Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

Hivi tunataka aseme ili iweje, kama ni kuandika watu wameadika sana kuhusu Dkt. Ulimboka, kama ni kuhumu tulishahukumu sana humu, sasa tunataka aseme ili itusaidie nini? ukweli uliopo ni kuwa hata akisema leo ndiyo ni serikali unadhani nini kitatokea.

Tuache ushabiki usikua na maana sasa. Kama anataka kusema kama alivyosema atasema, siyo kila siku Uliombo Ulimboka inatia kinyaa sasa.

Well said mkuu!, sijui ni lipi jipya ambalo halijulikani hadi sasa!?? tufanye mambo mengine bwana!
 
Mimi labda sijui maana ya kujichanganya,hebu nisaidieni wadau.
 
mi nilishasema toka mwanzo dk uli kamwe hatosema chochote never.....msiwe kama wageni wa nchi hii bana
 
"Mytake ameshatishwa, maana vyombo vya habari vimekuwa vikimnukuu kauli zake tangu arudi anaonekana kubadilika na kutoihusha serikali tena na sasa anaanza kulaumu media???"

bdo mapema sna kumjudge hvy............ lets give him tym......
 
Well said mkuu!, sijui ni lipi jipya ambalo halijulikani hadi sasa!?? tufanye mambo mengine bwana!

unaeza ukawa unajua kila kitu ila ukawa ni UWONGO............. we need to hear it from the dragons mouth.........

no assumptions nor theories...
 
Je akisema hakuwa na fahamu vyema alipotoka mabwepande?
 
Dk Ulimboka amerudi mpaka sasa hajanena/hajalonga!!!!! hapa msubiri propaganda tu, asije akafa bila kusema chochote kama kesi ya akina zombe,mwenye ukweli alikufa hajasema.
 
endelea kufanya biashara na media DR. magazet yakiweka jina lako tu yanaisha fasta.

Wajinga ndo waliwao..na haongei ng'ooo.!
 
nahisi Dr.Ulimboka unatumika ama kwa kujua au kutojua,hasa magazeti na wanasiasa. Kama hana cha kuongea ni bora angekaa kimya uma uamue,hizi kauli anazotoa mwishoni atajichanganya.!
 
KIONGOZI wa madaktari, Dk Stephen Ulimboka amewataka watanzania wasiwe na hofu na wasubiri siku maalum ambayo ataweka wazi ukweli wote kuhusu namna alivyotekwa na kuteswa, pia hali yake ya kiafya kwa sasa.

Dk Ulimboka ambaye amerejea nchini hivi karibuni kutoka Afrika Kusini alikokuwa amepelekwa kwa ajili ya matibabu alisema jana kuwa hawezi kuzungumza lolote kwa sasa na aachwe apumzike kwani ameugua
na ametengana na familia yake kwa muda mrefu, hivyo anahitaji muda wa kuwa peke
yake.

"Niacheni nipumzike kwa sasa. Wakati muafaka ukifika, nitasema yote. Sitaacha kusema, muda muafaka ukiwadia nitayasema yaliyonitokea na taratibu maalum zitaandaliwa ili nizungumze na watanzania," alisema Dk Ulimboka.

Alisema hawezi kuzungumza bila utaratibu maalum bali atazingatia taratibu zitakazoandaliwa na uongozi wa Jumuiya ya Madaktari (MAT) ndipo ataueleza umma na kusema yaliyo moyoni kuhusu kutekwa
na kupigwa kwake.

"Haya mambo yatawekwa hadharani lakini ni kwa utarartibu maalum, si kama hivi mnavyotaka ninyi.
Kila mtu ananiuliza halafu mnakwenda kuandika ya kwenu, naona hii imekuwa kama biashara sasa,"
alisema.

Aidha Dk Ulimboka alivilaumu baadhi ya vyombo vya habari kwa kuandika habari ambazo si za kweli kuhusu suala la kutekwa na kuteswa kwake na kusema kuwa wamekuwa wakipotosha ukweli wa tukio
lenyewe.

"Wengine wananipigia simu na kunijulia hali, nikiwaambia basi wanaenda kuandika tofauti, kwa mfano juzi wameandika kuwa nimeonekana nikipanda boti, jambo ambalo si la kweli," alisema.

