yusuphfrancis
JF-Expert Member
- Oct 26, 2016
- 433
- 361
Ni kweli mkuuUsichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?
Una uhakika gani kuwa TISS hawakushauri lolote kabla ya haya kutokea?
Tanzania tuna bahati ya kuwa na taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.
Usiku mwema!!
Mimi naamini TISS wako vizuri kwenye operation za kupambana na raia wanaokosoa serikali hasa hasa wanasiasa ndani ya nchi basi na siyo nje ya nchi, tofauti na hapo, mkuu tutadanganyana.
Tuwe wakweli tu mkuu,
Raia wengi wanaamini kuwa usalama wa taifa ni usalama wa raia, ardhi na mipaka ya nchi yetu akini nionavyo mimi tafsiri hii si sahihi kama inavyotafsiriwa na Tiss ambapo wao usalama wa taifa huenda wanatafsiri kuwa ni usalama wa Rais na serikali yake!
Nimefikiria hivyo kutokana na mwenendo wa matendo yanayofanywa na baadhi ya viongozi kama RC Chalamila, Bashite na wengine wengi ambao ukiwafuatilia kwa karibu utabaini kuwa hotuba zao nyingi zinalenga kuvunja amani ya nchi, lakini Tiss wapo hawachukui hatua yoyote ile dhidi yao kwa kuwa ni viongozi serikalini lakin vitendo hivyo vingefanywa na wengine ambao siyo viongozi wa serikali ni dhahiri wangeshughurikiwa mapema sana.