TANZIA Dkt. Isaac Ndodi afariki dunia

TANZIA Dkt. Isaac Ndodi afariki dunia

Mwenyenzi Mungu awafariji wafiwa na wote walioguswa na msiba

Inna Lillah wa Inna Illah Rajiun
 
Katika mafundisho yake ya ndoa na malezi aliwahi kusema, Popote panapotafutwa haki lazima kuwe na vita.

Ukiona kwenye ndoa mke anasema kwa kuwa yeye ni mfanyakazi na mume ni mfanyakazi, wote wana digrii sawa, mshahara sawa nk, ana haki sawa na mume hivyo wote wapike, wafue nk, hapo tayari kuna vita.

Ukiona chama cha siasa kinasema kina haki fulani na kinaitaka, hapo kuna vita dhidi ya chama tawala. Kwa hiyo ukipambana kupata haki ujiandae na vita
 
Uingereza, taifa lenye wasomi wengi na linaloamini kuwa ndio wastaarabu zaidi duniani mpaka leo wanatawaliwa na familia moja, yaani mtoto anayezaliwa leo kwa kina King Charles tayari ana maisha na ni mtawala. Husikii waingereza wakilalamika kuwa kwa nini familia moja iwatawale milele? Siku wakiamka kudai haki ya kubadilishana, hapo tayari itaibuka vita.

RIP Dr. Isaac Ndodi, mpambanaji kutoka Songea Bombii Numbi
 
1. Aliwadis sana wenye vitambi, alipopata pesa, nae akafuga kitambi
2. Aliwadis sana Wala ugali wa sembe, akidai tunazidiwa akili na panya.

Nakumbuka Kwa hayo
 
Kumbe alikuja nenepa hivi?
Mara ya mwisho kumuona ni 2008.

Ajaliwe pumziko jema aiseee, aliweza
Kutushika na vipindi vyake vile,hadi mchele tulikua hautoshi na tuliacha kupikia sufuria na kupikia vyungu!

Achilia mbali kula malimali mia mpka moja kisha moja mpaka mia!!!

Kwa mujibu wa taarifa za awali Dkt Ndodi hakuwa Mgonjwa mapema leo alipata changamoto ya ya kiafya na kudondoka chini ghafla na hadi anafikishwa hospital kwa matibabu tayari alikuwa amefariki dunia

Taarifa zinaeleza msiba uko Malamba Mawili

Kwaya ya kurasini kwa tumepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mshiriki mwenzetu Dr Ndodi Mungu akawe faraja kwa familia pamoja na sote tulioguswa na msiba huu….Vita umevipiga na mwendo umeumaliza 😭😭😭

View attachment 3718477
Aliwafanya wabongo wajisikie fahari kula dona badala ya sembe, sema hakutoa tahadhari kwa Wala dona kwamba mahindi yanawekwa dawa ya kuhifadhia ambayo ni sumu na wafanyabiashara wanasaga na kupaki unga bila kuyaosha kwanza.
 
Back
Top Bottom