Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,568
Mawazo ya kimasikini haya.Ndo uko sawa kabisa JKT inapaswa kurudi kisawasawa na mimi napendekeza vijana wakae kambini kwa miaka miwili.
Hii wanafanya Israeli na Korea Kusini na baadhi ya nchi zingine.
Hii itasaidia watu kushika moyo na kuonyesha wanaipenda nchi yao na wako tayari kuitumikia "no matter what".
Hata kama kuna kiongozi ambae na kasoro zake lakini linapokuja suala la ndege kuzuiwa nchi nyingine khasa ndege mpya watanzania wanaungana pamoja kutafakari juu ya mstakabali wa mali hiyo ya taifa.
Marekani pamoja na Donald Trump kufanya anayofanya lakini wakaikung'uta Syria kwa mabomu na sasa wanaishughulikia Iran na Korea Kaskazini, hiyo yote ni kwa "maslahi ya taifa" hilo.
Unafahamu hata nchi zilizoendelea likija jambo la "kwa maslahi ya taifa" wanageuka na kuunga mkono, hayo utaona kwenye televisheni, radio na magazaeti.
Masuala kama ya ugaidi na kutishia usalama wa mataifa yao wanaweza wakayaongelea kwa siku kadhaa masaa 24 na ukijaribu kubadilisha chennels habari ni hizohizo mpaka kieleweke mbele ya wananchi.
Viongozi mbalimbali, wasomi na watu wengine wa kada mbalimbali kwenye jamii wataitwa kwa interviews.
Sisi Tanzania kuna kitu kimeharibika ndani ya miaka 20 ilopita na tunapaswa kujitafakari na kujifunza uzalendo na kulinda maslahi ya taifa.
Vijana wasitafute maisha wakakae jeshini kisa uzalendo?
Upumbavu wa hali ya juu.