Dkt. Kipilimba, sasa yatosha!

Dkt. Kipilimba, sasa yatosha!

Ungeendelea na hiyo kazi yako ya kuchafua serikali na taasisi zake. Mkurugenzi wa TISS atakuwa mtu wa mwisho kabisa kupokea lawama na kuwajibika, in fact Dr. Kipilimba anafanya kazi kutokana na mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na uongozi wa awamu ya tano.
Sawa kabisa!
 
Kwa kweli hali inayoendelea hapa nchini na duniani kote kwa ujumla kuhusiana na hii taasisi, Inasikitisha Sana kupita kiasi, tena inakatisha tamaa kwa kweli.

Wao badala ya kujikita zaidi na kuelekeza nguvu zaidi kwenye ECONOMIC ESPIONAGE wamebaki kuhangaika na ku-deal na vijitu vidogo kidogo vinavyokosoa Serikali, kutwa kucha wanashinda kwenye Facebook, twitter, JF, WhatsApp, n.k. kuangalia nani anaikosoa Serikali jambo ambalo hakuna tija yoyote kwa maslahi mapama ya umma.
Kwa jinsi wapenda vya dezo walivyojipanga kama Idara hii isingekuwa makini tungesikia mengine saizi. Usilolijua ni kama usiku wa giza! Ingekuwa ni disaster hilo ndilo ulijue kuanzia leo.
 
Nyote wawili mnazungumzia kitu kimoja.

Kwanini TISS 'inadeploy resources' kuwafikia Wapinzani wa CCM na wanaomsema JPM wakati inashindwa 'kudeploy resources' kulinda maslahi ya Taifa mpaka ndege inakamatwa Afrika Kusini?

Au unasema TISS walijua wakakaa kimya?
TISS ni ya kuishukuru isingefanya kazi kwa uadilifu tungekwishamwaga damu kwa ulafi wa wachache!
 
Hivi kuna TISS ilikuwa mbovu kushinda ya awamu iliyopita?? wizi wote huo kuanzia kagoda mpaka escrow..tena hapa hapa ndani, Dr. Kipilimba amerithi TISS mbovu huwezi mlaumu kwa yanayotokea sasa.
Definitely true.
 
Ha ha ha
Tiss kwa sasa kazi yao kubwa ni kumaliza upinzani jambo ambalo ni ndoto hayo masuala ya kimataifa wanakwenda kuhudhuria semina tu
Ha ha ha Semina za wapi Ngurudoto au? Mtaisoma namba! Msidhani wananchi watamchukia Rais kwa ndege kushikwa wakati ninyi ndio mmeshika usukani!
 
Wewe umeonesha uafrika wapo kwa comment yako.

TISS iko weak, sio tu ktk sakata hili la ndege ila mengi mengi mno, mauaji, vitisho, maadili n.k

Kuna kipindi Lissu alimwambia mpka Kipilimba kwamba yeye anafatiliwa na vijana wa TISS, Lissu akaja kupigwa risasi kweli, mpaka leo kipo wapi kinachoendelea?

Suala la ndege limetuvua nguo, kuonesha ujuha wetu tumeenda kuandamana ubalozini.
Hako kandege kamoja tu kanakubabaisha! Eti imetuvua nguo, kwa hiyo mafy over yooote. vivukooo vyoote . Mabarabara yooute mlidhani yataharibiwa na kandege! Pole yako sana. Hebu kazana kujikwamua kimaisha kijana!
 
Hapo ndipo walipokosea.

Ingawa makuruta huchukuliwa tangu vyuoni, makazini na sehemu zingine ulizotaja, bado ile misingi ya kumpata mtu sahihi ilianza kuvunjwa.

Tulianza kuiga wenzetu waloendelea ambao hata kama wanachagua watu kutoka vyuoni lakini wale watu wanakuwa wamepita mafunzo maalum kama kile cha Mbweni.

Tatizo ni aina ya mtu unaemchagua ambapo ukianza kuingiza undugu na kujuana ndipo matatizo yanaanza hapo.