Akizungumzia hilo, makamu wa rais wa MAT, Prinus Saidia alisema Dk Ulimboka kwa sasa yupo mapumzikoni na atazungumza kwa kina baada ya muda mfupi. Alisema madaktari wamekubaliana kuwa Dk Ulimboka aachwe apumzike baada ya kipindi kigumu cha muda mrefu lakini atazungumza kwa undani wakati ambao utakubaliwa na jumuiya hiyo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki za Raia, Siasa na Mwenendo wa Bunge, Marcossy Albanie amesema ataitisha mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumatatu ambapo pamoja na mambo mengine atazungumzia suala la kutekwa na kuteswa kwa Dk Ulimboka.

Albanie hakutaka kuweka wazi ni nini hasa ambacho atakwenda kuzungumzia kuhusu Dk Ulimboka bali alisisitiza kuwa taasisi yake itazungumzia suala hilo la kutekwa na kipigo cha daktari huyo.
 
waandishi makanjanja bwana..sasa amejikanganya wapi???

Wewe ndio kanjanja hujui unalosema wala hujui kulia kwako kutoka kushoto sio lazima ukashifu kama huna point! look at your mouth! it looks as if you didnt suck your mother's milk!
 
Hivi kova mbona yuko kama kokwa???

anapindua pindua semi zake kila kukicha.

yule mkenya vipi sasa kesi yake?:sleepy:
 
Nnachoamini kwa jinsi alivyoponea tundu la sindano,na hali ya vyombo vyetu vya usalama ilivyo anahitaji mda wa kujipanga,ila kama anamawazo tofauti na nnampa pole.

vee mkikuu nya nyanyuu?
 
Uhai na uzima ni kitu kikubwa kitu chochote.Ulimboka atulie.
 
Unamdanganya nani hapa? Mbona viongozi wa Tanzania bado wanapelekwa India? Mbona Watanzania wanaojiweza bado wanakwenda Nairobi? Kikwete ni janga la taifa na madhara ya sera zake zisizo na ruuya yatatutesa kwa miaka 25 ijayo..............

Asilimia 80 ya wagonjwa wanaopelekwa kutibia India ni wananchi wa kawaida.Huu ukweli unaujua au unajifanya haujui but it is a fact.
 
HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, ameibuka toka mafichoni na kuwaambia Watanzania kwamba anayejua mpango mzima wa kumteka, kumtesa na kumpiga ni yeye pekee.

Dk. Ulimboka ambaye juzi alikuwa mafichoni, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusiana na tukio zima la kutekwa, matibabu yake nchini Afrika Kusini na mambo mengine yaliyojiri wakati akiwa nje.

Huku akiwa makini kuchagua maneno, Dk. Ulimboka alisema waandishi wa habari wasiihoji familia yake wala mtu mwingine yeyote, kwani ukweli wa tukio lake anaujua yeye mwenyewe.

Dk. Ulimboka ambaye tangu arejee amekuwa akiishi kwa kujificha, amewataka Watanzania kuvuta subira kwani anajipa muda wa kueleza ukweli wa tukio la kutekwa kwake.

“Najua waandishi wa habari na Watanzania wengi wanataka kujua ukweli ambao ninao mwenyewe, lakini hakuna sababu ya kuwa na haraka, wakati ukifika nitazungumza yaliyonisibu,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari uliolitikisa taifa hivi karibuni, hivi sasa anaishi kwa hofu na kujificha huku akichagua marafiki wa kukutana na kuzungumza nao. Kiongozi huyo, yuko makini pia katika kuzungumza na simu, na amekuwa akipokea zile za watu anaowajua tu.

Alipobanwa ili azungumze kwa ufupi juu ya wanaohusika na kutekwa kwake, Dk. Ulimboka alisisitiza kuwa hayuko tayari kueleza ukweli huo kwa sasa na kuongeza kuwa muda ukifika ataeleza kila kitu.

Polisi wapanga kumhoji

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova ametoa kauli inaonesha kwamba vyombo vya usalama vitamuhoji Dk. Ulimboka.

Kova ambaye alikuwa akizungumza na gazeti hili, lililotaka kujua msimamo wa vyombo vya usalama katika kulishughulikia suala la Ulimboka, hasa baada ya kurejea kutoka kwenye matibabu nchini Afrika Kusini, alisema kwamba taratibu za kipelelezi zitafuatwa.

Wakati Kova akizungumza hayo, chanzo kimoja cha habari toka kwa maofisa wa ngazi za juu wa polisi kilidokeza kuwa endapo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika uchunguzi wake atabaini kuwa kuna shahidi muhimu anahitajika, atahojiwa.

