Dr Ulimboka ataongea muda ukifika.
Ingawa hii picha ya kihindi inachelewa kuanza, lakini muda wake ukifika picha ya kihindi itaanza tusiwe na haraka.
Tuendelee kumuombea Doctor afya yake iwe nzuri, na atakapoongea aseme ukweli mtupuuuu.
Mwanahalisi nao waliujuwa ukweli 90%, ndiyo maana wakafungiwa, habari walizotoa zilikuwa na details za kutoshaaa, walifanya kazi nzuri sanaaaa, ambayo serikali haikutegemea kutoka kwa wandishi wetu wa Tanzania na pia hawakuogopa kutoa details.
Binafsi nawaamini sana Mwanahalisi kwa hili jambo la Dr Ulimboka.
Doctor Ulimboka tulizana, upone vizuri halafu utakuja siku moja kutuhabarisha, ila ni lazima uwe muangalifu sana, maana serikali this time wakikupata watakuuwa hawatafanya kosa tena kama walilolifanya, watakuchoma moto au watakupiga risasi huo ni ushauri wangu kwa Doctor Ulimboka.
Kwa bahati mbaya sana serikali za kiafrika ni za kishenziiiiiiiiiiiiii sanaaaa, siyo hapa Tanzania, ni Afrika nzima mambo na michezo ni hii hii tuuu, serikali za kiafrika hazitaki kukosolewa wala kuelekezwa.
Nawatakia siku njema