Unafahamu, hata ukipata kijana aleiva kisawasawa na ukamtuma afanye espionage nchi fulani na akatoa taarifa za kutaka kuizuia ndege kule Jo'burg, ujue unao vijana makini, lakini tumeshindwa hata kuvuna vijana hata wale ambao wamezamia tu kule nakuwapa mafunzo makini watusaidie kwenye majangq kama hili la ndege, wategemea nini zaidi?

Kwenye masuala ya kulinda maslahi ya taifa haijalishi ni mtu au watu fulani tuu ndo wateule wachache wewe waangalia masuala haya kwa upana wake.

Wenzetu wengine siku hizi wameenda mbali sana wanaweza kuanza kukufuatilia hata unapokuwa ukitumia Xbox au PS na wakawa wanakupa mitihani bila wewe kujua wafanya majaribio ya kuonakama wafaa.

Mara tu waona barua inakwambia unahitajika mahala kwa uasili (wanakwambia labda umepata kazi nzuri tu) ambapo ukifika kule waambiwa kazi yako halisi na iwe siri na hata familia iisijulishwe.

Ila serikali hii sasa inednelea kuifumia TISS ambayo ilioza sana na kuwa nyuma kwa kila kitu.
Hebu waambieni hao walio against Government kwa sababu tu ya kubwanwa maslahi wajitafakari. Uzalendo kwanza. Actually JKT ingerudi tena ianzie form 4 maana kuna kizazi kwa kweli kinatishia amani ya nchi!
 
Ni kweli hili linawezekana maana msafara wa mamba kenge pia wamo.
Si unajua binadamu tulivyo hasa sisi ambao tunaishi kwa mazoea ngumu kuacha ghafla mazoea yetu ya kubebana.
Ila sio mbaya maana wamechomekwa kwenye taasisi mbalimbali as informers, so na imani wanafanya kazi nzuri.
 
Unauhakika gani kipilimba bado ni ceo wa tiss? Je unaweza kuamin kama ameshatenguliwa?
Jioni hii n njema.
 
Mna hasira na nini kubaniwa ulaji. ACtually kama sio TISS tungekuwa tunaogelea damu sasa hivi! Nyie wenywe mlete matatizo halafu muilaumu TISS.
Hiyo damu imwagike Mara ngapi? Hawa watu ambao wamekuwa wakitekwa, kupotezwa na wengine kuuawa na maiti zao kutupwa baharini, mitoni, ziwani, maporini e.g huko Mkuranga n.k., je hiyo siyo damu iliyomwagika? Au inatakiwa wafe watu wa aina gani hapa nchini ili ijulikane kuwa damu imemwagika?
 
Usichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?

Una uhakika gani kuwa TISS hawakishauri lolote kabla ya haya kutokea?

Tanzania tuna bahati ya kuwa taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.

Usiku mwema!!
Mkuu kama hao TISS wangeweza ku deploy resources na kumfikia usiku huohuo mbona hao TISS wameshindwa kuwakamata waliompiga risasi lissu,waliomteka ben saa nane na azory gwanda???
 
Hebu waambieni hao walio against Government kwa sababu tu ya kubwanwa maslahi wajitafakari. Uzalendo kwanza. Actually JKT ingerudi tena ianzie form 4 maana kuna kizazi kwa kweli kinatishia amani ya nchi!

Ndo uko sawa kabisa JKT inapaswa kurudi kisawasawa na mimi napendekeza vijana wakae kambini kwa miaka miwili.

Hii wanafanya Israeli na Korea Kusini na baadhi ya nchi zingine.

Hii itasaidia watu kushika moyo na kuonyesha wanaipenda nchi yao na wako tayari kuitumikia "no matter what".

Hata kama kuna kiongozi ambae na kasoro zake lakini linapokuja suala la ndege kuzuiwa nchi nyingine khasa ndege mpya watanzania wanaungana pamoja kutafakari juu ya mstakabali wa mali hiyo ya taifa.

