TANZIA Mchungaji Dkt. Charles Sokile amefariki dunia

TANZIA Mchungaji Dkt. Charles Sokile amefariki dunia

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Wakuu, nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Dkt. Charles Sokile, kilichotangazwa na Mchungaji Kiongozi wa CCC Upanga, Dkt. Lucas Shalua.

1793599168865.png

Dkt. Sokile alikuwa msomi na mtaalamu mkubwa aliyefanya kazi kwenye masuala ya utawala bora, uwajibikaji na maendeleo.

Lakini kwa waliomfahamu, hakuwa mtu wa kujivuna kwa elimu na nafasi yake.

Nakumbuka wakati nikijiunga UDSM mwaka 2006 pale utawala kwa jamaa wanaouza viji booklet nilinunua kakitabu fulani kanaitwa campus living wakati nimetoka zangu kwetu mpitimbi huko na ndio mara ya kwanza kufika Dar es Salaam (asante chuo), kitabu kilinielekeza vitu vingi kabla sijaenda kuishi mabibo hostel wakati huo chuo ilikuwa chuo kweli baadae nikafanikiwa kumuona huyu mzee kwenye kozi za development.

Alikuwa mtu mwema sana, mnyenyekevu na mwenye moyo wa kuwajali wengine hata wanafunzi wake. Na mpaka umauti unamkuta alikuwa mchungaji msaidizi hapo Upanga CCC.

Ni uchungu kumpoteza mtu wa aina hii. Poleni sana familia, ndugu, marafiki na wote mlioguswa na msiba huu.

Pumzika kwa amani Dkt. Charles Sokile.

Wema wako na mchango wako hasa semina zako kwa vijana vitaendelea kukumbukwa.

WITO: Naiomba Serikali iangalie kwa upya usimamizi wa bodaboda na bajaji iwe marufuku kubwa vijana kuendesha hivi vyombo bila kuwa na leseni na mafunzo ya kutosha ya usalama barabarani. Unakuta jitu kwenye zebra limetungua na kipikipiki chake halijali kama kuna watu wanavuka, halijavaa helmet, linakimbia hovyo na limevaa malapa, Rwanda tu hapo huezi ona huu ujinga, tutekeleze tusiweke siasa kwenye usalama barabarani.

1793599425926.png

MODS chapisheni uzi, sio kuufuta. Verify the information & publish.
 
Bodaboda wameingiaje tena kwenye Tanzia ya Dr? Ndiyo chanzo cha kifo chake?
 
Back
Top Bottom