndoto zake za alinacha za kutawala milele. Inashangaza sana, yaani Idara haikuweza hata kuzuia maandamano ya kuharibu Diplomasia yetu na SA.

Watumishi wa Idara hii wanatakiwa wawe wafia nchi (wazalendo kweli kweli) siyo wafia CCM au CHADEMA.

CCM itakufa, CHADEMA itakufa, lakiniTanzania ipo tu!

Mengine yote unamuonea tu Mkurugenzi.
Hoja hii inamhusu Mwenyekiti wa CCM- Mstari wa mwisho. Tanzania itaendelea kuwapo hata bila CCM,CDM nk.
 
Dah umeandika uzi wa kutoka moyoni mwangu kabisa.

Sio siri TISS wanatuangusha sana watanzania nimewai kueleza huko nyuma kuwa TISS ipo kisiasa zaidi kuliko kiuchumi.

Kama Magufuli anataka kweli nchi ya viwanda wauangalie mfumo wote wa hiyo I Dara, ila kama anatamani yeye au CCM yake mpya kutawala milele waiache ilivyo, lla kwa maoni yangu TISS ifumuliwe na kuundwa upya.
Tiss ikifumuliwa Magufuli and his ccm out, hili haliwezi kufanyika kamwe.
 
Kwa mara ya tatu tena nakuandikia Mzee wangu Dr Modestus Kipilimba, mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa, TISS.

Natamani sana, Rais Magufuli awe wa kwanza kusoma hii mada kabla yako.

Nimeshindwa kuendelea na kazi niliyokuwa naifanya usiku huu kwenye Computer, moyo wangu umekosa amani kabisa hadi niandike hii mada.

Dr. Kipilimba, unadhani bado unastahili kuongoza Idara nyeti na muhimu Kama hii ya TISS?

Kwanini mikononi mwako serikali ya awamu ya tano inadhalilika sana kimataifa?

Kwanini Idara yako imeruhusu uwepo wa watu Kama Musiba wanaokashifu viongozi wakubwa hadharani?

Sikufundishi kazi, ila nashangaa kwanini hujui kuwa idara kama TISS ndo Roho kamili ya Tanzania.

Kifo cha TISS ni kifo cha Tanzania, kwanini hujifunzi magumashi ya CIA, MI5, Mossad na mashirika mengineyo kama TISS?

Ninaposema magumashi nadhani umeelewa vizuri kabisa, maana nikielezea itahitaji kitabu.

Uimara wa TISS ndo Uimara wa Tanzania, na udhaifu wa TISS ndo udhaifu wa Tanzania.

Tunajua ya kwamba dawa ya Deni ni kulipa, lakini ilikuwaje TISS ikashindwa kubaini kuwa Steyn kafungua shauri mahakamani dhidi ya Tanzania kudai mali yoyote ya nchi ikamatwe?

TISS ingeitaarifu serikali basi, ndege isingeenda SA, na hivyo wangetafuta namna nyingine ya ku-solve tatizo.

Ni aibu kubwa mno nchi kudaiwa na raia mmoja Halafu mali ya nchi kukamatwa kwa Deni nje ya nchi, hii fedheha kubwa.

TISS mngeweza kuepusha hii fedheha. Kama TISS, ilishindwa kubaini njama za kutaifisha mali ya nchi, je itaweza kujua nini kinapangwa Somalia na Alshabab kwa mfano juu ya nchi?

Dr Kipilimba, TISS chini yako ni dhaifu mno, nakushauri u resign tu. TISS chini ya Dr Hansy Kitine na hayati Imran Kombe ilikuwa imara kupindukia.

Nakumbuka Tukio moja (siwezi kulitaja) nilikuja kushtuka mission accomplished muda mrefu kumbe yule jamaa alikuwa TISS na akapotea kama jini.

TISS ya leo imejaa vijana wa UVCCM, wasiojua lolote kuhusu intelligence wala miiko yake. Idara hii imegeuzwa kuwa ya kisiasa ili CCM itimize ndoto zake za alinacha za kutawala milele. Inashangaza sana, yaani Idara haikuweza hata kuzuia maandamano ya kuharibu Diplomasia yetu na SA.

Watumishi wa Idara hii wanatakiwa wawe wafia nchi (wazalendo kweli kweli) siyo wafia CCM au CHADEMA.

CCM itakufa, CHADEMA itakufa, lakiniTanzania ipo tu!

Umeandika na Kuelezea vizuri mno Kiongozi na nitashangaa kama siyo kusikitika wasipokuelewa na Wahusika kufanyia Kazi. Hauko mbali na ukweli kuwa TISS sasa kuna Mapungufu makubwa hasa ya Kiutendaji japo kuna lawama zingine za chini chini ambazo nahisi nazo zinaweza kuwa ni sehemu ya Utendaji wao usioridhisha wa sasa kwamba huyo Boss Wao Mkuu hakuandaliwa kuwa hapo, hana Uwezo thabiri wa kuwa DG na kwamba wale ambao Idara iliwaandaa Amiri Jeshi Mkuu alipopelekewa Majina yao aliwadharau akidhani kuwa walikuwa ni Watu wa Mstaafu ( aliyemwachia Kijiti ) huku wengine akiwachukia kwakuwa alipewa taarifa za Kiumbea kuwa hawakuwa upande wake katika Harakati zake za kuwa hapo alipo sasa na kwamba walikuwa ' Loyal ' kwa Mzee Mamvi.