Marekani pamoja na Donald Trump kufanya anayofanya lakini wakaikung'uta Syria kwa mabomu na sasa wanaishughulikia Iran na Korea Kaskazini, hiyo yote ni kwa "maslahi ya taifa" hilo.

Unafahamu hata nchi zilizoendelea likija jambo la "kwa maslahi ya taifa" wanageuka na kuunga mkono, hayo utaona kwenye televisheni, radio na magazaeti.

Masuala kama ya ugaidi na kutishia usalama wa mataifa yao wanaweza wakayaongelea kwa siku kadhaa masaa 24 na ukijaribu kubadilisha chennels habari ni hizohizo mpaka kieleweke mbele ya wananchi.

Viongozi mbalimbali, wasomi na watu wengine wa kada mbalimbali kwenye jamii wataitwa kwa interviews.

Sisi Tanzania kuna kitu kimeharibika ndani ya miaka 20 ilopita na tunapaswa kujitafakari na kujifunza uzalendo na kulinda maslahi ya taifa.
 
Dharau ilitoka kwa Jiwe ukite Ramaphosa alimhakikishia hiyo hali haitatokea
Jiwe ana dharau sana na ndo maana hata acacia wametushinda kwenye majadiliano
Hakuna ushahidi wowote kwamba waliongelea hili, tuache speculations.

Ramaphosa kumhakikishia hilo litatokea ni ujinga wa hali ya juu, kwa sababu hana mamlaka juu ya mahakama. I don't think the guy is that dumb.
 
Idara hii ipo, na hailali kucha ipo kazini. Tofauti ni malengo yamebadirika, kuhakikisha uimara wa ccm na maslahi mapana ya viongozi wake. Maslahi ya kitaifa si jukumu lao tena. Hata jirani zao TCCB, tofauti hakuna, kama mapacha vile.
They are busy for NOTHING not for SOMETHING ADVANTAGEOUS for the general public!!!
 
Kibaya zaidi wanadhani wanajua recruitment and grooming ya watu wa idara inafanyika vipi.

Huenda wamekaririshwa na watu waliopitia idara zamani. Kwani hawaoni mabadiliko ya recruitment process hata idara za kawaida za serikali haipo kama zamani?

Kama kuajiri mtu wa kada za kawaida kumeboreshwa sasa serikali au idara ya usalama wa taifa itakuwa wazembe kiasi gani kutofanya mabadiliko na kuendelea kutumia njia za zamani zisizo bora na kisasa?

Ina maana huko idarani na serikali kuna watu wasiojua kitu au hawana akili na yeye huku mtaani ndio ana akili nyingi sana kuliko wote waliopo serikalini?

Anataka waje hapa kutoa ufafanuzi jinsi wanavyo ajiri, walivyo chukua hatua mbalimbali kwenye matukio tofauti? Sasa hiyo itakuwa idara ya usalama wa taifa au kitengo cha uenezi cha chama au cha serikali?!!!

Tuwaache hawa watu wafanye kazi zao na tushukuru kwa kazi zao tunapata muda wa kutafuta pesa ya bundle na kuwatukana mitandaoni.
Tatizo lenu mna uwezo mdogo mno wa kufikiria ,unajuaje Kama na mimi nimeiva ktk masuala ya intelligence?
Halafu ni wapi nimetukana zaidi ya kushauri?
TISS haiko imara ,ni kichaka cha CCM kufanya upumbavu wao.
Tungekuwa na TISS imara, hata uchumi ungekuwa imara, kwa sababu kazi za Taasisi Kama TISS ni kuhujumu mataifa mengine kwa maslahi ya nchi na siyo kuhujumu vyama vya siasa.
Ningeandika mazito ila namwonea huruma Melo watamtesa bure, hapa mbona nimeshauri tu, nikiweka nondo nzito hadi ikulu watapoteana.
Wewe kula ukalale huna unalojua, Tuachie sisi wanaume tuikosoe serikali.
 
Back
Top Bottom