Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

WEWE MUNGU NA HARDSHIP ALLOWANCE WAPI NA WAPI?..unatumia mistari ya mungu kuhalalisha mauaji ya wagonjwa wasio na hatia?

Hardship allowance tena ndugu mbona sijaongea Hilo? Mama au mwanamke yo yote anapoona mwanae ameumia anasikia uchungu. Nilidhani umenielewa Kumbe umehamia kwingine. Anyway jambo hili litamalizwa na maombi kwa wote wenye kuitakia mema Tanzania. Mungu ni mwema atatusaidia na kuzidi kuwapaka mafuta viongozi wetu tunawaombea usije na mchana. Hata sasa EBENEZA.
 
Da Radhia labda wewe uko kwenye Tanzania yao sie tulioko Tanzania jua kali tunapambana kujiepusha na hawa baladhuli wanaojifanya viongozi wetu kumbe ni vibaraka wa mabwenyenye na huyu ni mpiganaji shupavu tuko nyuma yake na tutapambana mpaka tone la mwisho kwa hakuna sababu ya kuogopa we cheated death.


Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.
 
Ritz inaelekea hii thread inakunyima usingizi kabisa. Naona kila page ina michango yako kati ya nne na sita. Tafuta walau muda wako binafsi wa kupumzika badala ya kupata pressure humu JF. Kama humpendi Ulimboka si ungesema wazi na yale ya moyoni unayomuombea badala ya kujifanya unamtetea wakati tunajua uliyosema alipotoka mstu wa pande mzima.

Mr. Zero,
Naona comment zangu zimekuchoma sana naona unaangaika ku-copy...mkuu hujue JF kuna hansard ebu weka maneno yangu yeyote ambayo nimefurahi Dr Ulimboka kutekwa ukiweka mie na najitoa JF na usipoweka nakuweka kwenye kundi la Vapour...na nitakutuku PhD ya Umbeya.
 
Last edited by a moderator:
hili jambo lina mambo mengi, moja niwatu kupelekwa ICC, kutokupata matibabu hospitali za nje kwani MaDr wengi wanalielewa rejea british medical journal, kuna UN na diplomasia yao ya kutokupiga kelele, kuna hisia za muathirika wa jambo hili na hatima yake ya baadae, je auze issue au asiuze, majadiliano bado yanaendelea. chochote kile kinaweza kutokea, plus or minus, au plus plus, sasa sitaki kumwaga kuku kwenye mtama kidogo, watapigana
 
Mr. Zero,
Naona comment zangu zimekuchoma sana naona unaangaika ku-copy...mkuu hujue JF kuna hansard ebu weka maneno yangu yeyote ambayo nimefurahi Dr Ulimboka kutekwa ukiweka mie na najitoa JF na usipoweka nakuweka kwenye kundi la Vapour...na nitakutuku PhD ya Umbeya.
hapo kwenye red ulimanisha nini???
 
Tujikumbushe ya Dr Mwakyembe alivyorudi na kusema kuwa anajua ukweli na angesema.... Wazee wakatuliza na wamempa wizara, wametupiga chenga mbili tatu kutusahaulisha... Hamna mtu aliyemtaka tena Mwakyembe aeleze ukweli wa ugonjwa wake... Hii ya Dr Ulimboka is just the same story in different scenario.. Statement yake tu tayari ipo kisiasa "NINAEJUA UKWELI NI MIMI" Kuna nini tena hapo???
 
Bado tanzania hatuna uhuru wa kuongea. Hatuna uhuru kabisaa. Nchi ni kulindana sana. Huyo kala fedha, katulizwa kelele zote zimeisha. Ukweli unajulikana Ikulu hapo hapo maifa salama ndo wamehusika. Anajua yeye wapi, kuna ma intelligencia wa ukweli Tanzania. Jamaa atakuwa katishiwa maisha na familia yake, ndo maana kawa mpole sio hivi. Wana JF, hivi kama ungekuwa wewe umepigwa mpaka hoi bin taaban, ukapelekwa nje kutibiwa, ukirudi na vitisho juu. Utafurah kusema ukweli waki uko hatarini. Chadema wamepeleza na hawawez kulipuka. Na Kova nae kala kona kumzungumzia Huyo Ramadhan. Mwanahalisi chake nae kule. Hali mbaya jaman
 
Kitu kilichotokea Dr.Ullimboka maadui zake sasa hivi wako kwenye mazungumzo nae ndio maana analeta siasa hataki kueleza kilichomtokea usishangae asieleze kabisa au akaeleza story tofauti na ile ya mwanahalisi.Manake maadui zake wanaweza kumweleza bwana samehe yale yalikuwa ni matatizo ya kiufundi wakampa shavu akatulia zake kimya.Ndio maana ameanza kuleta porojo.
Manake hili neno:Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi... limepigwa kiufundi sio ajabu ameambiwa aliseme ili kunarrow ushaidi.

Mmmh huko ni kutokota sasa na si kuchemsha. Sasa kama akipewa shavu akatulia ....what about the money ambayo madaktari wenzake walichanga Tanzania nzima kuhakikisha anapata matibabu na kurudi salama?? What about risk iliyochukuliwa na madaktari wenzake kuji-expose kwenye issue yake? Huo utakuwa ni ubinafsi na siamini mwanamageuzi kama Ulimboka anaweza kukubali hilo shavu. Kama akilikubali hilo shavu basi hana umaana wowote kwa jamii, angebaki huko huko Mwabepande.....sorry that is the truth (That's what we call "USALITI")
 
Huyu Uli nae anazidisha kiza ,si ajabu yakaishia kwenye horizon na kutoweka kwenye thin air !
 
Atasema na wala hatasema kwa kuwa kesi iko mahakamani haisemwi!
 
Huyu Uli nae anazidisha kiza ,si ajabu yakaishia kwenye horizon na kutoweka kwenye thin air !

Tutaishia kusema atasema ila hatasema! Horizon itachukua nafasi yake na habari kupotea bila Khabari. Jambo lolote linakuwa na raha likiwa la motomoto sasa hii habari ni nitasema ukifika wakati muafaka inakuwa kama habari ya kuku na vifaranga kuhusu kunyonya; utanyonya kesho na kesho huwa haipo. Naona kama muda muafaka nao haupo.
 
Hakuna wa kuogopwa zaidi ya Mungu,nidhamu ya uoga na kumsujudia mwanadamu mwenzako ni mbaya na dhambi mbele ya Mungu,walishashindwa kumuangamiza mara ya kwanza sasa ni zamu yao kupata pigo takatifu ambalo familia zao hawataka kuja kusahau


We unacheza na kung'olewa kucha.., lazima atulie sasa... Chezea usalama wewe
 
Hiyo movie ya Dr.Ulimboka STAR wake amezimia.Tusubiri akizinduka tutajua la kumhoji mpaka kieleweke.
 
Ritz inaelekea hii thread inakunyima usingizi kabisa. Naona kila page ina michango yako kati ya nne na sita. Tafuta walau muda wako binafsi wa kupumzika badala ya kupata pressure humu JF. Kama humpendi Ulimboka si ungesema wazi na yale ya moyoni unayomuombea badala ya kujifanya unamtetea wakati tunajua uliyosema alipotoka mstu wa pande mzima.

umeona eeh...
 
Back
Top Bottom