Hoja yako kuwa Vijana wa TISS wa sasa wengi Wao ni kutoka ndani ya CCM naweza kukubaliana nalo kwa 95% kwani wapo ambao wanajulikana kuwa walikuwa ni Makada Watiifu wa hicho Chama na sasa nao ni sehemu ya TISS na walipo wa hovyo hovyo hata wakikaa Vijiweni hawajui Kujificha na hupenda ama Kuropoka na Kujisifia kitu ambacho kwa hiyo Tasnia ni HATARI mno.

Misingi Mikuu ya Kuajiri Vijana ambao ulikuwepo nadhani tangia awamu ya Kwanza hadi ya Tatu imekiukwa kabisa na kwa taarifa yako tu Kiongozi TISS ilianza Kuharibika katika Awamu ya Pili na ya Mwisho ya Kiongozi wa Awamu ya Nne na yanayoendelea sasa ( katika Awamu hii ya Tano ) ni muendelezo wake sema tu nao umekuwa ni Mtindo wake.

Bado sijalithibitisha hili ( bado nalifanyia utafiti wangu binafsi ) ila nasikia kuwa TISS ya sasa ukiachilia mbali ili uchukuliwe huko yakupasa Kwanza uwe ni mwana CCM kuna hii kwamba kwa sasa ili iwe rahisi kwa Wewe Kuajiriwa huko inabidi pia uwe unatokea Mikoa ya Kanda ya Ziwa au uwe karibu ya Kiongozi Mmoja wa Mkoa ambaye kwa sasa anatajwa kuwa ndiyo Mratibu Mkuu wa Kuwaingiza Watu huko TISS ambaye nimedokezwa kuwa huko nyuma alikuwa anaingia Makao Makuu yao anavyotaka ila baadae alidhibitiwa baada ya ' Swahiba ' wake ' Robie ' kuhamishiwa Mkoa Mmoja unaolima sana Tumbaku nchini Tanzania ambako pia alishushwa Cheo kutoka kile Kikubwa tu alichokuwa nacho TISS.

Kamwe usitegemee kuwa na TISS imara kama hizo za akina CIA, KGB / FSB au MOSSAD au MI5 na MI6 kama wanaoajiriwa wengi wao ni wale ambao Kwanza ni ' Failures ' katika ngazi za Kitaaluma, hawana Akili ( hasa za Kuzaliwa na siyo zile za Kufundishwa ) na wale ambao wameingizwa huko kwa Mgongo wa ama Baba, Mama, Mjomba, Hawara ( Ngono ) na hata kwa Kutoa Rushwa na ambao kwa bahati mbaya kwa sasa ndiyo wamejazana huko na ndiyo wanaichafua sana TISS Kiutendaji.

Nami naomba niishie tu hapa Kiongozi ila nimefurahi mno jinsi ulivyolileta na kuliezea hili vizuri kabisa. Hongera na Ubarikiwe.
 
Usichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?

Una uhakika gani kuwa TISS hawakishauri lolote kabla ya haya kutokea?

Tanzania tuna bahati ya kuwa taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.

Usiku mwema!!

Are you serious? Tungekuwa na taasisi imara sasa hivi zingekuwa zishaanza kumchunguza Ndugai kwa kufanya ufisadi wa bilioni 27 kwa matibabu ya miezi sita, yaani matumizi ya 153M per day. Mambo mengine fungeni midomo tu.
 
Sio vizuri kumtisha mtu mkuu sasa kama walijua hilo kwa nini wasingeishauri serikali ili ndege isiende mda mwingine unapokataa kuambiwa ukweli nako ni shida
Huyo ni mshamba tu mkuu, Hana la kunifanya, walivyoweza kumpata Ben Saanane wanadhani kila mtu watampata
 
Kwa kweli hali inayoendelea hapa nchini na duniani kote kwa ujumla kuhusiana na hii taasisi, Inasikitisha Sana kupita kiasi, tena inakatisha tamaa kwa kweli.

Wao badala ya kujikita zaidi na kuelekeza nguvu zaidi kwenye ECONOMIC ESPIONAGE wamebaki kuhangaika na ku-deal na vijitu vidogo kidogo vinavyokosoa Serikali, kutwa kucha wanashinda kwenye Facebook, twitter, JF, WhatsApp, n.k. kuangalia nani anaikosoa Serikali jambo ambalo hakuna tija yoyote kwa maslahi mapama ya umma.

Tena siku hizi nasikia wanakataa kulipa hata parking, wakidaiwa wanaanza yale maneno ya shombo - unanijua mi nani?? Lack of professionalism to an alarming extent.
 
Usichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?

Una uhakika gani kuwa TISS hawakishauri lolote kabla ya haya kutokea?

Tanzania tuna bahati ya kuwa taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.

Usiku mwema!!
Uimara gani wa taasisi wakati tayari tumeathirika kidiplomasia dunia nzima?
 
Usichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?

Una uhakika gani kuwa TISS hawakishauri lolote kabla ya haya kutokea?

Tanzania tuna bahati ya kuwa taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.

Usiku mwema!!
Gutter nonsense, read btwn the lines ndio ukimbilie key board!
 
Back
Top Bottom