Hata hivyo Kova alisisitiza kuwa; “watu wakipeleleza hawasemi ila tambua tu kwamba taratibu za upelelezi zitafuatwa.”

Tayari taarifa na mwenendo wa tukio zima zinaonesha pasipo shaka kuwa, Jeshi la Polisi katika taratibu zake sasa linafikiria kumuita na kumuhoji Dk. Ulimboka ili liweze kuondoa maneno ya kusikia sikia.

Kuhusu kutajwa tajwa kwa mtu anayedaiwa kuwa ni ofisa wa Usalama wa Taifa wa Ikulu, Ramadhan Ingondhur kuwa alihusika na njama za kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, Kova aliahidi kulizungumzia hilo siku ya Ijumaa.

Mbali na gazeti la MwanaHalisi kumtaja Ramadhan kuwa ndiye mhusika mkubwa wa kutekwa kwa Dk. Ulimboka, mwingine aliyeungana na msimamo huo ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa ambaye aliitaka Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na serikali ithibitishe hadharani juu ya mtu anayetajwa kuhusika na tukio hilo.

Dk. Slaa alisema chama chake kitaanzisha harakati za kutaka kujua ukweli wa nani anahusika kumteka Dk. Ulimboka. Mwanzoni mwa wiki, Dk. Ulimboka alirejea kwa kishindo nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, na kusema yupo tayari kuendeleza mapambano na kazi baada ya kupona kabisa. Dk. Ulimboka alikwenda Afrika Kusini Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya matibabu baada ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 27, 2012.

Aliondoka nchini akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa kwa vile alikuwa kwenye hali mbaya kiafya, lakini alirejea akitembea kwa miguu na kuonekana mwenye afya njema.


Ulimboka waumbue hao.... Kumbe Magazeti yote yalikuwa yanaongea uongo hasa Mwanahalisi kwa mujibu wa Ulimboka
 
Dr Ulimboka ataongea muda ukifika.

Ingawa hii picha ya kihindi inachelewa kuanza, lakini muda wake ukifika picha ya kihindi itaanza tusiwe na haraka.

Tuendelee kumuombea Doctor afya yake iwe nzuri, na atakapoongea aseme ukweli mtupuuuu.
Mwanahalisi nao waliujuwa ukweli 90%, ndiyo maana wakafungiwa, habari walizotoa zilikuwa na details za kutoshaaa, walifanya kazi nzuri sanaaaa, ambayo serikali haikutegemea kutoka kwa wandishi wetu wa Tanzania na pia hawakuogopa kutoa details.
Binafsi nawaamini sana Mwanahalisi kwa hili jambo la Dr Ulimboka.

Doctor Ulimboka tulizana, upone vizuri halafu utakuja siku moja kutuhabarisha, ila ni lazima uwe muangalifu sana, maana serikali this time wakikupata watakuuwa hawatafanya kosa tena kama walilolifanya, watakuchoma moto au watakupiga risasi huo ni ushauri wangu kwa Doctor Ulimboka.

Kwa bahati mbaya sana serikali za kiafrika ni za kishenziiiiiiiiiiiiii sanaaaa, siyo hapa Tanzania, ni Afrika nzima mambo na michezo ni hii hii tuuu, serikali za kiafrika hazitaki kukosolewa wala kuelekezwa.

Nawatakia siku njema

Mkuu acha uongo hapa ni pa Great Thinker sio kule facebook umeskia?

Sasa MWANAHALISI litajuaje ukweli kwa 90% ilhali ULIMBOKA anasema mwenye kuujua ukweli ni yeye pekee na atauweka wazi mbele ya Watanzania? ILA ANGALIA UKWELI WA ULIMBOKA USIJE UKAKUACHA MDOMO WAZI UKAWAOGOPA HAO UNAOWASHABIKIA KWA SIASA ZAO CHAFU
 
Ndugu nimekupa mistari usome ikupe ufahamu, chondechonde Hilo neno ni upanga na ni moto ulao usilidhihaki litakumaliza Zomba.
Queen Esther

WEWE MUNGU NA HARDSHIP ALLOWANCE WAPI NA WAPI?..unatumia mistari ya mungu kuhalalisha mauaji ya wagonjwa wasio na hatia?
 
Back
Top Bottom